Nimedokezwa hali si shwari kwa CCM katika kampeni za uchaguzi mdogo zinazoendelea Kata ya Nyasura iliyopo jimbo la Waziri Steven Wassira wa CCM mjini Bunda mkoa Mara, kwamba CHADEMA haishikiki huko. Nimetonywa majuzijuzi mkutano wa chama hicho tawala ulisambaratika saa 10 jioni kwa kile kinachodaiwa kuhudhuriwa na raia kiduchu. Aliyepo huko Bunda atujuze ukweli ulivyo tafadhali.