mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,227
- 6,666
"LIPUMBA: Ni Shein pekee anayeweza kumaliza utata wa uchaguzi Z'Bar" limeripoti gazeti la MWANANCHI, Alhamisi, Desemba 31, 2015. Gazeti hilo limeongeza likimnukuu Lipumba kwamba "... Dk Shein ndiye anayeweza kuifanya Zanzibar iwe na amani au vurugu, ninashauri arihusu kutangazwa kwa matokeo."
Pamoja na kuamini kwamba Prof Lipumba ana nia nzuri na ushauri wake una uzito kiasi fulani, ni vyema kuzingatia yafuatayo:
1) Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha, alitoa kasoro kadhaa zilizobainishwa wakati wa kupiga kura, zilizomfanya atumie madaraka yake kisheria kufuta huo uchaguzi. Kasoro hizo zirejewe, moja baada ya moja, kukamilisha uhakika wake na kutafuta suluhisho la kudumu.
2) Kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi uliopita, ni budi kila kura za kituo cha uchaguzi zihesabiwe upya na kuhakikiwa kwa kutumia kitabu cha wapiga kura. Hili litabainisha kura halali zitazowekwa kwenye hesabu.
3) Zoezi la kurejea uhesabuji wa kura hizo, liundiwe tume huru.
4) Vyama vyote vikubaliane na matokeo hayo.
TAFAKARI CHUKUA HATUA