Lengeri
Senior Member
- Jul 3, 2009
- 180
- 18
Mchakato wa kuwania nafasi mbalimbali ndani ya Chama hicho ulianza Julai 15 mwaka huu, na mpaka sasa ni mtu mmoja aliyerudisha fomu katika nafasi ya Mwenyekiti Taifa wakati nafasi ya Katibu Mkuu hakuna aliyerudisha fomu mpaka sasa.
Katika ngazi ya Makamu Mwenyekiti Bara, waliorudisha fomu mpaka sasa ni watu wawili, na Zanzibar aliyerudisha fomu katika nafasi hiyo ni mmoja tu, wakati katika nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar ni Mtu mmoja na Bara hakuna aliyerudisha fomu mpaka sasa.
Kitengo cha wanawake Taifa waliorudisha fomu ni watu wawili, kitengo cha Vijana taifa ni mmoja, Makamu Mwenyekiti kitengo hicho ni wawili na katika kitengo cha wazee taifa ni wawili.
Kwa upande wa majimbo, kati ya majimbo 239 ni 182 tu ndiyo yamerudisha, wakati katika ngazi ya taifa, ujumbe wa halmashauri kuu ya taifa ni fomu 74 tu zilizorudishwa kati ya 152 zilizochukuliwa.
Aidha, Mwenyekiti wa sasa wa chama hicho, James Mbatia na Katibu Mkuu wake, Samuel Ruhuza bado hawajachukua fomu.
Mchakato wa kuchukua na kurudisha fomu ndani ya NCCR Mageuzi unatarajia kumalizika Octoba 31, mwaka huu.
CHANZO: NIPASHE
Lengeri.