Uchumi wa viwanda ni tukio au matokeo?

Uchumi wa viwanda ni tukio au matokeo?

Victor Deusfrid

New Member
Joined
May 3, 2018
Posts
2
Reaction score
1
Uchumi wa viwanda ni jina la sera za uchumi na kijamii zinazolenga kupata njia madhubuti katika kuongeza thamani ya bidhaa, mazao na huduma. Uchumi wa viwanda unaunganisha jitihada na mifumo yote inayolenga kuleta maendeleo ya kiuchumi katika eneo husika.

Tukiangalia dhana ya maendeleo na ukuaji wa uchumi ni dhahiri kwamba, maendeleo na ukuaji wa uchumi ni matokea na sio tukio. Ni matokeo yanayojumuisha matukio mbalimbali yanayoshabiihana katika sifa. Mfano, mjasiriamali akifungua kiwanda cha uzalishaji au kutolea huduma kama shule na hosipitali nk mwendelezo wa matukio ya ufunguzi kama hayo yenye nia na lengo moja ndio ulete ukuaji wa uchumi.

Ufunguzi wa kiwanda au viwanda katika sehemu siyo kibali cha kufikia uchumi wa viwanda Bali ni daraja katika mbio za kufikia uchumi huo.

Ufunguzi wa idadi kubwa ya viwanda kama shule mahospitali pia sio kigezo cha kufikia uchumi wa viwanda. Utekelezaji na utimilifu wa malengo ya uanzishwaji ndio utuonesha matokea dhahiri ya kufkia uchumi wa viwanda

Mwendelezo wa uanzishwaji wa viwanda vya huduma na uzalishaji katika maeneo ambayo tayari yalikua na viwanda utupa sura mpya ambayo ni UKUAJI WA UCHUMI au UKUAJI WA VIWANDA ambayo kwa utimilifu wa malengo yake ndipo tunafikia hatua ya UCHUMI WA VIWANDA.

Kuna mambo matatu ya kutumia kutathimini kiwango cha uchumi wa viwanda
#1 pato la taifa GDP
#2 namba ya nguvu kazi katika viwanda
#3 hali ya huduma na utendaji kazi katika viwanda

Hivyo bhasi katika mujumuhisho uchumi wa viwanda ni matokeo ambayo uja taratibu ila kwa kuwekewa nia madhubuti na thabiti.
 
Back
Top Bottom