Uchaguzi Igunga: Chadema kutumia Helikopta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi Igunga: Chadema kutumia Helikopta

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kessy kyomo, Aug 22, 2011.

 1. kessy kyomo

  kessy kyomo Member

  #1
  Aug 22, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 72
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  [h=3]Mbio za ubunge Igunga Dkt. Slaa, Zitto kuzindua kampeni[/h]

  *CHADEMA kutumia helikopta Igunga
  *Yaanika mikakati ya kushinda jimbo
  *CCM yavuta pumzi, yasubiri CC

  Na Benjamin Masese

  VUGUVUGU la uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, mkoani Tabora linazidi kupanda
  huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikitangaza safu ya viongozi wa kitaifa watakaozindua kampeni za chama hicho Septemba 9, mwaka huu.

  Mbali na kuanika majina ya viongozi wake watakaozindua kampeni, chama hicho kina mkakati wa kutumia helikopta ili kufikia maeneo yote ya Jimbo la Igunga.

  "Kama kawaida yetu tayari helikopta imeandaliwa kwa mashambulizi ya kampeni jimbo la Igunga, lakini hatutaanza nayo, tutaanza na vyombo vya ardhini kwanza tukiona kuna ulazima, ndipo tutakaponyanyuka juu kwa juu na kumwaga sumu 'chini'."

  Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Habari Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Bw. Erasto Tumbo, wakati akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu akiwa Igunga. Alisema viongozi wa kitaifa watakaohudhuria uzinduzi wa kampeni za chama hicho ni Katibu Mkuu, Dkt. Willbroad Slaa na Naibu Katibu Mkuu Bw.Zitto Kabwe.

  Bw. Tumbo alisema kuwa tayari Kamati Kuu ya CHADEMA ilikutana juzi na kupitia majina ya wagombea 16 waliochukua fomu, ambapo kwa kuzingatia sifa na mtu mwenyewe anavyokubalika kwa wananchi wa Igunga, ilimpitisha Bw.Joseph Kashindye, kuwania kiti hicho.

  "Hapa tulipo hatujaanza kampeni, lakini wananchi wameonesha shauku kubwa ya kukiunga mkono chama chetu ili kuwaongoza, kwani wamedai kwamba kwa miaka mingi walikuwa hawajapata kiongozi wa kukaa nao na kujadiliana wanachohitaji," alisema Bw. Tumbo.

  Alisema baada ya uzinduzi huo viongozi wa kitaifa watasambaa maeneo yote ya jimbo hilo kumnadi mgombea Bw. Kashindye, ili kuhakikisha jimbo hilo linaondoke mikononi wa CCM).

  Alisema utafiti wa awali umeonesha kuwa CHADEMA itaibuka na ushindi kwa zaidi ya asilimia 80, huku vyama vingine vikigawana asilimia zilizobaki.

  Alisema CCM ina hali mbaya kuliko vyama vingine vinavyoshiriki uchaguzi huo. Alisema dalili zinaonesha kuwa wananchi wamechoka na sera za chama hicho.

  "Hadi sasa tunajua tunashinda na harakati za kumwaandaa mgombea wetu kwenda bungeni zimeanza na tutampeleka kwa maandamano hadi Dodoma na kufanya hafla fupi ya kumkaribisha,"alisema.

  Naye Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi, CCM Bw. Nape Nnauye, alisema muda wowote kuanzia sasa Kamati Kuu itakutana kumteua mgombea wa chama hicho na kutangaza siku ya kuanza kampeni.

  Akizungumza na gazeti hili jana,Bw. Nnauye alisema kauli za CHADEMA kujihakikishia ushindi ni mbinu za kuwatisha watu na wagombea wengine, lakini CCM inazichukulia kama kelele ambazo zimezoeleka kwao.

  "Hakuna chama ambacho kinatangaza mikakati yake barabarani,tunatarajia Kamati Kuu itakaa muda wowote kumpitisha mgombea mmoja na kutangaza siku rasmi ya uzinduzi wa kampeni, wao ndio wanasuasua sisi tuko imara na ushindi ni wetu kama kawaida,"alisema.

  Awali alisema CCM ina asilimia 90 za ushindi katika jimbo hilo na kuongeza kwamba kampeni za chini chini za baadhi ya vyama vya siasa zilizoanza Igunga ni mchezo wa watoto wadogo.

