Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,265
- 21,443
Uchaguzi wa marudio Zanzibar umekwisha, na Shein ametangazwa mshindi. Kila mtu anajua huu umekuwa ni uchaguzi wa kulazimisha ili kuhalalisha matokeo. Ikiwa leo hii Watanzania kwa ujumla, sio Wazanzibari peke yao, tukidhani kwamba kitakachofuata Zanzibar ni hali ya amani na utulivu basi sisi ni watu wa kuhurumiwa sana.
Haingii akilini kwamba watu na busara zao wameshindwa kuona kwamba kulazimisha uchaguzi wa marudio kulikofanyika Zanzibar ni kutengeneza tatizo ambalo litakuwa gumu kutatua kuliko kufikia muafaka katika mazungumzo yaliyokuwa yakifanyika kati ya CUF na CCM. Kwa nini viongozi wetu wanakuwa na shingo ngumu kiasi hiki?Hivi kweli haya yote yamefanyika kwa faida ya wananchi kweli?
Haya, sisi yetu macho. Mmeyavulia nguo maji na sasa iliyobaki muyaoge. CCM kazi kwenu. Dunia nzima inawaangalia. Wapo watakaowaambia tuliwaambia sisi hamkutaka kutusikia.