Uchambuzi: Ni ngumu Yanga kukwepa kipigo toka kwa Mnyama

Baba Kiki

JF-Expert Member
May 31, 2012
1,544
943
Kuelekea 'big match' ya michuano ya kombe la mapinduzi katika hatua ya nusu fainali itakayofanyika kesho Jumanne Januari 10, 2017, uchambuzi huu unaonesha kuwa itakuwa ni ngumu sana Yanga kuepuka kupigo kutoka kwa mtani wake wa jadi Simba.

Hadi majira ya usiku wa saa nne na nusu, kama mambo yatakwenda kama yalivyopangwa, umma wa wapenda michezo ndani na nje ya Tanzania utakuwa umeshajua nani ni nani watakaokutana na mshindi kati ya Azam ya Dar es Salaam na Taifa Jang'ombe ya Unguja.

Mechi hii ya nusu fainali ya watani wa jadi wa soka la Tanzania kati ya Simba ambao ni wababe wa kihistoria wa kombe la mapinduzi na Yanga ambayo imeshawahi kutwaa ubingwa huu mara moja tu, inatarajiwa kuwa kali na yenye ushindani mkubwa katika kila eneo la ndani na nje ya uwanja, hasa kutokana na namna ilivyokuja 'ghafla' ambapo timu zote zina siku moja tu ya kujiandaa.

Katika kukuchambulia mchezo huu, tumezingatia mambo matatu ambayo yanaonekana kuinufaisha Simba na hivyo kutoa uelekeo wa Yanga kulala mapema hiyo kesho. Mambo haya matatu (three factors) ni uimara wa vikosi, ufundi/mbinu na morali ya timu.

Tukianzia na uimara wa vikosi, Simba inaonekana kuwa timu iliyokamilika zaidi katika michuano hii kwa kuwa na kikosi imara, kipana, chenye uwiano mzuri na kilichoanza kuzoeana vizuri. Tutafafanua!

Licha ya kuonekana kufunga magoli machache, Simba imeonekana kuwa imara sana pengine kuliko timu zote katika eneo la kiungo, lakini pia ikiwa na defensi bora na hata safu ya ushambuliaji yenye kasi kubwa. Kuipasua ngome ya Simba chini ya mlinzi shupavu Method Mwanjale, Abdi Banda, Mohamed Hussein 'Tshabalala' na Mkongo Besala Bokungu, na kisha kupita golini kwa Daniel Agyei, ni moja kati ya kazi ngumu mno inayoweza kufanywa na aina ya washambauliaji walionekana katika michuano hii. Hadi sasa Simba imelazimika 'kujifunga' yenyewe ili kuipatia timu pinzani goli.

Katika uchambuzi huu hatuizungumzia safu ya kiungo ya Simba ambayo hakuna kocha yeyote katika ukanda huu asiyeweza kuitamani kufanya nayo kazi, lakini tutagusia eneo la ushambuliaji ambalo bado kuna watu wanalitia shaka hususani kutokana na ukame wa mabao licha ya timu kutengeneza nafasi nyingi za wazi. Pamoja na hali hii, safu ya kiungo cha timu imekuwa iki-complement vizuri na pia kasi ya ingizo jipya la washambualiaji Juma Luizio na Pastory Athanas wakisaidiana na wachezaji wasiotabirika kama Laudit Mavugo na Shiza Kichuya kunaweza kuiletea matatizo makubwa safu ya ulinzi ya Yanga ambayo inaonekana kupungua makali hasa kwa performance iliyoonyeshwa ktk mechi ya juzi.

Kikosi cha Simba hakiwezi kukamilika bila kutaja utulivu na kuzoeana kunakoanza kuonekana ndani ya timu na Mwalimu Joseph Omog na Jackson Mayanja wanaonekana kuwa 'chemistry' nzuri baina yao na hata dhidi ya wachezaji.

