Uchaguzi wa igunga:dalili ya ccm kudondoka

NEW NOEL

JF-Expert Member
May 21, 2011
861
403
Kwanza nianze kwa kusema kuwa mimi sipo upande wa chama chochote kinachoshiriki kampeni za ubunge huko Igunga. Ila yanayoendelea huko yanatoa picha halisi ya jinsi kila chama kinavyokubalika katika jamii ya wa TZ,kwa jinsi vyama vinavyoendesha mambo yao.
CCM ni chama ambacho ukikitazama utaona kuwa kinazidi kuporomoka na kutokukubalika mbele ya macho ya Watanzania wengi.
Ninasema kuwa CCM hakina mvuto mbele ya macho ya Wa-TZ kwa sababu kinatumia muda mwingi kupambana na CHADEMA kuliko kujitangaza wao kama wao.
1. CCM kinatumia karata ya udini kupambana na CHADEMA kwa kujaribu kuwahadaa waislamu hususani waliopo Igunga kwamba CHADEMA ni chama cha Wakristo na hakiwajali Waislamu. Mf. Suala la mkuu wa wilaya kuvuliwa kitambaa cha kichwani na CCM kugeuza suala hilo kuwa la kidini kwa kudai yule Mama(mkuu wa Wilaya) halinyanyaswa kwa sababu ya dini yake.
2. CCM inatumia nguvu ya pesa iliyopitiliza ili kukubalika kwa wananchi mf. Kugawa fulana za CCM na hata mpango wao wa kutumia Helikopta. Kama CCM ingekuwa na mvuto mbele ya wana Igunga isingetumia nguvu hiyo ya pesa kabisa. Kulikuwa kuna sababu gani ya kumpeleka Mzee Mkapa kwenda kufungua kampeni,kama bado kinakubalika?
3. Kuna sababu gani ya CCM kununua shahada za kura?
4. CCM kinatumia udhaifu wa watu wa Igunga ususani wale wasio na elimu ili kuendelea kuongoza Igunga.
SABABU HIZI NA NYINGINE NYINGI ZINADHIBITISHA KUWA HATMA YA CCM KUENDELEA KUSHIKILIA DOLA HIPO SHAKANI. NA NI NAFASI NZURI KWA CHADEMA KUJITANGAZA MBELE YA WA-TZ KWA SABABU KINAONYESHA KUWA KATIKA NAFASI NZURI.

HUU NI MTAZAMO WANGU:
1. CCM=TUSHIKILIE TULICHONACHO
2. CHADEMA= SISI TUNANYAKUA KILA JIMBO
3. CUF NA VYAMA VINGINE=NA SISI TUMO(BORA LIENDE).
CCM wanapaswa kutambua kuwa ''hakuna marefu yasiyo na ncha'' na siku moja kitakuja kugeuka kuwa chama cha upinzani.

Mimi nimeandika haya bila ya kuegemea upande wa chama chochote kile. Na sishabikii chama chochote kinachoshiriki uchaguzi huko Igunga.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom