Mkuu uko wapi? Kama ni Dar Es Salaam basi kupata
maziwa halisi ya ng'ombe ni changamoto kubwa kama kwenda sayari ya Mars! Unatakiwa umjue mtu anayefuga na anayeaminika ufanye nae dili la bili. Au tafuta rafiki yako anayeaminika mwenye rafiki anayeaminika anayefuga ng'ombe ufanye dili la bili.
Bora wewe umejibu vizuri.
Kwa jiji la Dar maziwa kwa mfumo wa Order ni janga.
Unaweza kukuta mwanzo mnaenda vizuri,ila baada yamuda ndio anaanza kuyazimua.Na pia anaangalia ni mtu wa mkoa gani na umekulia wapi.
Mie ambae niliwahi Kuishi Magu na kusomea pale Shule ya Itumbili,mliopo Magu mtakumbuka shule hii ipo njiani kabisaa.Na mzee wangu alikuwa anafanya kazi Bima,karibia na CCM na nyumba kama ya nne ndio nilikuwa nakaa mie.
Sasa nilijifunza mengi sana kwa Ndugu zangu wakarim wasukuma,maana msukuma ujuzi hakunyimi.Yaani maziwa feki huhitaji hata kuonja,yaani kuna watu vichwa kweli,akiyatizama tu anakuambia hapa hamna kitu,na wengine akiyatizama tu,anakuambia kwamba mwenye ng`ombe hamlishi vizuri ila maziwa ni halisi,au mwenye ng`ombe amempa chakula chenye mchanganyo mbaya,na mambo mengine teleee.
Kubadilika ladha ya maziwa kuna factors nyingi sana,ng`ombe mmoja anaweza kutoa maziwa yenye ladha tofauti zaidi ya tano,kutegemea na umri wa ng`ombe,malisho,magonjwa, na mazingira kwa ujumla.
Ila kwa jiji la Dar wao wanapiga dili kwa kuchakachua.We ukitaka kujua hilo,huyo anaekuuzia tafuta anapokaa,kisha nenda mtume mtu akanunue maziwa kwake,hapo ndio utajua kwamba yote ni sawa au anakupiga.Watu wa order wengi huwa wanaumizwa sana kwa kuchakachukuliwa maziwa,ila wale wa vuu vaa huwa wanauziwa maziwa mazuri ili kesho waje,maana sio wateja permanent.
Kuna mama mmoja Kisukulu ana ng`ombe wake pale kwake,nahisi kama wanne hivi,aisee anapiga hela mbaya.Maziwa yake ni mazuri ile mbaya ahhh nimesahau maziwa yake ni mazuri ile nzuri.
Na jinsi jiji la Dar linavyoelekea ni kwamba wale wanofuga ng`ombe mitaani yaa kwenye nyumba za mitaani ndio wenye kupata hela nzuri na wateja wengi sana,maana huyu mama kuna watu waacha chupa usiku na kuchukua kesho yake kwa jinsi wateja walivyo wengi.Hii pia ni fursa kwa vijana na ndio mtajifunza kununua pia viwanja vyenye sehem kubwa ya kutosha.
Ushauri,usimpe maziwa ya Kopo.Ungekuwa na eneo kama la chumba kimoja hivi ungenunua mbuzi wa maziwa,maana ni rahisi kuwahudumia,nunua kama wawili tu watakutosha na familia yako vizuri sana tu