Uchaguzi.. tutashuhudia mengi......

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
31,234
31,332
Waziri apeleka udongo Israeli kuombea mvua
na Rodrick Mushi, Siha
MBUNGE wa Siha, Aggrey Mwanry, amechukua udongo wa Wilaya yake ya Hai na kuupeleka nchini Israel kwa ajili ya tambiko la kuombea wapiga kura wake waondokane na ukame na njaa.
Mwanry, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), alieleza hayo juzi kwenye mahafali ya darasa la saba katika Shule ya Punchimin iliyopo Kijiji cha Karansi, wilayani humo, mkoani Kilimanjaro.
Alisema jimbo lake limekuwa likikabiliwa na tatizo la ukame kwa muda mrefu linalosababisha wananchi kutaabika kwa uhaba wa chakula, hivyo amelazimika kuchukua udongo na kuupeleka nchini Israel alipozikwa Yesu, kwa kuwa ni nchi yenye ahadi na baraka.
“Mimi nimekuwa nikiumia sana pindi ninapoona wananchi wa jimbo langu mkitaabika na kuteseka kwa ajili ya tatizo la njaa. Watu wengi watajiuliza ni kwanini Mwanry ameamua kufanya hivyo, ila ni imani yangu kuwa tatizo hili litaisha tukimtegemea Mungu,” alisema.
Alisema kutokana na maombi hayo, tayari hali ya mvua inaimarika wilayani Siha, huku wananchi wakiwa na matarajio makubwa ya mazao katika msimu huu.
Alisema mpaka sasa wilaya hiyo tayari imekwishaanza kupandikiza mazao huku mengine yakionekana kuota katika sehemu mbalimbali za wilaya hiyo.
Hata hivyo, baadhi ya wadadisi wa masuala ya kisiasa na kiimani walisema hatua hii ya mbunge kutambika kwa udongo ni ya kishirikina.

Source: Tanzania Daima
 
Aisee hii ni kali kwelikweli, kwani hapa Tanzania hakuna wanamaombi? Ajabu kwelikweli na sitashangaa kama atakwenda kwa mganga wa kienyeji kuomba apate ubunge
 
Kuchaguana hasa kwenye Majimbo ya Kilimanjaro sio lelemama. Sio pesa, umaarufu wala wadhifa wako serikalini utakaokusaidia. Natamani Tanzania nzima tufikie kiwango hiki ili mambo yaweze kwenda.
 
Back
Top Bottom