Uchochezi wa viongozi wa dini dhidi ya wananchi.

Uchochezi wa viongozi wa dini dhidi ya wananchi.

Status
Not open for further replies.

T.Ramla

Member
Joined
Mar 29, 2013
Posts
6
Reaction score
0
Kuna kauli nyingi za uchafuzi wa hali ya amani unaoendelea hapa nchini ambao unaendeshwa na viongozi wa dini, kama ule uliotolewa na Sheikh ILUNGA KAPUNGU wa kitio cha Thaaqib Islamic Centre cha jijini Mwanza, Kwamba Bakwata ni tawi la kanisa, Muislamu rudisha heshima ya uislamu na nyenginezo. Ikiwa Mwenyezimungu anatuambia tushikamane wala tusifarakane jee huu sio mfarakano? Ambao utakaoweza kutugawa na kutuvuruga ili tusitambuane, Vile vile tunaambiwa mfitinishaji makaazi yake ni Motoni. Jee kwa uchochezi huu hautopelekea kufarakana?Vile vile uchochezi mwengine ni ule uliotolewa na Askofu AGUSTINE MPEMBA wa Kanisa la Tanzanian Field Evangelist la Mwanza, unaosema “Inuka chinja ule” Jee inamaana kama nikikaa sikuchinja sitokula, huu ni uchochezi na kutaka kumwaga damu kwani hata kwenye Biblia katika amri kumi za mungu tumekatwazwa tusiue. Jee kiongozi kama huyu amri za Mungu anazifuata kweli au tunamfuata tu kwakufuata matamanio yake?Viongozi kama hawa tukipigana wao wanakuwa mbali na mji na wala hawasogei kabisa. Tuwe na akili.Tuwasikilize viongozi wetu wa dini kwayale mema wanayotufunza sio kwa maovu, tutakwenda kuulizwa hamkuwa na akili?TAFAKARI
 
Sasa na wewe umeleta topic...! nadhani haifiki saa 5 itakuwa imeshafutwa..!
 
I am not biased, lakini mleta thraed hakumuelewa mchungaji, alimaanisha kuchinja kitoweo, sio watu.
 
Hizo CD za Dr / Sheikh Ilunga kama unazo zoote zisikilize mwanzo mwisho ndio utajua kuwa BAKWATA ni tawi la kanisa ama sio....

Bahati nzuri sana hizo CD zoote ninazo na Sheikh Ilunga alichokieleza wala sio uchochezi na wala Sheikh Farid anachowaeleza Wazanzibar wala sio uchochezi kabisaaa.... Kuna UNAFIKI unaendelea hapa Tanzania na madhara yake ni makubwa sanaaaa...yaani dini moja kutenda mambo kana kwamba wao ndio Watanzania daraja la kwanza na akitokea mtu kuumbua mfumo huo anaitwa mchochezi na mvurugaji Amani....

Mnaficha moto kwa mikono eeenh, Subirini sasaaaa !
 
Mimi huwa nashindwa kumpa grade.
Hivi yule ni Sheikh Ilunga au Dr. Ilunga au Profesa Ilunga au Senior Lecturer Ilunga au ??. sipati jibu.

Mwaka 1995 niliwahi kuhudhuria semina yake pale Bihawana sekondari na akawa na mada ya mabadiliko ya ukuaji wa mtoto tumboni kwa kila baada ya miezi mitatu huku akilinganisha ushahidi wa kitabu cha waislam Qur'an na Sayansi. Kwa kweli baada ya hapo nilifuatilia na kukuta kila alichokisema kilikuwa ni sahihi kabisa kabisa kabisa.

Tokea hapo amekuwa mentor wangu. Namuamini kwa yote anayoyasema. Yana uchambuzi wa kina.
Ndio maana wapinga ukweli wnamuona mchochezi.
Wayahudi walimuona Yesu pia mchochezi na wakamfanyia fitina.

Haijalishi: Pengine hayo ndiyo walioandikiwa walio-karibu na Mungu mwenyezi.

Sasa wewe tafakari ikiwa unamchukia Profesa Ilunga nacheleya utakuwa mbali na Mungu. Msikilize, fuatilia, utaona ukweli wa mnyamwezi wa mtaa wa isike.
 
Hizo CD za Dr / Sheikh Ilunga kama unazo zoote zisikilize mwanzo mwisho ndio utajua kuwa BAKWATA ni tawi la kanisa ama sio....

Bahati nzuri sana hizo CD zoote ninazo na Sheikh Ilunga alichokieleza wala sio uchochezi na wala Sheikh Farid anachowaeleza Wazanzibar wala sio uchochezi kabisaaa.... Kuna UNAFIKI unaendelea hapa Tanzania na madhara yake ni makubwa sanaaaa...yaani dini moja kutenda mambo kana kwamba wao ndio Watanzania daraja la kwanza na akitokea mtu kuumbua mfumo huo anaitwa mchochezi na mvurugaji Amani....

