Uchambuzi Wa Habari: Tunafanyaje na Naibu Spika Tulia Ackson?

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
Ndugu zangu,

Swali hili lilipaswa wajiulize Wabunge wa upinzani wenye kutoka Bungeni kila baada ya dua ya asubuhi.

Kwa kufuatilia kwangu siasa za nchi hii na dunia, na kwa kuyaangaalia mahitaji ya wananchi kwa sasa, naona mkakati huu wa wabunge wa upinzani ni wa kimakosa.Ni mkakati utakaokuwa na gharama zaidi kwa wapinzani huko tunakokwenda kuliko Chama cha Mapinduzi chenye wabunge wengi Bungeni.

Unapopanga kulifanya jambo ni vema ukatafakari pia matokeo ya jambo husika. Kwa sababu za kibinadamu, ikiwamo kupandwa na jazba na mengineyo, wapinzani kutoka Bungeni siku ile ya kwanza baada ya mtafaruku kuanza ingeeleweka kwa wapiga kura. Lakini, kwa kuendelea kwao kutoka kila asubuhi ya siku ya kazi za Bunge walizotumwa na wapiga kura kwenda kuzifanya inaanza kujenga hisia miongoni mwa Watanzania, mimi mmojawapo, kuwa huko ni kukosekana kwa umakini.

Niliangalia Bunge lilipoanza jana asubuhi na hakika nilisikitika moyoni. Naamini, siko peke yangu, maana, hayo si matarajio ya Watanzania kuwa na wabunge watakaokuwa wakichaguliwa na kufanya mambo kama yale. Kama nchi, hakuna namna yeyote ya kuikimbia mifumo na kanuni tulizojiwekea. Haina mashiko, hoja ya kumkataa mtu katika nafasi yake na ambaye hajafanya lolote linalomtaka ang'atuke kwa mujibu wa kanuni, sheria na taratibu zetu kimfumo.

Yanapotokea mapungufu ya kimfumo ndani ya kanuni, sheria na taratibu zetu mahali pekee kwa kuanzisha jitihada za kuyabadili hayo ni ndani ya Bunge au Mahakamani. Si kwenye viwanja vya Bunge. Na kwa ilivyo sasa hakuna namna, Wabunge wanaotoka itafika siku itawalazimu wabaki tu ndani ya Bunge na Naibu Spika huyo huyo. Tatizo hapa watakuwa wamepoteza muda mwingi nje ya Bunge badala ya kuwa ndani na kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi kupitia Bunge.

Hii ni Nchi Yetu sote. Iko siku wapinzani ndio watakaounda Serikali na Spika au Naibu Spika atatoka miongoni mwa wapinzani wa sasa.
Kama wabunge wa CCM watafanya haya ya kutoka bungeni kwa vile tu hawatampenda au kumtaka Spika, basi, kwa namna hii hii, tutawashutumu wabunge hao wa CCM kwa wakati huo.

Maggid Mjengwa,
 
Sidhani kama wanatoka kwa hiyo hoja moja tu. Mimi naona kama bunge linasimamiwa na serikali badala ya serikali kusimamiwa na bunge. Haya tunayosimuliwa ubaya wake jioni tulipaswa kujionea wenyewe live kama zamani. Kulikoni tusilione bunge?
 
Ukitaka kujua nguvu ya upinzani nchi hii, waambie CCM na dikteta wao waruhusu mikutano ya hadhara ya wapinzani. Na ili kumfanya Naibu Spika aendelee kukomaa hapo kwenye kiti ni kumuongezea pampas tu ili asiende hata kujisaidia.
 
Aliteuliwa kuwa mbunge wa viti maalumu, anafanya kazi maalumu, kwa ajili ya mambo maalumu, na kwa watu maalumu,ataimaliza kazi hiyo ktk kipindi maalumu na ataondoka ktk wakati maalumu!.
pilipili hilo ndilo jibu haswa na wanajf na Watanzania kwa ujumla wetu tunapaswa kujadili hili. Good stream, I loved it
 
Ndugu zangu,

Swali hili lilipaswa wajiulize Wabunge wa upinzani wenye kutoka Bungeni kila baada ya dua ya asubuhi.

Kwa kufuatilia kwangu siasa za nchi hii na dunia, na kwa kuyaangaalia mahitaji ya wananchi kwa sasa, naona mkakati huu wa wabunge wa upinzani ni wa kimakosa.