Hali ni tofauti kwa Yanga ambayo licha ya kuwa na wachezaji wakubwa katika eneo la ulinzi lakini inaonekana kuna tatizo la ukosefu wa utulivu hasa timu inapokabiliana na mashambulizi yenye kasi. Kwa vyovyote iwavyo Yanga inamkosa sana Vincent Bosou ambaye licha ya kuwa kiongozi lakini pia ana kimo na umbo kubwa kukabiliana na mipira ya juu lakini pia akiwa na utulivu wa asili wakati wa ukabaji. Ni upande wa kulia tu aliko Juma Abdul ndiko kuna utulivu wa kutosha na haikuwa ajabu Azam kunufaika na panic na ukosefu wa nidhamu ya ulinzi katika defensi ya Yanga.

Aidha, Yanga ina pancha pia ktk eneo la kiungo kwa kuwa bado Justine Zullu hajawa na maelewano mazuri na wenzake lakini yeye mwenyewe akiwa bado hajaibeba safu hii ya kiungo huku mzee wa kampa kampa tena Thabani Kamsoko akiwa na pressure ya kugombania namba na kinda Said Makapu. Haruna Niyonzima ndio mchezaji aliye katika kiwango cha juu kwa sasa lakini hatarajiwi kuwika dhidi ya 'mande' atakalopigwa na Jonas Mkude, James Kotei na Mzamiru Yassin.

Yanga ni hatari sana katika eneo la ushambuliaji ambako Simon Msuva, Amisi Tambwe na Donald Ngoma katika ubora wao huwa ni ngumu kuzuilika, lakini huku nako kuna tatizo hasa kutokana na majeraha ya Ngoma na Tambwe yanayowafanya kutokuwa fit kama ambavyo ilikuwa ktk mechi dhidi ya Azam. Ikiwa hali itakuwa hivi maana yake mzigo wote wa kutafuta mabao utabakia mabegani mwa Simon Msuva kitu kitakachoirahisishia Simba kumdhibiti hasa anapopambana na mlinzi bora wa kushoto nchini Mohamed Hussein

Bado Juma Mahadhi hajaonesha lolote la maana katika mechi kubwa na ingizo jipya Emmanuel Martin anatarajiwa kujitengenezea jina mbele ya mashabiki wa timu yake hiyo kesho kama atapunguza anao anao. Tatizo la msingi la Yanga ni ufinyu wa kikosi, majeraha ya wachezaji waandamizi kama Tambwe na Ngoma na hata uchovu. Unapoona kocha anatoa mshambuliaji na kumwingiza Oscar Joshua au kutoka beki Haji Mwinyi na kumwingiza Geofrey Mwashiuya, ujue kuwa kuna tatizo kubwa ktk kikosi cha Yanga. Katika michuano hii imedhihirika kuwa baada ya first eleven, Yanga inabakia na wachezaji chini ya 3 wanaoweza kubadilisha mchezo!

Tukija kwenye kipengele cha pili ambacho ni ufundi na mbinu za timu, ni dhahiri Joseph Omog anafaidika zaidi kwa kukaa na timu kwa muda mrefu kiasi ukilinganisha na George Lwandamina. Omog ameanza kazi ya kuisuka Simba tangu wakati wa maandalizi ya msimu, wakati Lwandamina ameipokea timu katikati ya msimu hivyo bado ni ngumu kuona Yanga ikicheza anavyotaka yeye.

Kitakwimu, Simba ni bora zaidi katika mashindano haya kwa kumiliki mpira, kutengeneza nafasi, na hata kwa kuwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa. Pia Simba imeonekana ikibadilisha mifumo kutoka mechi hadi mechi au hata ndani ya mechi moja na yote kuonekana kuwa na manufaa kiasi. Wakati Yanga inatabirika wakati wa kutengeneza mashambulizi ambapo mipira mingi hupitishwa kwa Niyonzima ambaye humpenyezea pasi ndefu Msuva ambaye huwa na maamuzi ya kufunga mwenyewe au kupiga krosi, Simba imeonekana ikitumia mipira ya kupenyeza katikati au hata kukimbia kwa viungo washambuliaji wa pembeni (sio mawinga) na kuingia nayo ndani. Mbinu hii ni hatari sana hasa kutokana na kuwa na wachezaji wenye kasi

