Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,789
Tumemaliza uchaguzi kwa salama kwa amani na Rais mteule ametangazwa. Hongera Dr Shein.
Lakini kama ningepata nafasi ya kudadisi siri ya ushindi wa kushindo umetokana na nini nisingelichelea kuhususha nguvu za kiza za maruhani au masubiani.
Kwa nini nasema hivyo kuwa haiwezekani kwa nguvu za kawaida zabinaadamu kuongeza idadi ya wapiga kura kwa speed ya shuttle halafu iendane na ile kuhesabu kura.
Sote tumeshudia vituo tokea asubuhi hadi kufungwa kwake alasiri vikikosa wapiga kura wengi hadi kufikia baadhi ya mafisa wa ZEC kuchapa usingizi. Sote pia tunajua mkoa wa mjini na mgharibi ndio unao asilimia kubwa ya wapiga kura Zanzibar na hali ya wapiga kura waliojitokeza tuliiona.
Kuambiwa kuwa kulikuwa na wapiga kura ( binadamu) waliofikia 320,000 inatia mashaka kuamini, kama inavyotia mashaka kuamini kauli za Jecha.
CUF waliwahi kutumia mfumo wa maruhani ( kuharibu kura ) kutumia wapiga kura kwa vile wagombea wao waliwekewa pingamizi kule Pemba, katika jitihada ya kukisambaratisha chama cha CUF katika moja ya chaguzi tata. CCM inaonekana imekuja na mfumo jibu wa maruhani, nao ni wa SUBIANI ( Kura 10 mtu mmoja)Matokeo yake ni ushindi wa kishindo!