Uchaguzi 2020 Uchaguzi 2020: Sioni hoja za Magufuli na CCM kutushawishi Watanzania tuwachague tena!

hivi huko upinzani mna hoja gani inayowabeba mpaka sasa; hoja yenu kuu ya ufisadi mlishaiua na muasisi wake kawakimbia kwa sasa yuko upande mwingine.
kwel we n stroke,mtu anajadili ishu ya maendeleo we unaweka hoj ya upnzan isiyo na kichwa,ama kwel ukiwa fisiem sifa kubwa n kua punguan
 
Wafanyakazi hawataweza kuongezewa mshahara kwa sababu serikali imeshindwa kuwa na uchumi imara unaoweza kuzalisha Fedha za kuwalipa.badala yake fedha kidogo zinazopatikana bahati mbaya CCM imezielekeaza kwenye umalaya wa kisiasa ikiamini inajijenga lakini wenye akili tunajua ndo inajimaliza. Poleni watanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 

NASIMAMA NA RAISI DR JOHN POMBE MAGUFULI
Sababu za JPM kupewa kura za Kishindo 2020:

1.Uchumi - Tumeshuhudia kasi kubwa ya ukuaji wa uchumi ktk kipindi cha uongozi wa JPM,Tanzania ni nchi inayoongoza kwa ukuaji wa uchumi ktk nchi za Afrika Mashariki.
2.Taifa kujiendesha kiuchumi- Pato la Taifa limeongezeka na kuipa uwezo mkubwa Serikali yetu ya awamu ya Tano kuweza kutekeleza miradi mingi mikubwa ya kimaendeleo kwa kutumia vyanzo vyetu vya kifedha vya ndani.
3.Biashara - Biashara ndogo na za kati zimekuwa kwa kasi,hii imetokana na mikakati thabiti ya kuondoa urasimu ktk uanzishwaji na uendeshaji wa Biashara.Maagizo ya JPM yalitoa chachu kwa BRELA na TIC kujitathmini upya ktk utendaji wao.
4.Uvuvi - Tumeshuhudia uimarishwaji mkubwa wa Mamlaka zinazohusika na uvuvi ktk bahari,maziwa,mito na mabwawa..Wavuvi wamewezeshwa kinyenzo na kimafunzo kupitia program maalum,pia uvuvi haramu umethibitiwa kwa kiasi kikubwa.
5.Ulinzi na Usalama - Vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama vimeimarishwa kimfumo na kitaasisi hivyo kupelekea hali ya Usalama kuimarika zaidi.Tanzania ni nchi inayoongoza kwa Usalama ktk nchi za Afrika Mashariki na ni Mjumbe mwenye heshima kubwa katika baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
6.Rushwa - Hili halihitaji maelezo,kila mtanzania anajua na anashuhudia nia na uwajibikaji wa Raisi wetu dhidi ya vitendo vya Rushwa,Ufisadi na Uhujumu Uchumi.
7.Kodi - Mfumo wa Kodi umeimarishwa ktk serikali ya JPM.Kila Mtanzania anao wajibu wa kulipa kodi kwa maendeleo ya Taifa letu,tumeshuhudia kuondolewa kwa kodi na ushuru kwa wafanyabiashara ndogo ndogo,hii imefanyika kwa kuanzishwa kwa mfumo rasmi wa kuwatambua pamoja na kuwapa Vitambulisho.
8.Demokrasia na Uzalendo- Demokrasia na Uzalendo wa kweli vimeimarika ktk nchi yetu ya Tanzania.
9.Sera ya Viwanda - Raisi Magufuli ameisimamia kivitendo zaidi Sera ya Tanzania ya Viwanda.Tumeshuhudia Viwanda vingi vikianzishwa na kuimarika zaidi ktk kipindi cha uongozi wa Raising wetu Dr John Pombe Magufuli.
10.Elimu- Sera ya Elimu Bure imefanikiwa kwa kiasi kikubwa na jitihada zaidi zinaendelea kufanyika ktk kuboresha sekta ya Elimu kuanzia ngazi za Shule ya msingi hadi Chuo Kikuu.
11.Maji- Huduma za Maji zimeimarika zaidi kwa kuzipa nguvu zaidi Mamlaka za Maji kujiendesha kibiashara chini ya Usimamizi wa Wizara ya Maji.Pili azimio la uanzishwaji wa Wakala wa Maji Vijijini chini ya uongozi wa JPM litaleta tija zaidi ktk kufikisha huduma za Maji kwa Watanzania
12.Huduma za Nishati - TANESCO na REA wameendelea kufanya vizur ktk kuwahudumia wananchi,pia tunashuhudia utekelezaji wa mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme wa STIEGLERS GORGE na mingine inayofanana na hii,yote hii ni katika kuhakikisha Nishati ya Uhakika inapatikana kwa Wa Tanzania.
13.Miundombinu - JPM ameleta kasi zaidi ktk kuboresha Miundombinu ya nchi,mahsusi ktk kusaidia ukuaji na uendeshaji wa sekta nyingine za kiuchumi.
14.Afya - Kazi kubwa imefanyika ktk kuboresha sekta ya Afya na jitihada zaidi zinaendelea ktk sekta hii muhimu kwa Taifa letu la Tanzania.
15.Umoja wa Kitaifa na Muungano- Hivi vimeimarika zaidi ktk uongozi wa Raisi wetu Dr John Pombe Magufuli.

NASIMAMA NA RAISI DR JOHN POMBE MAGUFULI

Imeandikwa na :
Engineer Yohana Mlaguzi,MSc.
Mhandisi wa Migodi,Miundombinu na Viwanda + Milki Kuu.
+255 717372262
 
Upinzani kuna hoja gani unaiona?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…