Uchaguzi wa TLS Tundu Lissu hawezi kushinda.!

magode

JF-Expert Member
Oct 2, 2014
2,204
3,337
Wanabodi
Salaam;

Uchaguzi wa chama cha wanasheria Tanzania TLS.wa mwaka huu umevutia na kujulikana wananchi wengi sana mwaka huu ukilinganisha na wengine.

Kilichosababisha kujulikana ni serikali yenyewe ilipoanza kuonyesha uoga wa wazi wa kumuogopa mwanasheria wa chademaTundu lissu. Ukizingatia Lisu mwenyewe alivyo mwanaharakati,walipoonyesha kumuogopa tayari akaona km ameshashinda uchaguzi.

Lkn ukweli ulivyo kwa mawakili wenyewe,kati ya wagombea wote 5 Tundu Lissu ndo mgombea dhaifu kuliko wote. Sema jambo hili linakuzwa sana na akina Harrison mwakyembe kwa uoga wao usio na maana kabisa.

Hao wapiga kura wenyewe wanamuogopa Lissu,hivi utampaje kura mtu ambae hata ushauri wako hawezi kuukubali!!? Nawashauri wanasiasa wakae kimya wawaachi wanasheria wafanye maamuzi yao. Tundu lissu hawezi kushinda kwa namna yoyote ile.

Lissu ni mbabe hawezi kuwa Rais wa TLS. Serikali iache kuingilia kwa sababu itaonekana km akishindwa ni kwa sababu ya hizo figisufigisu..wakati ukweli hata wakikaa kimya tu hawezi kushinda.
 
Kwa taarifa yako serikali ndiyo inewazindua mawakili kuwa Lissu ndio anawafaa kuwa rais wao.
Majuzi mkulu kasema MTU akikamatwa na kesi inayoonekana ushahidi upo akija wakili kumtetea weka ndani na yeye. Jee huyo Rais wa TLS wa sasa ametolea tamko gani jambo hilo? Maana kwa nchi hii kauli ya rais ni kama sheria.
Jee rais wa TLS angekuwa mtu wa aina ya Lissu kauki ile ingepita hivihivi?
Tunahitaji hata sie RAIA wa kawaida kuwa na kiongozi wa TLS imara ili mawakili wasiwe na woga na watuwakilishe wakiwa imara. Hao mawakili vibaraka wa watawala watafanya TLS iwe dhaifu kama ilivyo sasa yenye kazi ya kukusanya ada tuu
 
Binafsi mimi kama wakili msomi kura yangu kwa Tundu lissu ipo wazi wala si suala la kificho.
 
Wanabodi
Salaam;

Uchaguzi wa chama cha wanasheria Tanzania TLS.wa mwaka huu umevutia na kujulikana wananchi wengi sana mwaka huu ukilinganisha na wengine.

Kilichosababisha kujulikana ni serikali yenyewe ilipoanza kuonyesha uoga wa wazi wa kumuogopa mwanasheria wa chademaTundu lissu. Ukizingatia Lisu mwenyewe alivyo mwanaharakati,walipoonyesha kumuogopa tayari akaona km ameshashinda uchaguzi.

Lkn ukweli ulivyo kwa mawakili wenyewe,kati ya wagombea wote 5 Tundu Lissu ndo mgombea dhaifu kuliko wote. Sema jambo hili linakuzwa sana na akina Harrison mwakyembe kwa uoga wao usio na maana kabisa.

Hao wapiga kura wenyewe wanamuogopa Lissu,hivi utampaje kura mtu ambae hata ushauri wako hawezi kuukubali!!? Nawashauri wanasiasa wakae kimya wawaachi wanasheria wafanye maamuzi yao. Tundu lissu hawezi kushinda kwa namna yoyote ile.

Lissu ni mbabe hawezi kuwa Rais wa TLS. Serikali iache kuingilia kwa sababu itaonekana km akishindwa ni kwa sababu ya hizo figisufigisu..wakati ukweli hata wakikaa kimya tu hawezi kushinda.
Utakuwa na tatizo la miundo mbinu kichwani. Umekiri wazi kuwa Serikali yako inamhofia Lisssu na inapambana kwa hali na mali lakini bila aibu ukamwaga hisia zako kuwa Lissu hatashinda.

Kwa kifupi tu, acheni TLS ifanye uchaguzi wake kwa uhuru na kwa utaratibu. Vitisho na zuio la Mahakama vinaonyesha kiwango cha hofu ya Serikali na CCM dhidi ya Lissu.
 
Back
Top Bottom