Mkuu @ Kyalosangi, heshima kwako. Shida ni zile mbinu chafu za wanasiasa kuhakikisha wanakuwa na agenda zisizoisha kwa mwaka mzima zinazohusisha posho. Kisingizio ni demokrasia gharama. Sasa hv almost ofisi za kawaida za serikali ziko likizo. Unajua kuna ofisi posho tatu za mbunge wa bunge la katiba ni bajeti ya mwezi mzima kuzunguka wilaya nzima! Kibaya ajenda ni bandika bandua wako bize kupanga wanatutawala vp sio wanatuhudumia vp. Niliongea na mbunge mmoja wa zamani aliniambia jinsi wakivokuwa wakiwahenyesha mawaziri wagumu kutoa bahasha kwenye bajeti zao. Nasema hili tuone ugumu mtu kuja kupinguza maslahi makubwa ya wanasiasa ambayo upeo wake unaishia bungeni. Hii wanaita nikune hapa na mi ntakukuna pale!