Tukimalizia na factor ya tatu, Simba bila shaka inaingia katika mchezo huu ikiwa na morali kubwa hasa baada ya kuibuka vinara wa kundi A, lakini ikiwa ndio timu yenye pointi nyingi kuliko zote na pia ikiwa ni timu ambayo haijapoteza mechi yoyote hadi sasa. Kama ingekuwa ni ligi ya mapinduzi, Simba ingekuwa inaongoza ligi mbili kwa mpigo, kama inavyofanya kwenye VPL. Wakati huohuo, Yanga imefedheheka sana na 'kipigo cha 4G' kutoka Azam hapo juzi na hali hiyo kwa vyovyote imechafua hali ya kambi ambapo tuhuma za hujuma na rushwa zimeanza kusikika. Hali hii itaifanya Yanga kuingia katika mchezo huu wa nusu fainali ikiwa na morali ya chini hasa kama uongozi hautaweza kuituliza kambi. Kama ikitulia Yanga inaweza kunufaika na kujiamini kwa Simba lakini kama kushikana uchawi kutaendelea basi tunaweza kuona kipigo kingine kikali.

Tuhitimishe kwa kusema mchezo wa soka hautabiriki, na mbaya zaidi kila mechi ya baina ya Simba na Yanga hutoa matokeo tofauti na utabiri lakini ni ukweli pia kuwa dalili ya mvua ni mawingu na mwanzo wa ngoma ni lele basi Yanga itakuwa na bahati kubwa kuipandisha boti Simba mapema kurejea jijini Dar es Salaam. Tuombe uzima.
 
Sidhani kama kuna mtu alitegemea Yanga kulambishwa koni na Azam tena bao nne ambazo ni clear kabisa bila kulaumiwa hata referee kwa upendeleo.

Hata hivyo bado naipa nafasi kubwa kwenye huo mtanange sababu Simba ni butu mno kwenye safu ya ushambuliaji ukiilinganisha na Yanga.

Angalia hata aina ya magoli waliyofunga.

I wish Yanga na Azam wakutane Final tuone soka la kukamiana.
 
KIZUR ZAID KULE HAKUNAGA VITI KUNA MATAALUMA YA ZEGE MSHABEBA MATOKEO MIFUKONI MSIPOTOSHWE NA CHANGA LA AZAM
 
Kesho 4G FC watajuta Kuja Zanzibar Manake Miamala Mwisho Dar... Zanzibar Miamala Haifanyi Kazi...
 
Sidhani kama kuna mtu alitegemea Yanga kulambishwa koni na Azam tena bao nne ambazo ni clear kabisa bila kulaumiwa hata referee kwa upendeleo.

Hata hivyo bado naipa nafasi kubwa kwenye huo mtanange sababu Simba ni butu mno kwenye safu ya ushambuliaji ukiilinganisha na Yanga.

Angalia hata aina ya magoli waliyofunga.

I wish Yanga na Azam wakutane Final tuone soka la kukamiana.

Simba na Yanga zote zina goal difference ya 4+, huku Yanga ikiwa imeishinda timu dhaifu zaidi ktk michuano hii kwa mabao 6 na kufungwa mambao 4 baada ya kukutana na timu yenye akili.

Simba inaongoza 'ligi' zote mbili, hii ya VPL na hii ya mapinduzi kwa forward hii hii. Kukataa ubora wa timu hii kwa sasa ni kujitia upofu bila soni mchana kweupe. Takwimu zinaongea zaidi kuliko mwembwe za foward kali kwa timu dhaifu zaidi wakati hakuna chochote cha kuthibitisha wanapokutana na timu kali
 
Tilalila nyiiingi, halafu tena unajistukia! Kwani shida nini hasa!?

Najistukia vipi tena kijana? Huna namna nyingine ya kuelezea frustrations zako kuelekea mechi hii?

