Uchaguzi ukirudiwa CUF akishinda CCM watakabidhi nchi?

mdundo ngoma sana

JF-Expert Member
Jan 2, 2016
1,002
955
Wana jf wenzangu iwapo uchaguzi ukirudiwa ccm wapo tayari kukabidhi madaraka kwa cuf au ndo mengine yatazaliwa
 
Msamiati wa kushindwa ccm huwa haupo,ona walivyojiaibisha Ilala,kwa kukimbia,hesabu zao za ajabu sana,nyie mpo na madiwani wachache bado munaamini mtashinda umeya!? Zanzibar watashinda hata kwa magoli yote
 
CCM ifike mahali wawe na aibu.. Wakubali kushindwa,, wanaludia uchaguzi wa nn wakati dunia nzima inajua kuwa,, Maalim Sefu ni mshindi,,wasisubili damu imwagike waachie nchi tu kwa amani.
 
kilichoharibu uchaguzi bado hakijarekebishwa, si ajabu huu nao ukaharibika.
 
Ishinde mara ngapi? Ikishinda tena uchaguzi utarudiwa. Cuf hawaruhusiwi kushinda
Sasa wanafanya uchaguzi wa nini kama hawapo tayari kushindwa? Watangaze tu kwamba zanzibar ni nchi ya kifalme na ccm watatawala milele,, mzee wa kutumbua majipu kimya,, kana kwamba uchaguzi wa zanzibar siyo jipu.
 
Sasa wanafanya uchaguzi wa nini kama hawapo tayari kushindwa? Watangaze tu kwamba zanzibar ni nchi ya kifalme na ccm watatawala milele,, mzee wa kutumbua majipu kimya,, kana kwamba uchaguzi wa zanzibar siyo jipu.
Wanawadanganya wazanzibar
 
Cuf kuna baadhi ya maeneo walifanya magumashi na wanalijua hilo, ila hawatawaambia wala kukiri wazi...
 
Cuf kuna baadhi ya maeneo walifanya magumashi na wanalijua hilo, ila hawatawaambia wala kukiri wazi...
Nakubaliana na wewe CUF baadhi ya maeneo walifanya magumashi..... Uchaguzi ulikuwa urejewe katika hayo baadhi ya maeneo.

Hayo baadhi ya maeneo, basi wakala wa CCM aliyepewa dhamana ya kusimamia hajaona hayo magumashi aje ayaone Jecha aliyeko makao makuu Zanzibar na wewe uloyekuwepo huku kwenye JF?

Tutakuja kusikia vyama vitakavyoshiriki huo uchaguzi wakilalamika kwamba wamefanyiwa foul. Wanachoamini wao kwa vile CUF hatoshiriki na wenzao wanaounda umoja wa UKAWA, wanaweza wakapata kiti japo cha udiwani, lakini wataangukia pakavu na hapo ndipo watakapokuja humu kwenye vyombo vya habari na kutulalamikia.

Uchaguzi hauwezi kurejewa kwa kusimamiwa na tume iliyovuruga uchaguzi ulopita. Hilo haliwezekani na ni dhambi kubwa sana kutumia hard earned tax payers money kwa uharibifu kama hivi. Its a crime worth of death punishment
 
Back
Top Bottom