Uchaguzi Zanzibar wajadiliwa Bunge la Uingereza

Uchaguzi Zanzibar wajadiliwa Bunge la Uingereza

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,728
Reaction score
62,871
HALI ya kisiasa na kufutwa kwa uchaguzi wa urais pamoja na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar hatimaye imetua na kujadiliwa katika Bunge la mabwanyenye la nchini Uingereza.

Uamuzi huo umekuja siku moja baada ya wapinzani wawili wa kisiasa visiwani humo, Rais Dk. Ali Mohamed Shein na Makamu wake wa Kwanza ambaye pia alikuwa mgombea wa urais kupitia CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kuendelea na vikao vya siri vinavyoshirikisha marais wastaafu wa Zanzibar.

Sakata hilo liliibuka jana nchini Uingereza katika kikao cha Bunge ambapo mbunge Lord Steel wa Aikwood kutoka Chama cha Liberal Democrat, alitaka kujua tathmini ya Serikali ya Uingereza kuhusu uchaguzi nchini Tanzania, hasa ule wa Zanzibar na kilichoelezwa kwa Serikali ya Tanzania au Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola kuhusu uchaguzi huo.

Kutokana na swali hilo, Waziri wa Nchi, Baroness Anelay wa St. Johns, alisema kuwa pamoja na kuwapo matatizo kadhaa, uchaguzi wa Tanzania ulifanyika kwa amani na uliendeshwa vyema.

Alisema kutokana na hali hiyo, Serikali ya Uingereza ilitoa pongezi kwa Rais Dk. John Magufuli kutokana na ushindi wake alioupata katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Tulitoa pongezi zetu kwa Rais Magufuli kufuatia ushindi wake. Hata hivyo, tulisikitishwa na uamuzi wa kufuta uchaguzi wa urais na uwakilishi Zanzibar.

Kwa nyakati tofauti tulieleza masikitiko yetu kwa Serikali ya Tanzania kuhusu hilo, ikiwamo katika ngazi za juu na hivi karibuni kabisa ilikuwa wiki iliyopita wakati wa mkutano baina ya Balozi wa Tanzania mjini London na Waziri Mdogo wa Nchi kwa Masuala ya Kigeni na Jumuiya ya Madola, Mheshimiwa Mbunge wa Rochford na Southend East, James Duddridge,? alisema Anelay.

Mgogoro wa kisiasa Zanzibar umekuwa ukichukua sura tofauti, ambapo wiki iliyopita Wazanzibari wanaoishi nchini Uingereza walifanya maandamano na kuitaka nchi hiyo iingilie kati na kutoa shinikizo kwa Serikali ya Tanzania ili kuhakikisha mshindi wa uchaguzi wa rais wa Zanzibar anatangazwa na kuapishwa.

Wazanzibari hao walifikia uamuzi huo kutokana na hatua ya Mwenyekiti wa ZEC, Jecha, kutangaza kufuta matokeo ya uchaguzi, huku akitoa sababu tisa ikiwamo uchaguzi huo kutokuwa huru na haki.

Maandamano hayo yaliishia katika Mtaa wa Downing zilipo ofisi za Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron na kukabidhi barua yao.

Mbali na Uingereza, Wazanzibari wanaoishi nchini Marekani nao pia waliandamana hadi Ikulu ya nchi hiyo, ikiwa ni juhudi za kutafuta uingiliaji kati wa kimataifa ili kuupatia suluhisho mzozo huo.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi mbele ya Ikulu hiyo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazanzibari Waishio Marekani (ZADIA) iliyoandaa maandamano hayo, Omar Haji Ali, alisema uamuzi wao huo ni katika juhudi za kutafuta uingiliaji kati wa kimataifa katika kuukwamua mgando wa kisiasa visiwani Zanzibar.

Chanzo: Gazeti Mtanzania
 
Safi sana watoe maagizo ya haraka kwa utekelezaji tuu, Mwalimu alishasema "hata bei ya korosho wakiamua wanaweza kutupangia"

Waznz wameweza na waendelee zaidi kwa kila jambo na baadae waandamane hukohuko kudai kile kiti cha umoja wa Mataifa cha Zanzibar.
 
Hao waingereza Zanzibar inawahusu nini?

Hata mimi hushangaa nchi za Ulaya zinawahusu nini Nchi zetu za Kiafrika kuwa wao wachangie bajeti zetu, hata uchaguzi tunazofanya wao wanchangia asilimia kubwa ya Pesa.
Nafikiri hili suala ukilijibu , utapata jawabu ya suala lako
 
Wazanzibar wamefanikiwa kuzuia goli la mkono,watahangaika sana magamba mwaka huu.
 
