Udaku: Ubama kuwasili usiku huu Magogone

Udaku: Ubama kuwasili usiku huu Magogone

TUJITEGEMEE

Platinum Member
Joined
Nov 6, 2010
Posts
27,678
Reaction score
28,793
Ili kuonyesha shukrani zake kwa mkuu Chikwete kwa namna alivyokuwa anamtembelea mara kwa mara ili kumpa mipango ya kujipanga kimkakati mpaka amefanikiwa kuingia ikulu ya Malekane kwa mara ya piri.

Ni mchango wa Chikwete uliowezesha ushindi wa Ubama kwa asilimia 87. Kwa hiyo unaweza kuona umuhimu wa safari hii ya Ubama kwa Chikwete.

Haijajulikana atatumia usafiri gani kufika Magogone maana hata satelite za TB Joshua azijatoa utabiri mpaka sasa, baada ya mitambo yake ya ardhini kuingiliwa na virusi vilivyopotosha utabiri wa awali wa TB Joshua.

Lakini kwa wafukuaji wa habari za ki-udaku wanahabarisha kuwa Ubama atumia dakika 72 kutoa shukrani kwa Chikwete na ataondoka usiku huu kurudi Malekane akitumia usafiri wa drone mpya ilitumiwa na Hesbollah kuipeleleza Israel kwa msaada wa Jamhuri ya Kiislamu ya watu wa Iran.

Source:>>>Vikao vya Wauza Kahawa

UPDATE
=================

kweche: Ubama haji mjini, kabigwa mkwara na Wamachinga.

Valu: Ndiyo maana huwa sikosi kijiwe chako cha kahawa ...stori zako za kuunga huwa zimetulia sana...eeh Mkwara gani
tena wachimba hao nduguzetu wa Chamaki nchanga...!

Fu: Kweche niongeze gahawa nyingine...nasikia Valu kamtaja Chamaka wa Arsenal..hivi Wenger alimuuza mzembe yule!?

Valu: Fu wewe mbao yako kutibua tu...ebu tulia Kweche atupe habari za Wamachinga na Ubama.

Kweche: Valu maasa manne kikombe kimoja tu cha gahawa...poa ..basi bwana yule Bibi aliyetangaza kugeuza maji kuwa
gesi kasema....(anakatizwa na Fu...pamoja na vicheko kutoka kwa wajumbe wengine wa kijiwe hiki)

Fu: Rekebisha kidogo... Bibi aliyetishia kugeuza gesi kuwa maji....(Kweche anadakia)

Kweche: Eeeh..huyo huyo ...kawaagiza wapambe wake wampelekee salaam kuwa endapo Ubama atakanyaga Magogone
ajue kuwa atamrudisha Merekani kwa mguu.

Wajumbe wote wakijiwe: Vicheko, miguno, mayowe ....

Imenibidi nitoke mbio mbio maana nusura jamaa wanimwagie kahawa...
 
Sio kikao cha 'mateja' wala unga??

Vikao vya wauza kahawa vinawajumuisha watu wa makundi mbalimbali na kila mtu anapewa nafasi ya kusikilizwa. hivyo yawezekana habari hii itakuwa imetoka katika kundi ulilotaja.
 
Back
Top Bottom