Uchakachuaji wa maziwa fresh

JimCarrey

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
214
124
Jamani wapendwa mimi mkewangu ni mjamzito hivyo nimeamua kumuekea bili ya maziwa flesh.Lakini kila wakileta hayo maziwa siyaelewi.

Siku nyingine yanakua na harufu mbaya yaani yakichemshwa tu jikoni ukikaa sebuleni unasikia harufu yake sikuingine maziwa yanakua kama yameungwa chumvi na juu kuna mafuta meengi ya njano ambayo yametengana kabisa na maziwa.

Hata ukiyanywa hakuna radha halisi ya maziwa kabisa.Naogopa yanaweza yakawa kwa madhara kwa mtoto ambaye bado hajazaliwa.

Naombeni msaada nijue nini kinawekwa kabla hatujachukua maamuzi ya kununua maziwa ya box
 
Jamani wapendwa mim mkewangu ni mjamzito hivyo nmeamua kumuekea bili ya maziwa flesh... Lakini kila wakileta hayo maziwa siyaelewi,Siku nyingine yanakua na harufu mbaya yaani yakichemshwa tu jikoni ukikaa sebuleni unasikia harufu yake sikuingine maziwa yanakua kama yameungwa chumvi na juu kuna mafuta meengi ya njano ambayo yametengana kabisa na maziwa... Hata ukiyanywa hakuna radha halisi ya maziwa kabisa.. Naogopa yanaweza yakawa kwa madhara kwa mtoto ambaye bado hajazaliwa... Naombeni msaada nijue nini kinawekwa kabla hatujachukua maamuzi ya kununua maziwa ya box
Jaribu kupata maziwa fresh, hayo mengine siyajuwi kabisa!
Kwanza mi mwenyewe mgeni hapa!
 
Jamani wapendwa mim mkewangu ni mjamzito hivyo nmeamua kumuekea bili ya maziwa flesh... Lakini kila wakileta hayo maziwa siyaelewi,Siku nyingine yanakua na harufu mbaya yaani yakichemshwa tu jikoni ukikaa sebuleni unasikia harufu yake sikuingine maziwa yanakua kama yameungwa chumvi na juu kuna mafuta meengi ya njano ambayo yametengana kabisa na maziwa... Hata ukiyanywa hakuna radha halisi ya maziwa kabisa.. Naogopa yanaweza yakawa kwa madhara kwa mtoto ambaye bado hajazaliwa... Naombeni msaada nijue nini kinawekwa kabla hatujachukua maamuzi ya kununua maziwa ya box

Mkuu uko wapi? Kama ni Dar Es Salaam basi kupata
maziwa halisi ya ng'ombe ni changamoto kubwa kama kwenda sayari ya Mars! Unatakiwa umjue mtu anayefuga na anayeaminika ufanye nae dili la bili. Au tafuta rafiki yako anayeaminika mwenye rafiki anayeaminika anayefuga ng'ombe ufanye dili la bili.
 
Bora wewe umejibu vizuri.

Kwa jiji la Dar maziwa kwa mfumo wa Order ni janga.
Unaweza kukuta mwanzo mnaenda vizuri,ila baada yamuda ndio anaanza kuyazimua.Na pia anaangalia ni mtu wa mkoa gani na umekulia wapi.
Mie ambae niliwahi Kuishi Magu na kusomea pale Shule ya Itumbili,mliopo Magu mtakumbuka shule hii ipo njiani kabisaa.Na mzee wangu alikuwa anafanya kazi Bima,karibia na CCM na nyumba kama ya nne ndio nilikuwa nakaa mie.
Sasa nilijifunza mengi sana kwa Ndugu zangu wakarim wasukuma,maana msukuma ujuzi hakunyimi.Yaani maziwa feki huhitaji hata kuonja,yaani kuna watu vichwa kweli,akiyatizama tu anakuambia hapa hamna kitu,na wengine akiyatizama tu,anakuambia kwamba mwenye ng`ombe hamlishi vizuri ila maziwa ni halisi,au mwenye ng`ombe amempa chakula chenye mchanganyo mbaya,na mambo mengine teleee.

Kubadilika ladha ya maziwa kuna factors nyingi sana,ng`ombe mmoja anaweza kutoa maziwa yenye ladha tofauti zaidi ya tano,kutegemea na umri wa ng`ombe,malisho,magonjwa, na mazingira kwa ujumla.

Ila kwa jiji la Dar wao wanapiga dili kwa kuchakachua.We ukitaka kujua hilo,huyo anaekuuzia tafuta anapokaa,kisha nenda mtume mtu akanunue maziwa kwake,hapo ndio utajua kwamba yote ni sawa au anakupiga.Watu wa order wengi huwa wanaumizwa sana kwa kuchakachukuliwa maziwa,ila wale wa vuu vaa huwa wanauziwa maziwa mazuri ili kesho waje,maana sio wateja permanent.

