UCHUMI WA VIWANDA: Mawaziri Wanatosha mpaka nje ya mduara wa Mashaka?

SANCTUS ANACLETUS

JF-Expert Member
Mar 5, 2016
3,337
4,664
Wanauchumi:

Msimamo wangu uko wazi sana juu ya Dira aliyo nayo Raisi Magufuli na uelekeo anaoelekea kuisogelea hiyo Nyota ya Kaskazini ambayo haitui kamwe. Ninamkubali sana Raisi Magufuli isipokuwa katika maeneo machache ya Demokrasia. Sikubaliani na ile Rajua Yake kwamba pale anapoongoza Mwana-CCM ndipo maendeleo yanapopatikana. Mtazamo kama huo ni mtazamo Wa kumdogoesha Mungu wetu katika mambo mawili:
1. Kwamba Mungu wetu ana upendeleo (biased) kiasi kwamba wakati sisi ametuumbia mkondo mmoja tu Wa kutoa Viongozi Wa Nchi, sehemu zingine za Dunia ameumba watu kiasi kwamba yeyote yule anaweza kuongoza Nchi kwa mafanikio kutokea Chama chochote kwa sababu uongozi ni uwezo Wa KIAKILI na sio Suala la nguvu ya Kikundi(Political gathering).

2. Kwamba Mungu wetu ana mipaka ya kiuwezo katika kufanya mambo Yake. Ndio kusema kwamba kwa "Mungu" kutuumba watanzania akiwa ametupatia Option moja tu kuwa kwa kila anayetaka kuonekana Kiongozi mzuri ni lazima ajiunge na CCM basi, Mungu Wa namna hiyo anakuwa ana ukomo katika uwezo wake.

SASA, ukiachana na huo mtazamo( ambao una hizo dosari nilizozianisha) na kama kweli Raisi Magufuli atadumu katika uelewa wa namna hiyo dhidi ya wale wanaostahili kuiongoza Tanzania, maeneo mengine Mimi sina ugomvi naye, mintarafu suala la Rajua ya Uchumi Wa Viwanda.

Juzi nilikuwa na maongezi na Rafiki yangu mmoja ambaye amejitosa kufungua Kiwanda. Amekwisha kuwekeza vya kutosha takribani Bilioni 4. Sasa anasema amekwama katikati na hivi kuhitaji nyongeza ya mtaji kwa ajili ya kununulia Machines za kumwezesha kupata Malighafi kwa wingi na kwa haraka. Katika kufanya hivyo, ameenda Benki ya Kilimo(TADB). Cha ajabu anasema sasa huu ni Mwezi Wa Tatu Benki haina Bodi, chombo ambacho ndio kinahusika na Approval ya Mikopo Mikubwa zaidi ya Milioni 500.

Katika Tanzania, kwa sasa ziko Benki mbili tu zinakopesha mikopo ya Maendeleo. Ukiachana na Benki ya Kilimo(TADB), Benki nyingine ni TIB(Tanzania Investment Bank) ambayo hata hivyo kwa sasa inasemekana kuwa haina Ukwasi Wa kutosha kuwezesha kuhudumia wateja wenye mahitaji makubwa ya kipesa. Katika mazingira kama haya, kiuhalisia Benki moja tu ya TADB inayofanya Kazi ya kusukuma huo Uchumi Wa Viwanda.

Viwanda ni aina ya uwekezaji ambao unachukua muda mrefu mpaka kuanza kutengeneza Faida.Ni kwa sababu kama hiyo Benki za Biashara hili sio eneo lake la Kipaumbele badala yake Benki za Maendeleo ndio eneo lake stahiki.

Hebu sasa tujiulize kidogo: Katika mazingira kama hayo, ambako Raisi Magufuli ameamua kuilekeza Nchi, ni kwa nini Watendaji wake wakuu kama Mawaziri hawaonekani kujali kuielewa Ndoto hiyo? Kuliewa jambo ni kuonekana unaendana nalo. Hivi, kwa Benki kama hii ya Kilimo, kupita miezi mitano wateja wakiwa tu wanasubiria Approval ya mikopo, hivyo Viwanda unakuwa unalenga kuviendeleza au kuviua? Hivi ni nani asiyejua kuwa Benki na Viwanda ni sawa na Mafuta na Gari?

Katika Nchi ambayo Kuna Benki moja tu ya kuhudumia Sekta inayotegemewa kuendesha Uchumi Wa Nchi, inatokeaje kwamba Mawaziri Husika wanaotarajiwa kuteua Wajumbe Wa Bodi wako kana kwamba hawajaapishwa kuchukua majukumu yao?

Hivi kwa kuwa imekuwa kawaida Raisi mpaka aingilie jambo kati ndio wahusika wachukue hatua, Waziri Wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga na Waziri Wa Fedha na wengineo wanaohusika na Utendaji Wa Benki hii mnasubiria mpaka Raisi awakoromee ndio mteue Bodi?

Hivi Chombo kama Bodi inafikiaje muda wake unamalizika na watu hawajui kama muda umeisha na hivi kuanza mchakato wa kuteua Bodi nyingine kabla ya ukomo Wa bodi moja kufika? Je, tuseme Vyombo vinavyohusika na Vetting ya wajumbe viko likizo?

Nimehoji Maswali yote haya kwa sababu hatuwezi katika Nchi kuchochewa moto kwamba tuelekeze macho katika Kutumia Viwanda kufanya Upyaisho Wa Uchumi, kumbe wakati huo huo hatujajiandaa vya kutosha. Hivi Kweli kuteua Bodi kunahitaji Vetting ya miezi na Miezi kama hivi hali inavyosemekana kuwa hapo TADB?

Hivi, kwa miezi hii yote ambayo rafiki yangu anadai amekaa anasubiria Bodi ikae itoe maamuzi dhidi ya Maombi ya Mikopo ya Wateja, Mawaziri husika wanafahamu Nchi imepoteza Kodi kiasi gani na Benki imesinyizishwa kutengeneza Faida kiasi gani na je Ajira kiasi katika Viwanda zingalikuwa zimetengenezwa kwa miezi yote hii?

Anyway, kwa kuwa anayeonekana katika Nchi hii Mwenye macho ya kuona kila kona ni Raisi Magufuli pekee basi, tunampa hiyo siri kwamba huko TADB kuna mkwamo na achukue taarifa vinginevyo Benki inauliwa hivyo na Uchumi Wa Viwanda utabakia ni Wimbo Wa Mtu mmoja tu katika Taifa.

UCHUMI NI AKILI NA WEPESI WA KUTUMIA AKILI
 
Kabla ya kuuliza hayo maswali yako, jiulize:- Anayeteua hiyo bodi ni nani na kwa nini hajaiteua hadi sasa?
 
Back
Top Bottom