Uchaguzi wa Kenya vs tanzania

Uchaguzi wa Kenya vs tanzania

Naona tunaushobokea sana uchaguzi wa Kenya,TV karibia zote zinaonyesha huko je je. Wao.huwa wanaushobokea.uchaguzi wetu kama hivi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, namna unavyoendesha familia yako huko ndani kuwa makini sana. Ukiona wanao na mkeo wanaanza kuzungumza maendeleo ya jirani kila mara unapokuwa around, jitafakari mara mbili. Au ukisikia wanao kila wakati wanakuambia kina fulani wana raha, baba yao huwa anawaletea hiki na kile, ujue huo ni ujumbe wako. Au ukemee au ubadilike haraka sana maana ujue unapoteza dola. Kwa namna siasa za ndani zinavotengenezwa sasa hivi, uzalendo unapotea kwa kasi ya hali ya juu sana!!! Inasikitisha mno mno mno mnooo!! Mzalendo aliyekuwa amebaki ni rais na baraza lake, (naona na wao wametolewa kwenye kundi la uzalendo maana wanayoyafanya ni ya kipumbavu). Tumebaki na mzalendo mmoja, na wanafiki wengi wanaomshabikia mzalendo mmoja. Uchaguzi wa Kenya tayari umekuwa na pande mbili, wa Raila anayeungwa mkono na JPM (Raila amethibitisha katika kampeni zake na ameonekana mara kadhaa huko chattle hata kama jpm yuko kimya) na wa Kenyatta anayeungwa mkono na Lowassa. Sasa, kitendawili kiko hapa: Raila ni mgombea siyo Rais, JPM ni Rais tayari tena ...! Kenyatta ni Rais tena amesifiwa mara kadhaa kuwa ni mwana demokrasia na baadhi ya matukio yameakisi hilo, Lowassa siyo Rais wala mgombea maana huku hakuna uchaguzi. Sasa hebu fanya hiyo cross multiplication uje uniambie umepata jibu gani....
Kwa vyovyote, kwa hali ilivyo nchini na chuki zilizopandikizwa kwa namna mbalimbali, Mshindi wa urais Kenya kesho atatangazwa, lakini mwangwi wa sherehe zake utakuwa Tanzania. Je ni Kenyatta au Raila? Kama ni Kenyatta atakuwa ametetea, kama ni Raila itakuwa ni upinzani umeshinda Kenya, kwann siyo Tanzania? kuna mengi yatatokea.. Muda utaamua
 
Back
Top Bottom