Kuna mama mmoja Kisukulu ana ng`ombe wake pale kwake,nahisi kama wanne hivi,aisee anapiga hela mbaya.Maziwa yake ni mazuri ile mbaya ahhh nimesahau maziwa yake ni mazuri ile nzuri.

Na jinsi jiji la Dar linavyoelekea ni kwamba wale wanofuga ng`ombe mitaani yaa kwenye nyumba za mitaani ndio wenye kupata hela nzuri na wateja wengi sana,maana huyu mama kuna watu waacha chupa usiku na kuchukua kesho yake kwa jinsi wateja walivyo wengi.Hii pia ni fursa kwa vijana na ndio mtajifunza kununua pia viwanja vyenye sehem kubwa ya kutosha.

Ushauri,usimpe maziwa ya Kopo.Ungekuwa na eneo kama la chumba kimoja hivi ungenunua mbuzi wa maziwa,maana ni rahisi kuwahudumia,nunua kama wawili tu watakutosha na familia yako vizuri sana tu
 
Mara nyingi Maziwa ya namna hiyo utakuta Mwenye Ng'ombe alitibu Ng'ombe wake na kuendelea kuuza maziwa hayo,kwa mfano Ng'ombe akiwa na Mastitis ugonjwa wa kiwele maziwa yake hayataikiwi kwa matumizi ya binadamu,akichomwa sindano ya Antibiotic maziwa yanatakiwa yasitumike kwa muda wa siku 7 mpaka 14 sasa wafugaji wengi haswa wadogo wadogo huwa wana yauza bila kujali afya ya mtumiaji.
Wataalaam wanashauri kutumia maziwa yaliyosindikwa na kufuata kanuni zote za afya.
 
Pamoja na sababu walizochangia wadau hapo juu kuwa ni za kweli na za msingi,ninakubaliana nazo kabisa kwa asilimia zote mimi hii ndo shughuli kubwa kwa nyumbani kwetu tukiwa na experience ya ufugaji wa ng'ombe wa maziwa kwa takribani miaka 13 sasa. shida kubwa ya wafugaji wengi ni usafi yani hapo tatizo kubwa ni usafi wa hao wanaokupatia hiyo huduma. Ng'ombe kama walivyo wanyama wengine na binadamu wanahitaji matunzo mazuri ili waweze kukupatia matokeo bora kwa maana ya Maziwa,Nyama,Ngozi na Mbolea pia, mambo ambayo huwa yanahusisha gharama kiasi ambacho wafugaji wengi huwa hawataki kuziingia kabisa. mabanda yao yanatakiwa yasafishwe kila siku asubuhi na jioni kwa kupigwa na deki kabisa kwa sehemu zisizo na maji basi walau mara 3 au 4 kwa wiki asubuhi na jioni hapo utasaidia ng'ombe watakuwa hawachafuki na hawatakuwa na hatari ya kuvamiwa na magonjwa sasa unakuta ng'ombe wanalala pachafu, Ngozi yote ina kinyesi chake, kiwele cha maziwa ndo usiseme, Ng'ombe kama binadamu wanapaswa kuoga kwa kila wiki mara 1 angalau, na wapuliziwe dawa kabisa haya mambo ni wafugaji wachache wa mjini huzingatia lakini ni mambo muhimu sana ili ulinde mfugo na pia upate bidhaa bora kutoka kwa mifugo, chakula pia huchangia japo hakina athari kubwa katika harufu, chakula chenye kina mantiki kwa maana ya ujazo wa maziwa kuna vyakula vinamfanya ng'ombe atoe maziwa mengi sana na vingine madogo alikadharika kuna vyakula vinamfanya atoe maziwa mazito na vingine maziwa mepesi.

Sasa inawezekana kabisa huko unakochukuwa maziwa hawazingatii usafi haswa kipindi cha kukamua kwa sababu pindi unapotaka kukamua wataalamu hushauri kutumia maji ya moto kiasi katika kusafisha kiwele ili kukipa joto litakalomfanya ng'ombe awe relaxed kutoa maziwa, hili nina uhakika ni wafugaji wachache wanajali hili hasa ukitegemea linahusisha gharama za chanzo cha nishati iwe mkaa,umeme,au gesi kwa kuchemshia hayo maji sisi kwa bahati tunatumia biogas ya kinyesi cha hawa hawa ng'ombe tunao wafuga nyumbani.
unapo safisha kiwele inatakiwa yale maji yanayobaki kwenye ngozi uyakaushe na kitambaa kikavu kama tunavyojifuta maji ya mwilini na matauro baada ya kuoga. baada ya hapo kuna mafuta huwa yanatumika kurainisha chuchu hapo pia kunaweza kuwa na sababu ya hiyo harufu sababu yale mafuta yasipopakwa kwa umakini yakachanganyika na maziwa huwa yana ki harufu sio kizuri sana, hapa si huwa tunatumia yakawaida tu ya kupikia, Ndoo ambayo inapokea maziwa huwa inatakiwa iwe safi na kavu kabisa shughuli ya uzalishaji na uuzaji wa maziwa inapaswa kuwa na usafi wa hali ya juu sana kutokana na nature ya bidhaa yenyewe kuwa so perishable maziwa yakiwa exposed tu na tone hata la limao au kambegu kake yanachukuwa muda mfupi sana kuganda na kuharibika na yakiwa katika hali isiyo ya usafi basi hapo tegemea harufu maradufu.