  "Pale Igunga, CHADEMA haina kitu hata kama wameanza kampeni za chini chini...ule ni mchezo wa watoto na kawaida ikifika saa sita usiku lazima watoto walale na ndipo tutakaposhinda. Pia tathmini tulishafanya na tumebaini zaidi ya asilimia 90 tunashinda ndio maana hatuna wasiwasi,"alisema.

  Naye Rachel Balama anaripoti kuwa Chama cha Wananchi (CUF) kinatarajia kutangaza ratiba na mikakati mingine leo.

  Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu akiwa Igunga, Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Bw. Julius Mtatiro, alisema;

  "Nipo Igunga kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi, lakini kesho nitatoa taarifa zote kuhusu kampeni za CUF."

  Naye Mwenyekiti wa Chama cha National Reconstruction Alliance(NRA) Bw. Rashid Mtuta, alisema kuwa chama chake kina nia ya kusimamisha mgombea na kinasubiri timu iliyotumwa Igunga kuangalia mazingira ya kukubalika kwake jimboni humo.

  Alisema tayari timu hiyo ya watu watano ipo kwa wiki moja sasa na inatarajia kurudi wakati wowote kuanzia leo.

  "Tunapozungumza tayari timu ya watu watano ipo Igunga kuangalia mazingira na tutatoa tamko," alisema Bw. Mtuta.

  Alisema kuwa timu hiyo inaonngozwa na Kaimu Katibu Mkuu Taifa Bw. Hassan Kisabya.

  Mwisho.
   
 2. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  CCM itaenda kunadi nini Mungu wangu!ni bora hata wasingemsimamisha mgombea!maana sielewi kwani aliyeng'atuka si wa kwao?wataenda nadi kitu gani kipya!Mangamba ni hatari tupu
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Aug 22, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Jina la Kafumu litakuwa mtaji wa CHADEMA kuchukua ushindi kule Igunga. huyu jamaa amekuwa kamishna wa madini hakuweza kuwasaidia wananchi wa Igunga zaidi ya kujijengea Dar
   
 4. koo

  koo JF-Expert Member

  #4
  Aug 22, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mungu ibariki cdm mungu wabariki wana igunga waongoze kuchagua mabadiliko wade hekima wachague mwakilishi makini mkazi wa igunga anayejua mahitaji na matatizo yao kwapamoja tutakomboa taifa letu
   
 5. kessy kyomo

  kessy kyomo Member

  #5
  Aug 22, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 72
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  [h=3]Mbio za ubunge Igunga Dkt. Slaa, Zitto kuzindua kampeni[/h]

  *CHADEMA kutumia helikopta Igunga
  *Yaanika mikakati ya kushinda jimbo
  *CCM yavuta pumzi, yasubiri CC

  Na Benjamin Masese

  VUGUVUGU la uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, mkoani Tabora linazidi kupanda
  huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikitangaza safu ya viongozi wa kitaifa watakaozindua kampeni za chama hicho Septemba 9, mwaka huu.

  Mbali na kuanika majina ya viongozi wake watakaozindua kampeni, chama hicho kina mkakati wa kutumia helikopta ili kufikia maeneo yote ya Jimbo la Igunga.

  "Kama kawaida yetu tayari helikopta imeandaliwa kwa mashambulizi ya kampeni jimbo la Igunga, lakini hatutaanza nayo, tutaanza na vyombo vya ardhini kwanza tukiona kuna ulazima, ndipo tutakaponyanyuka juu kwa juu na kumwaga sumu 'chini'."

  Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Habari Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Bw. Erasto Tumbo, wakati akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu akiwa Igunga. Alisema viongozi wa kitaifa watakaohudhuria uzinduzi wa kampeni za chama hicho ni Katibu Mkuu, Dkt. Willbroad Slaa na Naibu Katibu Mkuu Bw.Zitto Kabwe.

  Bw. Tumbo alisema kuwa tayari Kamati Kuu ya CHADEMA ilikutana juzi na kupitia majina ya wagombea 16 waliochukua fomu, ambapo kwa kuzingatia sifa na mtu mwenyewe anavyokubalika kwa wananchi wa Igunga, ilimpitisha Bw.Joseph Kashindye, kuwania kiti hicho.

  "Hapa tulipo hatujaanza kampeni, lakini wananchi wameonesha shauku kubwa ya kukiunga mkono chama chetu ili kuwaongoza, kwani wamedai kwamba kwa miaka mingi walikuwa hawajapata kiongozi wa kukaa nao na kujadiliana wanachohitaji," alisema Bw. Tumbo.

  Alisema baada ya uzinduzi huo viongozi wa kitaifa watasambaa maeneo yote ya jimbo hilo kumnadi mgombea Bw. Kashindye, ili kuhakikisha jimbo hilo linaondoke mikononi wa CCM).

  Alisema utafiti wa awali umeonesha kuwa CHADEMA itaibuka na ushindi kwa zaidi ya asilimia 80, huku vyama vingine vikigawana asilimia zilizobaki.

  Alisema CCM ina hali mbaya kuliko vyama vingine vinavyoshiriki uchaguzi huo. Alisema dalili zinaonesha kuwa wananchi wamechoka na sera za chama hicho.

  "Hadi sasa tunajua tunashinda na harakati za kumwaandaa mgombea wetu kwenda bungeni zimeanza na tutampeleka kwa maandamano hadi Dodoma na kufanya hafla fupi ya kumkaribisha,"alisema.

  Naye Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi, CCM Bw. Nape Nnauye, alisema muda wowote kuanzia sasa Kamati Kuu itakutana kumteua mgombea wa chama hicho na kutangaza siku ya kuanza kampeni.

  Akizungumza na gazeti hili jana,Bw. Nnauye alisema kauli za CHADEMA kujihakikishia ushindi ni mbinu za kuwatisha watu na wagombea wengine, lakini CCM inazichukulia kama kelele ambazo zimezoeleka kwao.

  "Hakuna chama ambacho kinatangaza mikakati yake barabarani,tunatarajia Kamati Kuu itakaa muda wowote kumpitisha mgombea mmoja na kutangaza siku rasmi ya uzinduzi wa kampeni, wao ndio wanasuasua sisi tuko imara na ushindi ni wetu kama kawaida,"alisema.

  Awali alisema CCM ina asilimia 90 za ushindi katika jimbo hilo na kuongeza kwamba kampeni za chini chini za baadhi ya vyama vya siasa zilizoanza Igunga ni mchezo wa watoto wadogo.

  "Pale Igunga, CHADEMA haina kitu hata kama wameanza kampeni za chini chini...ule ni mchezo wa watoto na kawaida ikifika saa sita usiku lazima watoto walale na ndipo tutakaposhinda. Pia tathmini tulishafanya na tumebaini zaidi ya asilimia 90 tunashinda ndio maana hatuna wasiwasi,"alisema.

  Naye Rachel Balama anaripoti kuwa Chama cha Wananchi (CUF) kinatarajia kutangaza ratiba na mikakati mingine leo.

  Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu akiwa Igunga, Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Bw. Julius Mtatiro, alisema;

  "Nipo Igunga kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi, lakini kesho nitatoa taarifa zote kuhusu kampeni za CUF."

  Naye Mwenyekiti wa Chama cha National Reconstruction Alliance(NRA) Bw. Rashid Mtuta, alisema kuwa chama chake kina nia ya kusimamisha mgombea na kinasubiri timu iliyotumwa Igunga kuangalia mazingira ya kukubalika kwake jimboni humo.

  Alisema tayari timu hiyo ya watu watano ipo kwa wiki moja sasa na inatarajia kurudi wakati wowote kuanzia leo.

  "Tunapozungumza tayari timu ya watu watano ipo Igunga kuangalia mazingira na tutatoa tamko," alisema Bw. Mtuta.

  Alisema kuwa timu hiyo inaonngozwa na Kaimu Katibu Mkuu Taifa Bw. Hassan Kisabya.
   
 6. A

  ALJOTICHI New Member

  #6
  Aug 22, 2011
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "mchakato, tuko mbioni, kamati, tunasubiri majibu ya tume" n.k. Yamekuwa ni maneno ambayo yamekuwa ni kikwazo kwa juhudi za maendeleo kwa wananchi. Nakubaliana na wewe bwana koo kwani michakato isiyo na specification of time na mikakati madhubuti ya utekelezaji ni kama ubabaishaji ulio dhahiri. Lazima tukubali kuwa kuna mambo ambayo ambayo hayhitaji tume au kuwa na michakato isiyo ya lazima kwani yanabidi yatatuliwe kama janga. Huwezi sikia neno michakato, au tuko mbioni katika ilani za uchaguzi lakini ifikapo utekelezaji wa ilani hizo ni kama vile habari ya mtoto na peremende. Maoni yangu kwa wananchi wa igunga ni kwamba wawe makini na viongozi ambao kauli mbio yao ni michakto, tume, kamati, na tuko mbioni hata katika majanga kama njaa, mafuriko, milipuko, na mengine kama ya umeme na barabara.
   
Loading...