Uchokozi: Rais Magufuli unajua haya?

Uchokozi: Rais Magufuli unajua haya?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Napongeza juhudi za Serikali ya awamu ya tano ya kupambana na rushwa,ufisadi na uhujumu uchumi. Napongeza pia kukatwa kwa matumizi yasiyo ya lazima ya Serikali. Hongera Rais Magufuli na Serikali yako. Tunazidisha maombi juu yenu.

Lakini,unajua mambo haya? Unajua kuwa TRA na Bandari-TPA ndiko kwenye mizizi ya CCM? Unajua kuwa wanufaika wa huko ni wanufaika wa keki ya Taifa na ni wamwaga sifa kwa chama na Serikali tawala?
Rais Magufuli,unajua kuwa matajiri wa huko ndiyo wapenda chama tawala kuliko hata maskini ambao wao hudanganywa tu wakati wa kampeni?

Rais Magufuli,unajua kuwa matajiri wa TRA na Bandari ndiyo wachangiaji wakubwa wa chama tawala na hata wagombea bora wa chama uchaguzini? Kugusa huko,ni kugusa mfupa wa CCM. Chama kitahisi maumivu muda si mrefu.

Truly,the ongoing reforms and fighting pain the ruling party than anyone else!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
ninawasiwasi mwaka 2020 kazi itakuwepo ndani ya chama,
 
kiukweli sisi wanaccm ndiyo wahanga wakuu wa magufurification, hata yule aliyejitokeza kwenye media juzi akidai chama kimepata afya alikua anajisemesha tu!
 
Damu nzito kuliko maji !! Rais JP Maghufuli fuata roadmap uliyo dhamiria utafika tu.....
Tunakutakia heri.
 
kama mwalimu magufuli akiendelea hivi within six month. CCM nyanganyanga ndembe ndembe chalii
 
Muathirika wa Kasi na utendaji wa Magufuli...

Unatapatapa sana Mzee Tupatupa...
 
Nani atabisha hili kabla hajabisha kwamba ana akili ya kushikiwa.
 
Rais Magufuli, jenga heshima itakayodumu milele?..kwa kweli umewaumbua sana mafisadi pia chunga usije kuchagua vijana wa Kikwete (Nape, January, Mwigulu) kwa kuwapa uwaziri. Hawa wote ni vibaka na puppets wa Kikwete na kama wangechukua nchi wangelinda tu maslahi ya Kikwete na kina Mwinyi na Mkapa. Sasa wanakusifia ni kwa sababu hawana jinsi, walifikiri nawe ungekuwa useless kama JK. Haibu kwao.
 
Ndio wale nyani wawili wa JM walikua wakimshangaa binadamu mwenye mkia akidandia dandia mitaani.
 
MZEE VUTA-NKUVUTE

Wana ccm wenzio hili hawatakubali ila ndio ukweli wenyewe. Faida aliyonayo Magufuli ambayo BMW na JK hawakuwa nayo ni kwamba JPM hakushiriki kwenye mikutano na harambee za kuchangia chama fadha za kampeni.
Hilo linampa wepesi wa kusema NO!!! Wachangiaji wengi wanajulikana kwa January na Abrahman tu.....

Kwa nini msimshauri mzee wa Msoga kuachia uenyekiti ili kuepusha mgongano wa personalities???

Ila kusema kweli ccm mnaisoma namba,
 
Last edited by a moderator:
Sasa hivi unaelekea kuwa mzee tapatapa wa lumumba na sio tupatupa,

Mwacheni Rais wetu afanye kazi
 
MZEE VUTA-NKUVUTE

Wana ccm wenzio hili hawatakubali ila ndio ukweli wenyewe. Faida aliyonayo Magufuli ambayo BMW na JK hawakuwa nayo ni kwamba JPM hakushiriki kwenye mikutano na harambee za kuchangia chama fadha za kampeni.
Hilo linampa wepesi wa kusema NO!!! Wachangiaji wengi wanajulikana kwa January na Abrahman tu.....

Kwa nini msimshauri mzee wa Msoga kuachia uenyekiti ili kuepusha mgongano wa personalities???

Ila kusema kweli ccm mnaisoma namba,

Eti Magufuli anaifanyia ccm yale ya Nyoso alafu ccm inadai eti inafurahia!! Hahahaaa! Huu c ni ushoga jamani?
 
Last edited by a moderator:
Vyombo vyote vya habari dunia nzima zinapozungumzia jitihada za dhati za kuondoa rushwa katika bara la afrika lazima walitaje jina la MAGUFULI (P.H.D. HONS) , Tumuombee Mungu ambariki aweze kutimiza majukumu yake, na nafikiri katik dunia kuna watu wanaweka historia ya kudumu basi na DOCTOR JPM ataiweka.
 
Hongera sana Raisi kwani ww ni mkweli na unajua unachokitenda ucjali kwani hapa Duniani wote tunapita tu, tenda wema hapa duniani akhera ni mahesabu, wananchi tumekukubali sana kwani ww ni mtu wa kipee sana katika kuwatetea wanyonge ss tutakuombea kila kukicha kwa Allah akupe nguvu,afya na maisha marefu,anaekuombea mabaya bac limfike mwenyewe.
 
kuna watu (sijui tuite watoto) hapa jukwaan kazi yao kubwa kubisha tu.....

ivi nan hajui km wanaoguswa huko bandarini na TRA ni ccm damu damu?? nani hajui km hao ndo wanaofanya ccm ipate jeuri ya pesa??

nyie watoto mlioko humu jifunzeni, sio lazima kila uzi mchangie.....
 
Achana mambo ya chama chenu hicho, sisi wengine hatuna vyama,kwetu Tanzania kwanza.
JPM kanyaga twende.
 
Ukweli hua unauma na huo ndo ukweli kua ccm inapitia wkt mgumu nw
 
Back
Top Bottom