Uchaguzi Arumeru Vs Ufunguaji vyuo vikuu

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Joined
Sep 7, 2011
Posts
3,295
Reaction score
2,505
Taarifa nilizozipata kutoka kwenye chanzo changu cha kuaminika zinaeleza kuwa kutokana na serikali kukumbwa na ukata mkali, imeamua kuchukua fedha zilizokuwa zipelekwe bodi ya mikopo, na badala yake fedha hizo zimeelekezwa Arumeru kugharamia uchaguzi mdogo wa ubunge.

Kutokana na uamuzi huo, sasa serikali imeamua kusitisha ufunguaji wa vyuo vya elimu ya juu kwasababu bodi ya mikopo haitakuwa na fedha za kuwalipa wanafunzi hao ili waweze kujikimu. Na kwa kuanzia, tayari wanafunzi wa UDSM ambao walikuwa wafungue chuo chao wiki ijayo wametangaziwa wasiripoti chuoni HADI HAPO ITAKAPOTANGAZWA TENA!

Hii inamaanisha kuwa serikali haijui lini itapata fungu jingine kwa ajili ya kulipeleka bodi ya mikopo na kuwawezesha wanafunzi hao kurejea vyuoni. Uamuni huu wa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kuendelea na likizo zao kwa lazima huenda ukavikumba pia vyuo vingine vya elimu ya juu hapa nchini kwa sababu hizohizo.

Narudia tena. Taarifa hizi nimezipata kutoka kwenye chanzo changu cha kuaminika sana ndani ya SERIKALI!
 
Cha kujiuliza ni mabilioni kiasi gani yamepangwa kutumika Arumeru hadi kuathiri vyuo vyetu kiasi hiki????
 
Serikali lege lege isiyoweza kukusanya kodi!. Au wanaogopa wasomi wanaosoma arusha watapiga kura!, serikali hii ni janga la Taifa
 
Serikali lege lege isiyoweza kukusanya kodi!. Au wanaogopa wasomi wanaosoma arusha watapiga kura!, serikali hii ni janga la Taifa

Kodi wanakusanya sana tu, tatizo bwana mkubwa anazitumia safarini si unajua amepita juu kwa juu tola London to Gaborone!
 

hapana mkuu, hii ina maana serikali ina pesa ya kampeni za ubunge lakini haina pesa za kusomesha, pias erikali ina pesa za safari za rais lakini haina pesa za kuboresha elimu

hatuiishii hapo, serikali ina pesa za kulipa wabunge kwenda kukoroma bungeni lakini haina pesa za kulipa watuw asome

hatuishii hapo.... nk
 
Unamaanisha CCM wameshashinda uchaguzi Arumeru kwa kutumia pesa za mikopo ya masomo ya vyuo vikuu? au sio?
 
Janja hii ilitumika hata Udom last election---chuo chenye idadi kubwa
wanachelewesha kufungua kwa visingizio kadhaa kuwatwist akili lakini ukweli ni kuwa wanapunguza idadi ya wapiga kura wa upinzani kwani wanachuo wengi wamejiandikisha vituo vyao ikiwa ni chuoni na kwakuwa wengi ni damu changa wanamageuzi ni mwiba kwa chama tawala.AMINI
 
Huyu jamaa inaonekana amekukera sana mkuu, msamehe hajui atendalo. Back to topic, ikiwa mtoa habari chanzo chake kitakuwa sahihi hali hiyo itakuwa inatisha sana. Kwa mujibu wa Tendwa uchaguzi mmoja unaweza kugharimu mpaka 19bl, sasa kwa tabia ya CCM kuendekeza rushwa itahitaji 5bl kwa ajili ya ushindi, jumla 24bl.
Swali je vyuo vikifunguliwa ni bilion ngapi zinahitajika? Nadhani ni zaidi ya 24bl, hivyo natilia mashaka chanzo cha mshikaji ingawaje sipuuzii habari hii.
 
kwikwi teh teh teh. Magwanda wanapokuja na jazba na matusi wakijuwa matokeo ni yepi. Igunga, Uzini na sasa Arumeru.

Hata mkitukana, bado nyinyi ni vichinchiri ru, mtatafuta kila sababu, mara pesa za chuoni, mara za madrassa, mara wamehonga, mara matusi. Kule kama ni Mombasa tungesema "Munkula huu".
 
Inaweza kuwa kweli. Nachojua CCM wanahangaika kuhakikisha kwamba vyuo vikuu vya Arumeru winafungwa wakati wa uchaguzi. Wanafunzi wote hawaipigii kura CCM.
 
Vyovyote watakavyo amua kufanya hata kama nikwamanufaa yao leo wajue na kutambua athari zake ni kwa watoto na vizazi vyao baadae kwasababu hata matatizo tunayo kabiliana nayo leo hii nikutokana na mfumo wa elimu uliokuwepo awali kwamba watoto wa viongozi na watu maarufu wa wakati hu ndio walio pata elimu hata kama haikuwa bora wala ya manufaa kwao na ndio hao wanaotuumiza leo kwa uongozi uliofana na wawazazi wao.
 
Hili la kufunga vyuo ni la kimkakati wa ushindi kuliko ukosefu wa fedha za kuendeshea vyuo. Bilioni 20 zikipelekwa Arumeru kwa ajili ya uchaguzi wakati TRA wanakusanya mamia ya mabilioni kwa mwezi haziwezi kuathiri mipango ya uendeshaji wa vyuo!!
 
Kodi wanakusanya sana tu, tatizo bwana mkubwa anazitumia safarini si unajua amepita juu kwa juu tola London to Gaborone!

Hiyo juu kwa ju ndo zile fly over alizosema atawajengea anazijaribu kama zitafaa
 

Matatizo ya rasilimali za kata ni yaleyale, sasa sijui yameingiaje huku serikali kuu. MUKANDARA ni fake leader
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…