Ni mkakati utakaokuwa na gharama zaidi kwa wapinzani huko tunakokwenda kuliko Chama cha Mapinduzi chenye wabunge wengi Bungeni.

Unapopanga kulifanya jambo ni vema ukatafakari pia matokeo ya jambo husika. Kwa sababu za kibinadamu, ikiwamo kupandwa na jazba na mengineyo, wapinzani kutoka Bungeni siku ile ya kwanza baada ya mtafaruku kuanza ingeeleweka kwa wapiga kura.

Lakini, kwa kuendelea kwao kutoka kila asubuhi ya siku ya kazi za Bunge walizotumwa na wapiga kura kwenda kuzifanya inaanza kujenga hisia miongoni mwa Watanzania, mimi mmojawapo, kuwa huko ni kukosekana kwa umakini.

Niliangalia Bunge lilipoanza jana asubuhi na hakika nilisikitika moyoni. Naamini, siko peke yangu, maana, hayo si matarajio ya Watanzania kuwa na wabunge watakaokuwa wakichaguliwa na kufanya mambo kama yale.

Kama nchi, hakuna namna yeyote ya kuikimbia mifumo na kanuni tulizojiwekea. Haina mashiko, hoja ya kumkataa mtu katika nafasi yake na ambaye hajafanya lolote linalomtaka ang'atuke kwa mujibu wa kanuni, sheria na taratibu zetu kimfumo.

Yanapotokea mapungufu ya kimfumo ndani ya kanuni, sheria na taratibu zetu mahali pekee kwa kuanzisha jitihada za kuyabadili hayo ni ndani ya Bunge au Mahakamani. Si kwenye viwanja vya Bunge. Na kwa ilivyo sasa hakuna namna, Wabunge wanaotoka itafika siku itawalazimu wabaki tu ndani ya Bunge na Naibu Spika huyo huyo. Tatizo hapa watakuwa wamepoteza muda mwingi nje ya Bunge badala ya kuwa ndani na kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi kupitia Bunge.

Hii ni Nchi Yetu sote. Iko siku wapinzani ndio watakaounda Serikali na Spika au Naibu Spika atatoka miongoni mwa wapinzani wa sasa.
Kama wabunge wa CCM watafanya haya ya kutoka bungeni kwa vile tu hawatampenda au kumtaka Spika, basi, kwa namna hii hii, tutawashutumu wabunge hao wa CCM kwa wakati huo.

Maggid Mjengwa,

Huyo NAIBU SPEAKER....Mhhhh. Halafu, kwani Speaker mwenyewe yuko wapi?
 
Ndugu zangu,

Swali hili lilipaswa wajiulize Wabunge wa upinzani wenye kutoka Bungeni kila baada ya dua ya asubuhi.

Kwa kufuatilia kwangu siasa za nchi hii na dunia, na kwa kuyaangaalia mahitaji ya wananchi kwa sasa, naona mkakati huu wa wabunge wa upinzani ni wa kimakosa.Ni mkakati utakaokuwa na gharama zaidi kwa wapinzani huko tunakokwenda kuliko Chama cha Mapinduzi chenye wabunge wengi Bungeni.

Unapopanga kulifanya jambo ni vema ukatafakari pia matokeo ya jambo husika. Kwa sababu za kibinadamu, ikiwamo kupandwa na jazba na mengineyo, wapinzani kutoka Bungeni siku ile ya kwanza baada ya mtafaruku kuanza ingeeleweka kwa wapiga kura. Lakini, kwa kuendelea kwao kutoka kila asubuhi ya siku ya kazi za Bunge walizotumwa na wapiga kura kwenda kuzifanya inaanza kujenga hisia miongoni mwa Watanzania, mimi mmojawapo, kuwa huko ni kukosekana kwa umakini.

Niliangalia Bunge lilipoanza jana asubuhi na hakika nilisikitika moyoni. Naamini, siko peke yangu, maana, hayo si matarajio ya Watanzania kuwa na wabunge watakaokuwa wakichaguliwa na kufanya mambo kama yale. Kama nchi, hakuna namna yeyote ya kuikimbia mifumo na kanuni tulizojiwekea. Haina mashiko, hoja ya kumkataa mtu katika nafasi yake na ambaye hajafanya lolote linalomtaka ang'atuke kwa mujibu wa kanuni, sheria na taratibu zetu kimfumo.

Yanapotokea mapungufu ya kimfumo ndani ya kanuni, sheria na taratibu zetu mahali pekee kwa kuanzisha jitihada za kuyabadili hayo ni ndani ya Bunge au Mahakamani. Si kwenye viwanja vya Bunge. Na kwa ilivyo sasa hakuna namna, Wabunge wanaotoka itafika siku itawalazimu wabaki tu ndani ya Bunge na Naibu Spika huyo huyo. Tatizo hapa watakuwa wamepoteza muda mwingi nje ya Bunge badala ya kuwa ndani na kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi kupitia Bunge.

Hii ni Nchi Yetu sote. Iko siku wapinzani ndio watakaounda Serikali na Spika au Naibu Spika atatoka miongoni mwa wapinzani wa sasa.
Kama wabunge wa CCM watafanya haya ya kutoka bungeni kwa vile tu hawatampenda au kumtaka Spika, basi, kwa namna hii hii, tutawashutumu wabunge hao wa CCM kwa wakati huo.

Maggid Mjengwa,

Uchambuzi makini kwa watu makini. Hawa wanamiavuli wa UPAWA sorry UKAWA wakubali makosa ili tujenge nchi. Mtu mzima ukikosea si zambi na asiyekubali kushindwa si mshindani. Mbowe waruhusu wenzako wakatoe michango yao bungeni kwani wengi ni wageni wanaogopa. Siasa sio uwamuzi kama unaoufanya kwenye familia yako. Ulionayo ni zaidi ya familia acha maamuzi ya kiimla yatakugharimu na kudhoofisha upinzani nchini.
 
..suluhisho ni Tulia kutokuongoza vikao vya bunge.

..anachofanya sasa hivi ni kuwakomoa wananchi waliochagua wabunge wa upinzani.

..watu wazima wanapaswa kumshauri Dr.Tulia kujiweka pembeni ili shughuli za bunge ziendelee.
 
Kama ndivyo hata nyie mnaotoka si watu maalumu, hamjatoka katika kipindi maalumu tafuteni wakati maalumu wa kufanya haya sio sasa. Huu ni muda maalumu wa kujenga nchi
Kama kingozi mmoja anasema dawa ya kuwathibiti wapinzani ilikwenda kutafutwa
Nje ya nchi na aliyemteua Tulia Je unategemea nini hapo? Watoke wakae yote sawa kwani kwa vyovyote hatawasikiliza. Kwani hakuna yeyote aliyeipinga.

wa achosema
 
Taratibu mtaelewa tu kadri siku zinavyokwenda! Ukiona mtu anaanza kuingiza dawa za kichawi tena ni kufilisika kimawazo huko. Tujenge nchi wadau tuache ngonjera
 
Aliteuliwa kuwa mbunge wa viti maalumu, anafanya kazi maalumu, kwa ajili ya mambo maalumu, na kwa watu maalumu,ataimaliza kazi hiyo ktk kipindi maalumu na ataondoka ktk wakati maalumu!.
Huwezi kushtaki alafu ukaweka shinikizo ushinde kesi, wao wangeendelea na vikao bungeni wakati wanasubiri hatma ya mashtaka, istoshe sisi hatujawatuma kufanya haya wanayoyafanya, sisi haki yetu kama waajili wao iko wapi? wanajadili bajeti nje ya bunge wamamuwakilsha nani? Je minits za vikao vyao vinasaidia nini kama haziko kwenye ansadi za Bunge? Ni watu wazima hovyo kabisa
 
Uchambuzi makini kwa watu makini. Hawa wanamiavuli wa UPAWA sorry UKAWA wakubali makosa ili tujenge nchi. Mtu mzima ukikosea si zambi na asiyekubali kushindwa si mshindani. Mbowe waruhusu wenzako wakatoe michango yao bungeni kwani wengi ni wageni wanaogopa. Siasa sio uwamuzi kama unaoufanya kwenye familia yako. Ulionayo ni zaidi ya familia acha maamuzi ya kiimla yatakugharimu na kudhoofisha upinzani nchini.
ushauri mzuri, mshauri hata huyo naibu awaruhusu hao wapinzani wafanye kazi zao sawa na wabunge wa ccm. kibaya zaidi na bunge limefichwa hata hatuoni kinacho endelea.
 
Historia itamuhukumu, Mungu hashindani na mtu Muovu hata siku moja.
 
Back
Top Bottom