Uchumi Unakua,Uchumi Unashuka

Toosweet

JF-Expert Member
May 27, 2012
2,141
1,982
Salaam Wakuu.
Inajulikana kuwa bajeti ya serikali kwa mwaka wa 2016/2017 ni Tsh Trilioni 29.5.Katika hizo 40% ni miradi ya maendeleo na 60% ni matumizi ya kawaida.Wakati serikali inajitapa kukusanya mapato,ukweli ni kuwa haijaweza kumudu kulipa miradi ya maendeleo na matumizi ya kawaida kwa wakati.

Watoa huduma wamelipwa 11Bilioni badala ya 237 bilioni
Wazabuni wamelipwa 49 Bilioni badala ya 906 bilioni
Wakandarasi wamelipwa 365 bilioni badala ya 1.14 trilioni
Walimu wameambulia 46 bilioni. Hii ni mpaka Januari 2017

Kuna sababu za serikali kushindwa kufikia malengo ya bajeti,zinazojulikana ni;
1.Vyanzo vya ndani kutoingiza fedha kama ilivyotarajiwa pamoja na Naibu Waziri wa Fedha Ashantu Kijaju kudai kuwa kuna biashara mpya 139,554 wakati zilizofungwa ni biashara4,183 tu.
2.Washirika wa maendeleo kugoma kutoa fedha kwa asilimia 100
3.Matumizi ya serikali nje ya bajeti iliyopitishwa na Bunge kama vile
-Kuhamia Dodoma
-Ununuzi wa ndege za Bombadier Q400
4.Kutisha wafanyabiashara na sera za kodi zisizo rafiki zinazosababisha biashara kufungwa(tunaona kwenye matangazo ya magazeti kila siku)
Pamoja na haya yote tunaambiwa kuwa uchumi wetu unakuwa na serikali inakusanya mapato zaidi kuliko zamani.
Source: Magazeti na vyanzo vya mbalimbali
 
Back
Top Bottom