Kama una takwimu tofauti weka mezani otherwise kuwa mpole kama wenzio.
 
Simba na Yanga zote zina goal difference ya 4+, huku Yanga ikiwa imeishinda timu dhaifu zaidi ktk michuano hii kwa mabao 6 na kufungwa mambao 4 baada ya kukutana na timu yenye akili.

Simba inaongoza 'ligi' zote mbili, hii ya VPL na hii ya mapinduzi kwa forward hii hii. Kukataa ubora wa timu hii kwa sasa ni kujitia upofu bila soni mchana kweupe. Takwimu zinaongea zaidi kuliko mwembwe za foward kali kwa timu dhaifu zaidi wakati hakuna chochote cha kuthibitisha wanapokutana na timu kali

Tukutane hapa kesho Mkuu.
 
Simba msijidanyanye... Azam wanakamia sana wakicheza na Yanga.. Hatutaki injuries tuna Champions league mwezi ujao... Mnakumbuka faulo aliyofanyiwa Dante na domayo na Yahaya angeweza kuvunjika taya
..anyways kama waandaaji wangeruhusu tungewapeleka under 20...
 
Pamoja na sababu za kujiandaa na club Bingwa! Yanga wakija kwa kukamia leo wanaweza wakapoteana.Mechi hii simba anaweza kushinda kwa kumdhibiti Niyonzima kila apatapo mpira akabwe na watu zaidi ya mmoja.Hapo Martin na Msuva watakwama.Kwa Yanga kushinda wanatakiwa kupiga mipira mirefu ili washambuliaji wachomoke maana Mwanjali hana speed.Kiujumla karata inawabeba zaidi simba japo ushindi utakuwa mdogo sana.
 
Kuelekea 'big match' ya michuano ya kombe la mapinduzi katika hatua ya nusu fainali itakayofanyika kesho Jumanne Januari 10, 2017, uchambuzi huu unaonesha kuwa itakuwa ni ngumu sana Yanga kuepuka kupigo kutoka kwa mtani wake wa jadi Simba.

Hadi majira ya usiku wa saa nne na nusu, kama mambo yatakwenda kama yalivyopangwa, umma wa wapenda michezo ndani na nje ya Tanzania utakuwa umeshajua nani ni nani watakaokutana na mshindi kati ya Azam ya Dar es Salaam na Taifa Jang'ombe ya Unguja.

Mechi hii ya nusu fainali ya watani wa jadi wa soka la Tanzania kati ya Simba ambao ni wababe wa kihistoria wa kombe la mapinduzi na Yanga ambayo imeshawahi kutwaa ubingwa huu mara moja tu, inatarajiwa kuwa kali na yenye ushindani mkubwa katika kila eneo la ndani na nje ya uwanja, hasa kutokana na namna ilivyokuja 'ghafla' ambapo timu zote zina siku moja tu ya kujiandaa.

Katika kukuchambulia mchezo huu, tumezingatia mambo matatu ambayo yanaonekana kuinufaisha Simba na hivyo kutoa uelekeo wa Yanga kulala mapema hiyo kesho. Mambo haya matatu (three factors) ni uimara wa vikosi, ufundi/mbinu na morali ya timu.

Tukianzia na uimara wa vikosi, Simba inaonekana kuwa timu iliyokamilika zaidi katika michuano hii kwa kuwa na kikosi imara, kipana, chenye uwiano mzuri na kilichoanza kuzoeana vizuri. Tutafafanua!

Licha ya kuonekana kufunga magoli machache, Simba imeonekana kuwa imara sana pengine kuliko timu zote katika eneo la kiungo, lakini pia ikiwa na defensi bora na hata safu ya ushambuliaji yenye kasi kubwa. Kuipasua ngome ya Simba chini ya mlinzi shupavu Method Mwanjale, Abdi Banda, Mohamed Hussein 'Tshabalala' na Mkongo Besala Bokungu, na kisha kupita golini kwa Daniel Agyei, ni moja kati ya kazi ngumu mno inayoweza kufanywa na aina ya washambauliaji walionekana katika michuano hii. Hadi sasa Simba imelazimika 'kujifunga' yenyewe ili kuipatia timu pinzani goli.

