Rodrick Mushi
Member
- Jan 24, 2014
- 27
- 10
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mkoani Kilimanjaro leo kinafanya uchaguzi wake kuwachagua viongozi ngazi ya mkoa akiwemo mwenyekiti wa chama Mkoa ambayo inatetewa na mbunge wa Moshi mjini Philemoni aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo.
Uchaguzi unasimamiwa na mbunge wa Karatu mchungaji Natse pamoja na mwenyekit wa CHADEMA Arusha ndugu Golugwa.
Mpaka sasa Ndesa hana mpinzani baada Mbunge wa Rombo Joseph Selasin kudaiwa kujiondoa kwenye kinyanganyiro hicho.
Ndesamburo alisema kuwa yeye kugombea nafasi hiyo hakuzui wagombea wengine kujitokeza kuchuana naye hivyo wajitokeze, ni haki yao kikatiba, na wanachama ndiyo wenye maamuzi ya mwisho.
Katika uchaguzi huo nafasi ya Katibu wa Chadema Mkoa waliochukua fomu ni Bazil Lema anayeteeta nafasi yake,huku akipata upinzani mkali kwa Richard Mtui aliyekuwa katibu wa mbunge wa jimbo la Hai Freeman Mbowe.
Kwa upande wa Uenyekiti wa- Baraza la Wanawake Chadema(BAWACHA) waliochukua fomu ya kugombea uongozi ni ni Mbunge wa Viyi Maalumu
Grace Kiwelu,pamoja na Asha Mashaka,nafasi ya Katibu ndo wanaomba kura kuna Helga Mchomvu,Hawa Mushi pamoja na Ovena Komero ambaye ametangaza kujitoa muda huu.
Nafasi ya Mwenyekiti wa baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) waliochukua fomu ni Liston kibona, Rojas pamoja na Emanuel Saro,ambapo kila upande unajitahidi kujenga ushawishi kwa wapiga kura- ili kuhakikisha
wanaibuka na ushindi.
Nitaendelea kuwapa update ya kinachoendelea pamoja na picha.