Uchaguzi wa Meya Manispaa ya Ilala waahirishwa, kwa amri ya Mahakama

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,733
239,339
Hii ni baada ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ndugu Isaya Mngurumi kutangaza rasmi kwamba tarehe 9 January , 2016 kuanzia saa 4 asubuhi Baraza la Madiwani litakutana kwenye ukumbi wa Karimjee ili kuchagua Meya na Naibu wake.

Kama inavyofahamika dunia nzima, ni kwamba idadi ya Madiwani wa UKAWA inawazidi kwa mbali sana wale wa CCM.

Kila la heri UKAWA, kila la heri wana Dar es salaam, sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, machozi ya mama lishe hayatapotea bure.

====================

UPDATE

Uchaguzi wa Meya manispaa ya ILALA umeairishwa tena leo kutokana na Zuio la Makahama ya kisutu kufanya Uchaguzi Leo! Kwa ufupi Mahakama imetoa "Stop Order" ya Uchaguzi hadi hapo itakapo tangazwa tena!

Mkazi wa Dar, Elias Nawera alifungua zuio la Uchaguzi huo jana jioni.
 
Last edited by a moderator:
Baada ya vile viti maalum kutoka kisiwandui na kibanda maiti kuzuiliwa hatutegemei tena uchaguzi kuahirishwa .
 
Mungu aepushe yasije tokea kama yale ya Tanga.
It is very true.
Ukawa wasiwe na overconfidence.
Watambue kuwa 'timu' ya CCM ndiyo mabingwa wa dunia kwa ufungaji wa magoli ya mkono!
Tujikumbushe tukio la Tanga, pamoja na CUF kuwa na madiwani 20 jijini humo na CCM kuwa na madiwani 17, lakini kwa maajabu makubwa Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji hilo alimtangaza mgombea wa udiwani kwa tiketi ya CCM kuwa ndiye aliyeshinda Umeya kwa kupata kura 19 dhidi ya kura 18 za mgombea wa CUF!
 
Last edited:
It is very true.
Ukawa wasiwe na overconfidence.
Watambue kuwa 'timu' ya CCM ndiyo mabingwa wa dunia kwa ufungaji wa magoli ya mkono!
Tujikumbushe tukio la Tanga, pamoja na CUF kuwa na madiwani 20 jijini humo na CCM kuwa na madiwani 17, lakini kwa maajabu makubwa Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji hilo alimtangaza mgombea wa udiwani kwa tiketi ya CCM kuwa ndiye aliyeshinda Umeya kwa kupata kura 19 dhidi ya kura 18 za mgombea wa CUF!
Asante sana mkuu .
 
WAPO WAJUMBE WATATOKA ZANZIBAR KUJA KUCHEZA RAFU HAPO KARIMJEE/
fununu!
======
idadi ya madiwani wanafahamika!
what a shame behind!
 
UKAWA ishajifia zamani baada ya kugombea ruzuku. Hata hiyo, UKAWA bila Lipumba na Makaidi(rip), ni kikundi fulani cha wajasiriamalisiasa.
 
Mbona Gaidi dhaifu lenye uproffesor wa kichina Linaishi Msoga..

Ndo hilo unalolizungumzia..!!?
 
Ukawa wawe makini sasa ccm wamezoea fitina mara utasikia ccm imechukua kiti cha umeya wa ilala
 
Hii ni baada ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ndugu Isaya Mngurumi kutangaza rasmi kwamba tarehe 9 January , 2016 kuanzia saa 4 asubuhi baraza la madiwani litakutana kwenye ukumbi wa Karimjee ili kuchagua Meya na Naibu wake ,

kama inavyofahamika dunia nzima , ni kwamba idadi ya madiwani wa UKAWA inawazidi kwa mbaali sana wale wa ccm .

Kila la heri UKAWA , kila la heri wana Dar es salaam , sauti ya wengi ni sauti ya Mungu , machozi ya mama lishe hayatapotea bure .
Kwa kweli sijui ni lini maccm watakubali kushindwa kwa njia ya karamu halali ya wananchi, ila watanzania wapenda haki tusikatishwe tamaa
 
Back
Top Bottom