Katika uchambuzi huu hatuizungumzia safu ya kiungo ya Simba ambayo hakuna kocha yeyote katika ukanda huu asiyeweza kuitamani kufanya nayo kazi, lakini tutagusia eneo la ushambuliaji ambalo bado kuna watu wanalitia shaka hususani kutokana na ukame wa mabao licha ya timu kutengeneza nafasi nyingi za wazi. Pamoja na hali hii, safu ya kiungo cha timu imekuwa iki-complement vizuri na pia kasi ya ingizo jipya la washambualiaji Juma Luizio na Pastory Athanas wakisaidiana na wachezaji wasiotabirika kama Laudit Mavugo na Shiza Kichuya kunaweza kuiletea matatizo makubwa safu ya ulinzi ya Yanga ambayo inaonekana kupungua makali hasa kwa performance iliyoonyeshwa ktk mechi ya juzi.

Kikosi cha Simba hakiwezi kukamilika bila kutaja utulivu na kuzoeana kunakoanza kuonekana ndani ya timu na Mwalimu Joseph Omog na Jackson Mayanja wanaonekana kuwa 'chemistry' nzuri baina yao na hata dhidi ya wachezaji.

Hali ni tofauti kwa Yanga ambayo licha ya kuwa na wachezaji wakubwa katika eneo la ulinzi lakini inaonekana kuna tatizo la ukosefu wa utulivu hasa timu inapokabiliana na mashambulizi yenye kasi. Kwa vyovyote iwavyo Yanga inamkosa sana Vincent Bosou ambaye licha ya kuwa kiongozi lakini pia ana kimo na umbo kubwa kukabiliana na mipira ya juu lakini pia akiwa na utulivu wa asili wakati wa ukabaji. Ni upande wa kulia tu aliko Juma Abdul ndiko kuna utulivu wa kutosha na haikuwa ajabu Azam kunufaika na panic na ukosefu wa nidhamu ya ulinzi katika defensi ya Yanga.

Aidha, Yanga ina pancha pia ktk eneo la kiungo kwa kuwa bado Justine Zullu hajawa na maelewano mazuri na wenzake lakini yeye mwenyewe akiwa bado hajaibeba safu hii ya kiungo huku mzee wa kampa kampa tena Thabani Kamsoko akiwa na pressure ya kugombania namba na kinda Said Makapu. Haruna Niyonzima ndio mchezaji aliye katika kiwango cha juu kwa sasa lakini hatarajiwi kuwika dhidi ya 'mande' atakalopigwa na Jonas Mkude, James Kotei na Mzamiru Yassin.

Yanga ni hatari sana katika eneo la ushambuliaji ambako Simon Msuva, Amisi Tambwe na Donald Ngoma katika ubora wao huwa ni ngumu kuzuilika, lakini huku nako kuna tatizo hasa kutokana na majeraha ya Ngoma na Tambwe yanayowafanya kutokuwa fit kama ambavyo ilikuwa ktk mechi dhidi ya Azam. Ikiwa hali itakuwa hivi maana yake mzigo wote wa kutafuta mabao utabakia mabegani mwa Simon Msuva kitu kitakachoirahisishia Simba kumdhibiti hasa anapopambana na mlinzi bora wa kushoto nchini Mohamed Hussein

Bado Juma Mahadhi hajaonesha lolote la maana katika mechi kubwa na ingizo jipya Emmanuel Martin anatarajiwa kujitengenezea jina mbele ya mashabiki wa timu yake hiyo kesho kama atapunguza anao anao. Tatizo la msingi la Yanga ni ufinyu wa kikosi, majeraha ya wachezaji waandamizi kama Tambwe na Ngoma na hata uchovu. Unapoona kocha anatoa mshambuliaji na kumwingiza Oscar Joshua au kutoka beki Haji Mwinyi na kumwingiza Geofrey Mwashiuya, ujue kuwa kuna tatizo kubwa ktk kikosi cha Yanga. Katika michuano hii imedhihirika kuwa baada ya first eleven, Yanga inabakia na wachezaji chini ya 3 wanaoweza kubadilisha mchezo!

