Habari;
Nianze kwa kuweka kumbukumbu sawa kila mtu anao uwezo wa kufanya uchawi au kuwanga.
Uchawi sio kipaji cha kipekee bali ni uwezo tu ambao ukiuendeleza na kuuendekeza unaweza kuwa very addictive na ukakukosanisha na jamii.
Uchawi ni nini;uchawi ni uwezo wa mtu kufanya mambo ambayo katika hali ya kawaida ama hayawezekani au yanahitaji nyenzo nyingine lakini ye hufanya kwa kutumia namna na njia mabayo sio rahisi kuelewa ispokuwa tu kama una uwezo huo.
Kwa kawaia na kwa mujibu wa historia wachawi wengi huwa wansifikia kwa kufanyia watu mabaya.Sababu kubwa ya wachawi kufanya mabaya ni kwa sababu ya urahisi wa kufanya ubaya kwa kutumia uchawi kuliko kutumia njia za kawaida tulizo zoea
Mfano ukinikosea naweza kukupa adhabu ya kawaida lakini wakati mwingine kutokana na hali na nafasi yako inakuwa ngumu basi hapo ndipo nguvu ya uchawi hutumia.
Wengi wetu tumewahi fanyia watu ulozi ila kwa kuwa hatukuwa tukiitazama hali hiyo kwa jicho la tatu hatukujua kuwa labda tumeshaumiza mtu bila hata kumgusa.
Uwezo huu wa kichawa unaweza kujifunza na kuwa mzoefu ila unahitaji kuwa mvumilivu na mara nyingi watoto ni rahisi kufundishwa ulozi kuliko watu wazima kwasbb ya wao kuwa innocent
Hivyo basi unaposikia habari za wachawi basi jua hata wewe ni mchawi
Mjadala uko wazi