Mnaficha moto kwa mikono eeenh, Subirini sasaaaa !

Ilunga hajawahi kuwa sheikh
 
katika jamii kuna watu wa aina zote kuna wenye upeo mkubwa wa kuchambua, kutafsiri na kutafakari mambo kwa haraka hivyo uelewa sana mambo mengi , pia kuna watu wenye upeo wa kati hawa uelewa hawa uelewa kwa wastani tu lakini pia kuna watu wenye upeo mdogo, watu hawa ni wengi sana ndani ya jamii huwa wanapokea mambo kwa haraka bila kuyafanyia uchunguzi huwa wanawategemea viongozi wao wa serikali ya mitaa, madiwani, wabunge, mabalozi wao na viongozi wao wa dini kuwaongoza kwa kila jambo. kwa mantiki hiyo viongozi hawa wanatakiwa kuwa makini sana wanapokuwa wanatoa matamko, maamuzi,ushauri kwa watu wanaowaongoza kwa sababu kwa namna moja au nyingine wamekuwa wakileta malumbano ndani ya jamii hali ambayo inapelekea watu wanashindwa kufanya shughuli zao za kimaendeleo hivyo kushiriki katika mambo ambayo hayana faida kwao.

mfano baadhi ya viongozi wa dini wanawaalika wanasiasa na vinongozi wa serikali katika harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya jambo furani lakini viongozi hao hutumia sehemu hizo kutoa kauli ambazo zinajenga jazba, chuki na mifarakano badala ya kutumia sehemu hizo kuhamasisha umoja , amani na mshikamano wa watanzania kitu ambacho ndio utamaduni wa taifa letu. tukumbuke viongozi hawa wa kisiasa na kidini panapotokea machafuko huwa hawajitokezi kutetea waumini hao bali wanakimbia wao na familia zao. je wewe familia yako umeiandalia nini? pakitokea machafuko? ukiangalia nchi zenye machafuko hata siku moja huwezi kuona kiongozi wa dini anawatetea waumini wake na wala huwa hawaonekani si viongozi wa dini wala siasa , mara nyingi wanawake na watoto ndio huwa waathirika wakubwa katika machafuko, jamani tuache itikadi zozote tujenge umoja wetu taifa letu tusitegemee mtu atoke nje aje ndani kutuambia kwamba uchochezi wa kidini ni hatari kwa taifa letu. tafakari tumetoka wapi?, tupo wapi? na tunafanyaje kutoka hapa?.................!
 
Usisahau udini unaochochewa na Joseph Selasini mbunge wa Rombo!

Huyu ndiye aliyefungua mlango wa kupeleka CD "zenye uchochezi wa kidini" bungeni! na Muislamu naye akileta CD au nyaraka za uchochezi wa kidini wa Wakristo zisikataliwe bungeni! lawama zote ashushiwe Selasini aliyeufungua huu mlango wa shari.

*Nilitayarisha nukuu za kitabu cha Sivalon na kumpatia Mbunge (kupitia mtu wa kati) ninayemjuwa aipeleke bungeni kama ushahidi wa udini wa nyerere ndio ulioifikisha Tanzania hapa amekataa.
 
Hizo CD za Dr / Sheikh Ilunga kama unazo zoote zisikilize mwanzo mwisho ndio utajua kuwa BAKWATA ni tawi la kanisa ama sio....

Bahati nzuri sana hizo CD zoote ninazo na Sheikh Ilunga alichokieleza wala sio uchochezi na wala Sheikh Farid anachowaeleza Wazanzibar wala sio uchochezi kabisaaa.... Kuna UNAFIKI unaendelea hapa Tanzania na madhara yake ni makubwa sanaaaa...yaani dini moja kutenda mambo kana kwamba wao ndio Watanzania daraja la kwanza na akitokea mtu kuumbua mfumo huo anaitwa mchochezi na mvurugaji Amani....

Mnaficha moto kwa mikono eeenh, Subirini sasaaaa !

kama unaona hakuna uchochezi wa farid na ilunga inatosha kusema your nt normal
 
Ila akisema Askofu Pengo ni sawa kwa kila kitu...... Nimekuelewaaa !

nini pengo hata angekuwa pope kama anafanya vitendo vya kihuni na kigaidi lazima sheria ifuate mkondo wake sio kisa eti huyu mwezetu au kiongozi wetu ndio tuelee upuuuzi na wapuuzi kama hao, hao ni kifungo tu
 
Kama ni mjadala basi msipaniki, sie wengine tusiopenda majibu ya kihuni tunawafuatilia
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom