UCHAMBUZI: Kodi mpya ya VAT Yavuruga sekta ya Utalii

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Utalii ni sekta ambayo inaongoza kwa kuingiza fedha nyingi za kigeni hapa nchini.

Sekta hii mchango wake katika pato la taifa ni zaidi ya asilimia 17 na hadi sasa imetoa ajira za aina mbalimbali kwa zaidi ya watu 800,000 .

Ili kuongeza mapato, Serikali imeanzisha kodi mpya ya ongezeko la thamani(VAT) katika huduma za utalii.

Kodi hiyo mpya, imeibua mijadala katika sekta ya utalii, hasa kutokana wadau wa sekta hiyo, kuipinga kodi hiyo.

Wenye makampuni ya utalii wamekuwa wakieleza kuwa kodi hiyo, itawaathiri wao kwa kuwa tayari watalii ambao wanakuja nchini kuanzia mwezi huu wamekwishalipia safari zao.

Katika taarifa yao, kupitia chama cha watoa huduma za Utalii(Tato), watoa huduma hawa walieleza kuwa hawapingani na serikali lakini wanachopinga ni muda mfupi uliotolewa kuanza kodi hii.

Kwa ambao wanafuatilia sekta hii wanajua kuwa, makampuni mengi ya utalii nchini yanashirikiana na makampuni makubwa ya uwakala wa utalii yaliyopo nje ya nchi.

Mawakala hawa wa nje ndio ambao hufanya makubaliano na watalii na kulipwa na baadaye hutuma fedha za watalii wanaokuja nchini kwa makampuni ya ndani. Hili hufanyika kati ya mwaka mmoja hadi miezi miwili kabla ya mtalii hajaanza safari ya kuja nchini.

Kwa wale ambao hutembelea hifadhi watakubaliana nami kuwa katika msimu wa utalii ni vigumu sana kupata hoteli katika maeneo ya hifadhi kama Serengeti, Tarangire, Manyara na Ngorongoro.

Hivyo hoja ya Tato kutaka muda uongezwe wa kuanza kwa kodi hii ilikuwa na uzito kwa kuwa itavuruga sekta ya utalii.

Hoja hii ilikuwa na nguvu kwani kwa mfumo wa biashara ya utalii, ambao unafanyika kwa muda maalumu haiwezekani ndani ya muda mfupi kubadilisha gharama za utalii.

Kama nilivyosema awali wenye makampuni walikwisha pokea fedha na baadhi tayari walikuwa wamelipia huduma za watalii ambao watakuja nchini.

Hivyo katika mazingira ya sasa wenye makampuni wanalazimika kupunguza wageni ili kuwa na uwezo wa kutoa fedha zao kulipa asilimia 18 ya VAT.

Tukio hili lina sura tatu, kwanza huenda waliotoa mapendekezo ya kodi hii hawajui sekta ya utalii, ama wanataka kujionesha wanakusanya fedha nyingi ama wameshauriwa vibaya.

Lakini pia kukataliwa kwa maoni ya wadau kunajenga taswira mbaya kwani kimsingi wadau hawapingi kodi hii bali wanalalamikia muda mfupi uliotangazwa kuanza kulipwa.

Sakata hili linafanana na kodi mpya kwenye miamala ya fedha, sasa kuna utata nani anapaswa kulipa kati ya benki au mteja.

Wakati Mamlaka ya Kodi ya Mapato (TRA) ikitaka mabenki kulipa kodi hiyo,lakini mabenki yameweka wazi kodi hii ni ya mteja. Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndullu ameungana na mabenki kuwa kodi hiyo haiwezi kulipwa benki.

Utata huu unathibitisha kuwa, Watanzania walio wengi wanapenda kulipa kodi, lakini tunakosa mazingira bora ya kuwashawishi kulipa kodi. Maridhiano haya ndio ambayo yatawezesha wananchi na makampuni kulipa kodi bila ya malalamiko .

Hivyo itoshe kutoa wito, kwa serikali na kukaa na wadau kumaliza migogoro hii ya kodi kwani Tanzania ni ya watanzania wote si ya wachache.

Kupungua kwa watalii ambao mapato yao ndio yanaongoza kuingizia taifa fedha nyingi za kigeni kutaliathiri taifa hivyo ni busara kutazama upya kodi hii mpya isivuruge utalii wetu.
 
Propaganda za Mafisadi at work, Magufuli usirudi nyuma.

Hata aje mtalii mmoja kwa mwaka lazima alipe kodi
 
post: 16775477 said:
Propaganda za Mafisadi at work, Magufuli usirudi nyuma.

Hata aje mtalii mmoja kwa mwaka lazima alipe kodi
Aje huyo huyo mmoja, cha msingi alipe kodi
 
Back
Top Bottom