Tukija kwenye kipengele cha pili ambacho ni ufundi na mbinu za timu, ni dhahiri Joseph Omog anafaidika zaidi kwa kukaa na timu kwa muda mrefu kiasi ukilinganisha na George Lwandamina. Omog ameanza kazi ya kuisuka Simba tangu wakati wa maandalizi ya msimu, wakati Lwandamina ameipokea timu katikati ya msimu hivyo bado ni ngumu kuona Yanga ikicheza anavyotaka yeye.

Kitakwimu, Simba ni bora zaidi katika mashindano haya kwa kumiliki mpira, kutengeneza nafasi, na hata kwa kuwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa. Pia Simba imeonekana ikibadilisha mifumo kutoka mechi hadi mechi au hata ndani ya mechi moja na yote kuonekana kuwa na manufaa kiasi. Wakati Yanga inatabirika wakati wa kutengeneza mashambulizi ambapo mipira mingi hupitishwa kwa Niyonzima ambaye humpenyezea pasi ndefu Msuva ambaye huwa na maamuzi ya kufunga mwenyewe au kupiga krosi, Simba imeonekana ikitumia mipira ya kupenyeza katikati au hata kukimbia kwa viungo washambuliaji wa pembeni (sio mawinga) na kuingia nayo ndani. Mbinu hii ni hatari sana hasa kutokana na kuwa na wachezaji wenye kasi

Tukimalizia na factor ya tatu, Simba bila shaka inaingia katika mchezo huu ikiwa na morali kubwa hasa baada ya kuibuka vinara wa kundi A, lakini ikiwa ndio timu yenye pointi nyingi kuliko zote na pia ikiwa ni timu ambayo haijapoteza mechi yoyote hadi sasa. Kama ingekuwa ni ligi ya mapinduzi, Simba ingekuwa inaongoza ligi mbili kwa mpigo, kama inavyofanya kwenye VPL. Wakati huohuo, Yanga imefedheheka sana na 'kipigo cha 4G' kutoka Azam hapo juzi na hali hiyo kwa vyovyote imechafua hali ya kambi ambapo tuhuma za hujuma na rushwa zimeanza kusikika. Hali hii itaifanya Yanga kuingia katika mchezo huu wa nusu fainali ikiwa na morali ya chini hasa kama uongozi hautaweza kuituliza kambi. Kama ikitulia Yanga inaweza kunufaika na kujiamini kwa Simba lakini kama kushikana uchawi kutaendelea basi tunaweza kuona kipigo kingine kikali.

Tuhitimishe kwa kusema mchezo wa soka hautabiriki, na mbaya zaidi kila mechi ya baina ya Simba na Yanga hutoa matokeo tofauti na utabiri lakini ni ukweli pia kuwa dalili ya mvua ni mawingu na mwanzo wa ngoma ni lele basi Yanga itakuwa na bahati kubwa kuipandisha boti Simba mapema kurejea jijini Dar es Salaam. Tuombe uzima.
Ahsante kwa uchambuzi viva Simba
 
Simba msijidanyanye... Azam wanakamia sana wakicheza na Yanga.. Hatutaki injuries tuna Champions league mwezi ujao... Mnakumbuka faulo aliyofanyiwa Dante na domayo na Yahaya angeweza kuvunjika taya
..anyways kama waandaaji wangeruhusu tungewapeleka under 20...

Hiyo Ndiyo Sifa Yenu 4G FC mukishaona Hamuna Muelekeo Na Mnaishia Kupakatwa Kwa Juice Ya Ndimu Basi Munaleta Visingizio Vya Kiajabau ajabu......
 
Back
Top Bottom