Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,042
- 10,787
Uchaguzi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) umetinga mahakamani baada ya wakili Godfrey Sabato Wasonga kufungua kesi mahakama Kuu Dodoma kwa madai kuwa uchaguzi huo uahirishwe kusubiri bunge likafanye mabadiliko ya kanuni.
Kuna taarifa kuwa kesho katika mahakama kuu ya Dar es Salaam wakili Onesmo Mpinzile atafungua kesi yenye madai hayo hayo. Mpinzile Ni kada mtukufu wa Chama cha Mapinduzi.
* Ninachohisi hapa ni kwamba Mwakyembe anataka kufanya figisu bungeni ili kanuni zibadilishwe na hatimaye Lissu akose sifa.( Haya ni mawazo yangu jamani)
NOTE: Wakili Wasonga aliwahi kumshitaki Tundu Lissu mara mbili ili aondolewe kwenye ubunge. Kwa ufupi huyu ni wakili wa kujitegemea lakini anatumiwa na Chama cha Mapinduzi.