Sioni Mwingereza kufanya lolote hapo. Tanzania ni nchi moja ambayo hawawezi kuiingilia mambo yake ya ndani. Wanaweza kujaribu lakini hapo wamegonga mwamba na wanalifahamu hilo.

Kukosana na Tanzania ni kukosana na SADC ambako Tanzania ina ushawishi mkubwa. Mwingereza mwenyewe ana matatizo sugu ya Scotland na Wales atayaweza ya Zanzibar.

Halafu huyo Came ron yuko weak sana. Uchaguzi utafanyika na Seif haambulii kitu. Nafahamu JPM akimaliza kuunda timu yake na kuanza kulishughulikia swala la Zanzibar wengi mtashangaa.
 
Sioni Mwingereza kufanya lolote hapo. Tanzania ni nchi moja ambayo hawawezi kuiingilia mambo yake ya ndani. Wanaweza kujaribu lakini hapo wamegonga mwamba na wanalifahamu hilo.

Kukosana na Tanzania ni kukosana na SADC ambako Tanzania ina ushawishi mkubwa. Mwingereza mwenyewe ana matatizo sugu ya Scotland na Wales atayaweza ya Zanzibar.

Halafu huyo Cameron yuko weak sana. Uchaguzi utafanyika na Seif haambulii kitu. Nafahamu JPM akimaliza kuunda timu yake na kuanza kulishughulikia swala la Zanzibar wengi mtashangaa.

Kuna kitu muingereza atataka Tanzania kisikubaliwe? Je una habari hata private Jet ya Rais wako pesa kapewa na Muingereza!?
Watagonga Mwamba!

Muingereza akiitaka Tz kesho anaichukua kwa bei buree. Kaa mkao wa kula uone nini kitafanyika. Mabeberu wameshasema Sheni Mwizi. kuku mtaumia bure vichwa, shughuli bado pevu hii.
 
Umekurupuka tu wewe hufahamu lolote sina muda wa kupoteza.
 
Umekurupuka tu wewe hufahamu lolote sina muda wa kupoteza.

Teh teh teh.
Huna muda wa kupoteza mbona umejibu?
Kichwa kikijaa kamasi ni shida tu.

Muingereza akitaka wewe ulale nje kesho huna ujanja. Saana itabidi ukatafute mwamvuli tu.

Unalitambua deni Tz inayodaiwa na Uingereza? Au unabwabwaja tu.
Wakoloni wanakupatia choo mpk leo halafu unaleta jeuri!
Ovyooo.
 
Kuna kitu muingereza atataka Tanzania kisikubaliwe? Je una habari hata private Jet ya Rais wako pesa kapewa na Muingereza!?
Watagonga Mwamba!

Muingereza akiitaka Tz kesho anaichukua kwa bei buree. Kaa mkao wa kula uone nini kitafanyika. Mabeberu wameshasema Sheni Mwizi. kuku mtaumia bure vichwa, shughuli bado pevu hii.

Labda huyo muingereza akuchukue ww akakuoe huko ata hiyo kesho ila sio kuimlisha serikali ya Tanzania
 
Labda huyo muingereza akuchukue ww akakuoe huko ata hiyo kesho ila sio kuimlisha serikali ya Tanzania

Kuimlisha ndio kukufanyaje shangazi?
Au umeshanyweshwa kimpumu na mzee makolo?
Teh teh teh teh
 
Kwa taarifa km uingereza ni sebule basi tz choo potelea mbali vyote ni muhimu kwa binadamu.
 
Hata mimi hushangaa nchi za Ulaya zinawahusu nini Nchi zetu za Kiafrika kuwa wao wachangie bajeti zetu, hata uchaguzi tunazofanya wao wanchangia asilimia kubwa ya Pesa.
Nafikiri hili suala ukilijibu , utapata jawabu ya suala lako

Muulize JK aliyekuwa anashinda huko kuwaombeeni hela za kununulia vyandarua.

Mwl.Nyerere alikuwa anawaita hao wakubwa. Hata bei ya korosho za mzaramo wanapanga bei wao.

Unauliza wao wanahusika vipi na Zanzibar? Kaulize zanj. fedha zao za kigeni zinatoka wapi? Watalii wa ulaya ndio wanaozipeleka zzanj..
 
Hatimaye bao la mkono limedunda, hongereni wazanzibar, endeleeni kudai haki yenu.
 
Pol pot ndio zile shule za chini ya mti hizo, mpaka umri huo hujui nguvu na ushawishi wa waingeleza hapa tanzania na duniani, pole sana na elimu yako ya kujibia mitihani sio kufahamu.
 
Back
Top Bottom