Uchambuzi kuhusu Bunge la Tanzania

Suleiman Mfua

Member
Feb 27, 2014
62
64
TUJISAHIHISHE.......!!!

Bunge ni moja ya mihimili mitatu inayounda dola nchini, huku mihimili mingine ikiwa ni serekali kuu kwa maana ya mamlaka ya rais na idara zake pamoja na mahakama.

Pamoja na majukumu kadhaa ambayo bunge lina wajibu wa kuyatekereza lakini pia bunge lina wajibu wa kuisimamia na kuishauli serekali kuhusiana na mambo mbalimbali yanayoendelea ndani ya nchi.

Katika ziku za hivi karibuni kumeibuka tabia ndani ya bunge letu ambayo ni kinyume na utaratibu wa bunge namna ambavyo linapaswa kuendesha shughuli zake.
Tabia hiyo ni pamoja na baadhi ya wabunge kutokua na nidhamu pindi wawapo ndani ya bunge hali inayopelekea baadhi ya wabunge hao kuzomeana na mpaka kufikia hatua ya kutaka kushikana mashati kisa tu kutokubaliana kwa hoja kuhusiana na mijadala inavyoendelea.

Tabia nyingine mbaya na inayonikera ni namna baadhi ya wabunge hao kufanya shughuli za uenezi wa taasisi zao za kisiasa ndani ya ukumbi wa bunge!!
Hili ni jambo ambalo linapaswa kukemewa na wote wenye kujali maslahi mapana ya taifa letu.
Wabunge wote wanapaswa kujua kua katika taasisi zao za kisiasa kuna idara maalum na mahususi zinazoshughulika na uenezi, hivyo tuache idara hizo zitimize jukumu lake kama vile ilivyokusudiwa kwa mujibu wa miongozi mbalimbali ya taasisi husika. Na hata kama itatokea mmoja ya wabunge hao ni muhusika wa moja kwa moja katika idara hizo nae anapaswa kujua kua ukumbi wa bunge si mahala sahihi pa kufanyia uenezi wa taasisi yake ya kisiasa.

Lakini jambo kubwa ambalo limenipelekea kuandika waraka huu mfupi ni namna wabunge wa chama changu (CCM) kuunga mkono kila hoja inayoletwa na serekali tena pasi na kupima uzito wa hoja husika, hilo ni jambo lisilomaana na fedheha kubwa kwa chama chetu na hiyo wakati mwengine hupelekea washindani wetu wa kisiasa kuungwa mkono na makundi kadhaa ya kijamii huku mtaani.

Mimi si wa kwanza wala wa pili kuliona jambo hili na kuna wakati katibu mkuu wa chama chetu Comrade Abdulrahman Kinana aliwahi kulikemea jambo hili linalofanywa na baadhi ya wabunge wetu pindi wawapo kwenye mijadala mbalimbali ndani ya bunge.
Wabunge hao waliopewa dhamana na chama wanapaswa kujua kua hawapo pale kwa ajili ya kuitetea serekali, bali kwa ajili ya kuisimamia pamoja na kuishauli namna bora ya kuendesha mambo yake kwa maslahi ya taifa.

NOTE;
Ni vema sasa wabunge wote bila kujali itikadi za taasisi zao za kisiasa kushindana kwa hoja zenye tija kwa maslahi ya waliowapa ridhaa ya kua wajumbe wa chombo hicho cha maamuzi nchini (wananchi).

Lakini pia niwatake baadhi ya wabunge wetu kupitia chama cha mapinduzi (CCM) kurudi kwenye mstari kwa kuacha kuunga mkono kila hoja inayoletwa na serekali ndani ya bunge,kwa kua wajibu wa kila mbunge ni kuisimamia na kuishauli serekali ili iweze kutimiza wajibu wake kwa wananchi,kitendo cha kuunga mkono kila kinacholetwa na serekali hata kama hakina tija kwa wananchi tafsiri yake hakuna sababu ya wao kuendelea kuwepo ndani ya bunge.

NB; "UTAIFA WETU NI JAMBO LA MUHIMU SANA KULIKO MISIMAMO YA TAASISI ZETU ZA KISIASA"

Mfua suleiman
+255 713 660 746
sullemfua@gmail.com
 
Back
Top Bottom