VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Tangu kuingia madarakani, Rais Magufuli hakusafiri kwenda Amerika, Ulaya au Asia. Kwa mujibu wake, 'anasafisha' kwanza nchi humuhumu ndani. Rais Magufuli amebaki nchini, achilia mbali kwenda Kenya, Uganda na Rwanda. Ni hapa hapa kwanza hadi kunyooke na kusafishika.
Kama alivyo Rais, Mwenyekiti-wa-Msajili wa CUF, Prof. Lipumba naye amekuwa wa kubaki Ofisi za CUF Buguruni tu. Tangu atambuliwe na Msajili kufuatia kujiuzulu na 'kurejea kwake madarakani', Prof. Lipumba hakuwahi kuvuka bahari na kwenda Zanzibar ambapo CUF ina nguvu hasa.
Ilitegemewa, kwakuwa ndiye Mwenyekiti-wa-Msajili halali, Prof. Lipumba angekwenda Zanzibar na mikoa mingine kutamba mikutanoni katika kujenga na kuimarisha CUF yake. Kwanini Mwenyekiti asitambe na CUF yake atakavyo? Au naye,kama Rais Mafuguli, bado anasafisha CUF yake akitokea Buguruni? Amakweli, ukistaajabu ya ACT-Wazalendo, utayaona na CUF!
Kupima mkojo na uchochezi wapi na wapi!?
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kibiti, Pwani)