Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,883
Uchaguzi wa Mwaka huu wa TLS ni uchaguzi muhimu zaidi tangia tupate Uhuru.
Mawakili tusikubali kabisa hoja ya kwamba TLS kuna siasa za vyama. Hii hoja itatugawa na kutupoteza kutoka lengo kuu la kuwa na TLS imara itakayopigania haki za Mawakili kufanya kazi bila kutishwa, itakayowajibia Majaji wanaposemwa hadharani na viongozi wa kisiasa wasiofahamu lolote kuhusu ugumu wa kazi hiyo, wakati Katiba ipo wazi nini kifanyike iwapo kuna tuhuma dhidi ya Jaji, itakayowatetea Mawakili wa Serikali kwamba si kweli wapo watano tu walio bora, itakayowatetea wananchi wanapoonewa na kuwa victims wa trial through media, itakayoongoza michakato ya mabadiliko ya kisheria kama vile Media Service Act na Cyber Crimes Act, itakayoongelea Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kukamata watu kwa makosa ambayo yanayakiwa yachunguzwe na vyombo mahsusi, Wakuu wa Mikoa kuwa-parade hadharani watoto wanaolindwa na Law of the Child Act katika kile wanachokiita vita dhidi ya nini sijui, itakayowalinda Mahakimu dhidi ya matatizo yanayotokona na wao kuwa na Viongozi wa kisiasa kama waamuzi wa kinidhamu chini ya Judicial Services Act, TLS itakayolisaidia Bunge kuwa msimamizi independent wa Serikali, TLS itakayosimamia Mahakama kuwa HURU.
Hebu tuone hii hoja ya siasa imetoka wapi, na kama ina mantiki yoyote. Rais wa sasa wa TLS ni muajiriwa wa Tanzania Women's Bank inayomilikiwa angalau kwa kiasi fulani na Serikali (ya CCM). Ukitaka kunyumbulisha kwa lengo maalum, unaweza fikia conclusion kwamba yeye ana uhusiano wa kisheria na Serikali ambayo aghalabu atahitajika kutofautiana nayo katika majukumu yake. Mawakili tulimchagua bila kujali hayo (tulipatia au kukosea quality-wise ni suala lingine ambalo ni risk ya ki-demokrasia unapochagua Kiongozi). Na safari hii alichukua forms kugombea tena.
Katika wagombea wa sasa wa nafasi hiyo ya Rais yupo Mgombea ambaye mwka 2015 alichukua forms za kugombea Urais wa nchi hii kupitia CCM (na all the attendant connotations arising).
Yupo mgombea ambaye alikuwa Mwanasheria wa NHC; inayomilikiwa na Serikali.
Wapo Mawakili wawili wenye mashabihiano na CHADEMA lakini wana Kampuni zao binafsi za uWakili.
Yumo Wakili ambaye pamoja na muda mrefu kutambulika kama Champion wa kupigania utawala wa sheria nchini; juzi katangaza kujitoa katika jopo la Mawakili ambao walijitolea kufungua case kupingana na vifungu vya Sheria ya Habari inayolalamikiwa sana na wadau mbalimbali nchini.
Katika wigo kama huo, ni nani anaweza kusema, na akaungwa mkono na science kwamba TLS imeingia katika siasa? Siasa ya chama kipi hasa kati ya hivyo vyenye mashabihiano na wagombea hapo juu?
Waziri wetu wa mambo ya sheria ni Mbunge kupitia CCM. Speaker wa Bunge ni Mbunge kupitia CCM.
Naibu Speaker alichaguliwa kwa ticket ya CCM muda mfupi baada ya kuachia nafasi ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali (alichukua lini card ya CCM ni suala linalohitaji kufanyiwa uchunguzi huru Mahakamani huko mbeleni. Najua ipo siku litaibuka tu hili suala).
Judge Mkuu mstaafu kabla ya huyu wa juzi aligombea kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM (umewahi sikia mara ngapi hii duniani?). Huyu alikuwa Mwenyekiti wa jopo la Mahakama ya Rufaa lililoamua case ya Mtikila (RIP) kuhusu Mgombea binafsi; na tulipokea maamuzi kwa mikono miwili ingawa hukmu hiyo ilimfanya mpaka Judge Mkuu Mstaafu Sammata kuandika makala ndefu sana kuichambua. (Hivi uongozi wa sasa waTLS kwa nini haumualiki huyu rafiki wa RULE OF LAW kuwa Mgeni rasmi ilicaje tujadili naye changamoto za kiSheria kipindi hiki? Itakuwa na tija mno kuliko sijui mambo gani)
List ni ndefu.
Tuko timamu sana; na tunamkumbusha kila mwenye kusikia kuhusu hilo.
Tufanye uchaguzi wetu kwa Uhuru amani na bila kubugudhiwa wala kuelekezwa na mtu awaye yote, na tumchague yule ambaye kila mmoja anamtegemea. Wasitushangae wananchi ambao wana matumaini mapya kwamba TLS itawapigania katika changamoto lukuki za sasa.
Mwanasheria kabisa anafikiria kuifuta TLS? Au TLS ifikirie kumfuta yeye Uanachama labda.
Me nafikiri kila mwenye vinasaba vya Sheria (awe hata Law school) anategemea tutachagua vizuri. Tusiwaangushe wa-Tanzania.