Hivi haya niliyoyasikia asubuhi hii kwenye vichwa vya habari vya magazeti kuhusu mikopo ya elimu ya juu ni kweli?Kama ni kweli hivi hiyo bodi ya mikopo inataka wanafunzi wa nchi hii wakatafute wapi hawa wafadhili zaidi ya serikali yao.Mimi sijui viongozi wa nchi hii wanafikiri wao watakuwa kwenye uongozi milele.Hivi taifa hili litakuwa na viongozi wajinga siku zijazo maana kuna muelekeo wa kuwanyima wananchi wa nchi hii yenye jamii kubwa ya wakulima elimu ya juu ili iwe ya kifalme maana wao ndiyo wana uwezo wa kuwalipia watoto wao elimu ya juu.
Hivi hizi kodi zetu zinashindwa kuwakopesha watoto wetu ila kuziingiza kwenya akaunti za mafisadi na kufadhili mikataba feki ni sawa tu.Hivi rasilimali za nchi hii ni mali yetu sote au ni za baadhi ya watu.Kwa mtaji huu tunatengeneza bomu ambalo litakapolipuka itakuwa nchii hii haikaliki.