Wateja pia ni kikwazo, hasa mnapo waachia wadada wa kazi wapo ambao hawajali kabisa usafi wa vyombo wanavyochukulia maziwa, huku ninapoishi wengi wamezea kuja na madumu ya maji haya sasa unakuta ukimuhudumia leo kesho analeta dumu ambalo lilizuuzwa tu na maji afu likatunzwa kopo linakuja lina mabaki ya maziwa na linanuka kabisa mtu amekuja nalo anataka umuwekee ukiweka yakaganda anakuja kukulaumu wakati yeye hakusafisha dumu lake kuondoa marumbano nakurinda biashara yako sometimes mtu akija na dumu chafu unalazimika kuliosha kwanza kwa maji na sabuni kabisa ndo unaweka maziwa likiwa chafu zaidi unatumia hata maji ya moto. Ni muhimu sana mnapo waachia ma dada wa kazi muwafundishe haya mambo wapo ambao hufanya kwa kutoelewa ukiwafundisha mnafanya kazi vizuri sana na vilaza pia wapo inabidi ujitolee tu ili maisha yaende. all in all shughuli yeyote inayohusu bidhaa za maziwa inahitaji usafi wa hali ya juu sana kwa mzalishaji{mfugaji/viwandani} na kwa Mlaji{wateja}
samahni kwa kuwachosha na maelezo marefu
 
Wahuni wanaongeza maji wakati maziwa yameshaganda, kwa macho yanakuwa mazuri mdomoni hayana ladha kabisa.

Wengine wanagandisha maziwa kutumia limau, ladha haifurahishi
 
Kuna kifaa kinachotumika kupima uhalisia wa maziwa fresh kinaitwa lactometer (au galactometer). Kifaa hiki kinauzwa kwa bei ya kawaida tu kwenye maduka hasa maduka ya vifaa vya hospitali. Pengine unaweza kujinunulia kifaa hicho ili kuepuka kununua maziwa yaliyochakachuliwa.
 
Jamani wapendwa mimi mkewangu ni mjamzito hivyo nimeamua kumuekea bili ya maziwa flesh.Lakini kila wakileta hayo maziwa siyaelewi.

Siku nyingine yanakua na harufu mbaya yaani yakichemshwa tu jikoni ukikaa sebuleni unasikia harufu yake sikuingine maziwa yanakua kama yameungwa chumvi na juu kuna mafuta meengi ya njano ambayo yametengana kabisa na maziwa.

Hata ukiyanywa hakuna radha halisi ya maziwa kabisa.Naogopa yanaweza yakawa kwa madhara kwa mtoto ambaye bado hajazaliwa.

Naombeni msaada nijue nini kinawekwa kabla hatujachukua maamuzi ya kununua maziwa ya box

Mkuu nakushauri kama unaishi Dar Es Salaam na ni maeneo ya mjini basi nunua maziwa ya Kampuni ya Tanga fresh mazuri sana wanajitahidi kwa kweli. Lakini kupata maziwa fresh unayotaka kwa mji huu ni vigumu sana. Labda ungekuwa unaenda kule Kigamboni, Dar Es Salaam Zoo maziwa yanakamuliwa unayaona na unaondoka nayo. Sasa utaweza kwenda mara kwa mara?
 
Dah uko pouwa. Ila cc miafrika tunalaana kill ki2 kuchakachua hata ki2 simple kama maziwa inaonekana ni kinywaji change anasa
 
Kama unaishi Dar, Maeneo ya karibu na Tegeta IPTL, naweza nikakuelekeza sehemu ambayo utapata maziwa mazuri sana ya ng'ombe
 
Kuna kifaa kinachotumika kupima uhalisia wa maziwa fresh kinaitwa lactometer (au galactometer). Kifaa hiki kinauzwa kwa bei ya kawaida tu kwenye maduka hasa maduka ya vifaa vya hospitali. Pengine unaweza kujinunulia kifaa hicho ili kuepuka kununua maziwa yaliyochakachuliwa.

Mkuu hiki kifaa kwa maziwa ya Bongo kila siku kitakupa jibu silo.
Na ukienda kupima kwa mtu siku ya kwanza atakupotezea ila siku ya pili atakulamba kisu.
 
ALL SAID, WELL AND FINE THE BOTTOMLINE NI KUWA BEI YA MAZIWA NI NDOGO WAKATI PRODUCTION COSTS NI KUBWA. MFANO A SINGLE DOSE OF PAVEXON IS 50,000 tSH..... A SINGLE INJECTION! WHAT DO YOU DO TO BALANCE THE PRODUCTION COSTS/EXPENDITURE AND INCOME.... WEKA MAJI...
 
Back
Top Bottom