samsonp
Member
- Aug 9, 2015
- 41
- 8
TULIKOTOKA NI MBALI SANA NA TUNAKOKWENDA NI MBALI SANA PIA.Wakati nikiwa mdogo niliamini kila anayeishi nje ya Tanzania maisha yake ni bora kuliko sisi waTanzania,niliposikia mtu anakwenda au anatoka Uganda,Sudan,Malawi niliamini maisha yake hayana matatizo hata kidogo.
Inawezekana kwa sababu ya ugumu wa maisha yetu ya kipindi hicho ya chini ya dola moja yalinifanya niamini kwamba matatizo ya maisha yako Tanzania pekee. Nilipoanza kusoma historia katika elimu ya msingi,ndipo nilipoanza kuamini kwamba tulikotoka ni mbali sana.Nilijaribu kutafakari kuhusu uhuru wa 1961 na muungano wa 1964 sikupata picha,niliendelea kuamini tulikotoka ni mbali hasa nikitazama jinsi taiga letu lilivyojengwa katika misingi ya utu,isiyo na ubaguzi wa dini wala kabila,niliamini tumetoka mbali. Kufuatia sera ya Rais Mkapa ya ubinafsishaji binafsi niliamini tunakokwenda ni mbali sana.Katika kipindi hicho ndipo niliposhuhudia Rais Mkapa akipewa koleo iliyojaa dhahabu pale Mgodi wa dhahabu Nzega.Niliamini tunakokwenda ni mbali sana. Mwaka 2005 ndio mwaka ambao nilibadilika na kuamini kwamba ile safari yetu imekaribia.Maisha bora kwa kila mtanzania,ari mpya nguvu mpya kasi mpya na pia ajira kwa vijana niliamini ndio wakombozi wamefika na muda umewadia.(Maisha bora kwa kila mtanzania PART 1). Baada ya miaka mi5 tu niliamini tumekosea njia na tumerudi nyuma hatua 1000,tunakokwenda ni mbali sana. Kuanzia mwaka 2005-2010 niliamini 100% kwamba hatukutumia kanuni za mabadiliko "principles of changes" na "uchunguzi" na badala yake tulifanya "uchaguzi" pekee.Niliamini "Changes do not happen because there is an announcement" ilikuwa ni muda wa kufanya "uchunguzi" yakinifu na si "uchaguzi pekee". Katika kipindi hicho cha ukubwa wangu niliamini kwamba kama Nyerere aliweza basi Mh Mbowe,Zitto,dkt Slaa na wengine wengi wasingeshindwa kutufikisha kanaani kwa kanuni safi "principles of changes".Ni viongozi shupavu waliohubiri tatizo kubwa linaloendelea kuitafuna Afrika na kusababisha machafuko makubwa mashariki ya kati Arab spring".Afrika nako watu wakizidi kuzikimbia nchi zao kuelekea ulaya. Changes move from what we had known and done through a period of transition to arrive at a desired new way.Mwaka 2015 hatimaye nashuhudia filamu yangu (Maisha bora kwa kila mtanzania part 2) ambayo Star ni Mh Edward Lowassa na washiriki wengine lukuki,naamini tena safari yetu ni ndefu na tumerudi nyuma hatua 2000 tena. Bado niko naiangalia ila ngoja nikusimukie kiduchu kinachoendelea katika Filamu hii. 1.Rushwa na ufisadi havikemewi wala kuhubiriwa tena zaidi ya ahadi za benki ya bodaboda na wakulima. 2.Ukigusia suala la rushwa na ufisadi Leo unaambiwa "lete ushahidi" na kama hauna "kaa kimya". 3.Naona pia kuomba kura kwenye nyumba za ibada sasa ni jambo la kawaida,ukiuliza unajibiwa "tunataka mabadiliko" ukiuliza mabadiliko yapi?..unatukanwa. 4.Namuona Said Kubenea aliyembana Sumaye siku ya kutangaza nia kuhusu kuuzwa nyumba za serikali na sakata zima huku akiachwa kinywa wazi kwa majibu mepesi,Leo jambo hilo kamsukumia magufuli. 5.Wakati naota hayo yote,Mara nashtuka kitandani kwangu lakini pembeni ya kitanda changu kuna TV,nakutana na mgombea amevaa nguo za kijani anasema "atapiga vita rushwa"........??????,nilishangaa TAFAKARI,CHUKUA HATUA