Uchaguzi wa mbunge Longido; Spika Ndugai kupeleka barua NEC

Reucherau

JF-Expert Member
Nov 26, 2014
756
1,740


SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, amesema wakati wowote kuanzia sasa ataiandikia barua Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iweze kuandaa ratiba ya uchaguzi mdogo katika Jimbo la Longido mkoani Arusha.


Uamuzi wa uchaguzi mdogo katika jimbo hilo umekuja baada ya Mahakama ya Rufaa kutupilia mbali rufaa iliyokatwa na aliyekua mbunge wa jimbo hilo, Onesmo ole Nangole, kupinga uamuzi wa awali wa mahakama hiyo uliotengua matokeo yaliyompa ushindi mbunge huyo.

Akizungumza jana, Spika Ndugai alisema kwa mujibu wa sheria za uchaguzi, anapaswa kuandika barua hiyo kuiarifu NEC juu ya kuwapo nafasi ya kiti cha ubunge katika jimbo hilo baada ya Mahakama ya Rufaa kuwaandikia barua ya kutengua nafasi ya ubunge.

Alisema barua hiyo itawasilishwa hivi karibuni kwenye ofisi ya tume iweze kuandaa ratiba ya uchaguzi na kuweka utaratibu wa wagombea watakaoshiriki kwenye uchaguzi huo, jambo ambalo linaweza kuvisaidia vyama vya siasa kuandaa wagombea.

“Kwa sasa nipo kwenye mchakato wa kuandika barua kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi iweze kuandaa utaratibu wa kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa jimbo la Longido, jambo ambalo linaweza kuwasaidia vyama vya siasa kuandaa wagombea,” alisema Ndugai.

Alisema kutokana na hali hiyo, uchaguzi mdogo utafanyika baada ya tume hiyo kumaliza mchakato huo ambao kwa mujibu wa sheria unatarajiwa kufanyika ndani ya siku 90.

Alisema mpaka sasa jimbo hilo halina mwakilishi, hivyo basi kufanyika kwa uchaguzi huo ni muhimu wananchi waweze kupata mwakilishi wao bungeni ambaye ataweza kutetea maslahi ya wapiga kura wake na taifa kwa ujumla.

Juzi, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, Ramadhan Kailima alisema anasubiri barua ya utenguzi huo kutoka kwa spika wa bunge iweze kufanya maandalizi ya uchaguzi mdogo wa jimbo hilo.

Alisema kulingana na sheria ta taifa ya uchaguzi kifungu namba 37(3) sura ya 343, endapo mbunge atajiuzulu, kufariki dunia na kutenguliwa na mahakama au kwa sababu nyinginezo, Spika atamuarifu Mwenyekiti wa Tume na kutangaza kwenye gazeti la serikali kwamba kuna nafasi katika kiti cha ubunge.
 
Hapo vyama vya upinzani kwa umoja wao wanapaswa kuweka mtu mmoja makini sana ili walishambulie jukwaa kwa pamoja!!
 
Najua attention ya siasa zooote za tz itahamia Longido, na sijui katazo la mikutano ya siasa litasitishwa kwa muda!?
 
Huu ni mwaka wa majuto kwa ccm maana Nangole anarudi kwa kishindo kuliko alivyoshinda awi .Ccm mwaka huu watajibeba na Daud Albert Bashite wao.
 
Kwani mwanzo alikuwa ameshindwa nani??Labda mumuweke jela Lema safari hii tuna kula nanyie sahani moja.
Mwambie atukane tena kama akibahatika kutoka..aone kama krismass hatailia tena kisongo
 
wema usikubali wema. [HASHTAG]#longido4wema[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom