Uchaguzi MKuu na Kiporo cha Mchakato wa Katiba

Uchaguzi MKuu na Kiporo cha Mchakato wa Katiba

sauverleau

Member
Joined
Nov 22, 2013
Posts
7
Reaction score
6
Ndugu watanzania wenzangu,

Kwa historia, Tanzania yetu imezoea kwenda kwa MATUKIO na kila tukio jipya hulifunika la nyuma yake na mwisho viongozi wetu wamekuwa wakitumia hiyo kama "loophole" kufanikisha mambo mbalimbali kwa faida hasa ya CHAMA na WACHACHE.

Tangu CCM impitishe ndugu Magufuli, (ambaye binafsi pia namkubali) kumekuwa na maneno meeengi lkn kubwa hasa kwamba CCM imecheza karata muhimu sana na kwamba sasa ni ANGUKO LA UPINZANI.

Inawezekana ukweli Magufuli ni mgombea anayejinadi kwa utendaji wake, (hii haifuti kwamba yeye sio malaika) kwahiyo atakuwa na mapungufu yake, lkn walau amejitahidi, kazi alofanya unaweza ukaonesha.

Ni dhahiri kuwa wengi kwa ushabiki tumeishia kusema kuwa Magufuli ni jembe na kufika mbali kusema atawagaragaza wapinzani.

Hii imenistua kwa sababu tumeshasahau tukio lililotangulia uliokuwa mchakato wa kupigia kura ya maoni katiba pendekezwa mchakato ambao uligubikwa na mambo mengi ya ajabu ambayo UKAWA pamoja na wananchi wengi tulikuwa na mtazamo wa kususia kura hiyo. Kazi kubwa ambayo UKAWA waliifanya ilikuwa kufanya lobbying kwa wananchi kuwa wasiipigie kura katiba hiyo. Bahati nzuri sana zoezi hilo halikufanikiwa, na ipo wazi kuwa Rais ajaye ndiye atakuwa na kazi ya kumalizia kiporo hiki.

Sasa, je hatuoni kuwa itakuwa rahisi sana wananchi kuipata katiba yetu kama tutawapa kura wapinzani kuanzia wabunge hadi kura ya Rais? achilia mbali Magufuli na uwajibikaji wake, kwasababu litakapokuja swala la katiba ni wazi hatapenda kukisaliti chama chake ambacho kwa kiasi kikubwa ndicho kilicholazimishia mapendekezo ya wananchi yatolewe? Na juzi ameahidi kukitumikia na kulinda maslahi ya chama.

Wito wangu ni kuwa sisi katika umoja wetu kila mmoja kwa nafasi yake, tuchukue nafasi ya kuwaelekeza ndugu zetu hasa wa vijijini, ambao kwa ukweli ndio wengi wao wanaopiga kura na kama wengi tunavyosema uelewa wao ni mdogo, lkn pengine wakisikia maneno kutoka kwa mtu wa karibu (mjomba, shangazi, kaka, mtoto wa jirani, nk.) nadhani wataelewa, na hivi kampeni ya chini kwa chini itakuwa imefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Tusiwaachie UKAWA peke yao kwamba ndio watafanya kazi ya kuwaelekeza haya yote wananchi katika kipindi hiki kinachokuwa na kelele nyingi sana na mambo yetu yale ya kugawa kanga, vitenge, pombe ili mradi tu watu wawaone wagombea kuwa wanafaa.

Tunaweza kuwabadilisha ndugu zetu wa huko vijijini (hata wa mijini ambao hawajielewi) kwa kutumia hoja ya KATIBA kuwa tuchague UKAWA na sio ushabiki wa CCM ambao tutarudi kulekule kupigana juu ya katiba yetu tuliyopokwa.

Nawasilisha
.
 
Magufuli ni jembe la Mkono, la kukokotwa na Ng'ombe au La trekta? Jembe gani hilo? ufafanuzi tafadhalini. Wengine wanamuita Tingatinga, Bulldozer , ana tinga tinga nini wakati barabara zake zote maintanance ni miezi sita tu time span ?
 
Katiba zipo mbili tuu Moja ya CCM nyingine ya UKAWA... wananchi wa Sumbawanga vijijini hatuna katiba ya kuilalamikia
 
Back
Top Bottom