Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,742
- 40,873
Ni nini kitatokea sasah ivi endapo wabunge wote wa upinzani (kutoka vyama vyote) wakaamua kujiuzulu Ubunge, kujiunganisha chini ya chama kimoja na kugombea tena katika uchaguzi mdogo?
1. Wapinzani watapata jukwaa kubwa la wakati mmoja la kufanya siasa nchi nzima (kupitia kampeni)
2. Chini ya chama hicho kimoja (siyo dubwasha la UKAWA) wataweza kusimama na ajenda moja ambayo wanaweza kuiuza nchi nzima.
3. Wataenda kupima mbele ya wananchi sasa hivi jinsi gani ajenda ya mabadiliko inayoendeshwa na Magufuli inakubalika. Wapo wanaoamini (miongoni mwa wabunge hawa) kuwa Magufuli hakubali na utawala wake ni wa kibabe na hivyo wananchi wengi wanaliona hili na wakipewa nafasi watatoa adhabu kali kwa Magufuli.
4. Wataweza kuuza ajenda mbalimbali kwa wananchi na watakuwa na uhuru mkubwa wa kujadili mambo.
5. CCM italazimisha kusimamisha wagombea wengine kwenye majimbo hayo na wananchi watapewa nafasi ya kuwakataa wagombea hao.
6. Itakuwa ni nafasi muaka ya kupima ni jinsi gani wamejiandaa kushinda chaguzi kwa kutengeneza mifumo ya kulinda na kusimamia kura za ubunge kabla ya 2020; na wabunge hawa wakishinda tena itakuwa ni rahisi sana
7. Watalazimisha mgogoro wa kikatiba; endapo wabunge wote wa kuchaguliwa wa upinzani wakijiuzulu je wale wabunge wa viti maalum ambao wanaingia kwa kupitia kanuni ya idadi ya wabunge wa kuchaguliwa wataendelea kuwa wabunge; na wakichaguliwa wengine kutoka chama hicho kimoja je Tume italazimika kutoa nafasi mpya za wabunge wa kupitia viti maalum?
Na mengine mengi..
Huu ni uchochezi wa aina yake.