Jacobus
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 4,703
- 1,724
Jamal Malinzi, rais wa shirikisho la soka nchini, sasa inafaa ajipime. Tokea aingie madarakani kafanya mambo mengi ya kulalamikiwa na soka letu haliendi mbele kama Taifa.
Hivi karibuni tu kuna sakata la kupanga matokeo ya mechi za mwisho ligi daraja la kwanza ambalo pana tetesi yeye kuhusika, wakati hilo likiendelea akajipachika kuhakikisha klabu ya Yanga inafanya uchaguzi wa viongozi wake mwaka huu.
Hata hivo hakuna kilichoendelea mpaka serikali kuingilia kati na wao TFF kupanga utaratibu wa uchaguzi kupitia kamati yake ya uchaguzi. Hivi majuzi tu klabu yenyewe imeweka utaratibu wa uchaguzi ambao hauendani na wa TFF na rais wa klabu hiyo kutoa shutuma dhidi ya TFF kupanga njama za kuhakikisha hagombei nafasi hiyo.
Mambo ni mengi ila naona ni jambo la busara kwa mheshimiwa huyu Jamal Malinzi kama kiongozi wa TFF kuona umuhimu wa kuwajibika. Tukumbuke hata 'electronic ticketing' imeshindikana licha ya maagizo toka kwa Waziri Mkuu na Waziri mwenye dhamana ya michezo. Tafakari kaka.