Uchafu wawatesa wakazi wa Kihonda

Jicho la Tai

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
1,449
574
WANANCHI wa Kata ya Kihonda Maghorofani, Manispaa ya Morogoro wameutaka uongozi wa Manispaa hiyo, hususani Idara ya Afya kuwaondolea kero sugu ya dampo lisilo rasmi la uchafu uliozagaa kwa muda wa miezi mitatu eneo la Mtaa wa Mbuyuni, hali inayohatarisha kutokea kwa magonjwa ya mlipuko. Hatua hiyo inatokana na kitendo cha Idara ya Afya ya Manispaa hiyo kushindwa kuondoa uchafu huo licha ya kulipwa Sh 120,000 kutoka uongozi wa Kikundi Kazi cha Twende Pamoja mara baada ya kuzikusanya kutoka majumbani mwa watu. Katibu wa Kikundi Kazi hicho, Alfred Gabriel, alisema hayo juzi eneo la Mtaa wa Mbuyuni katika taarifa yake kwa Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood, aliyefanya ziara eneo hilo ili kuhamasisha shughuli za maendeleo. Eneo hili ni la wazi, tuliuomba uongozi wa Serikali ya Kata ili tuweke kituo cha muda baketi la kuweka uchafu ambao baada ya kujaa, Idara ya Afya ya Manispaa itafika kuchukua hapa na kwenda kutupa dampo kuu, alisema kiongozi wa kikundi hicho. Yapo makubaliano ya kulipia gharama za usombaji kwa Idara ya Afya Sh 120,000, tumelipa huu ni mwezi wa tatu taka hazijaondolewa, sasa pamegeuka ni dampo na harufu ni kali ya uchafu, mvua zikianza kunyesha hofu yetu ni kutokea magonjwa ya mlipuko, alisema Gabriel. Hivyo aliuomba uongozi wa Manispaa kufuatilia kwa karibu utendaji wa Idara hiyo hasa katika maeneo ya pembezoni mwa mji ili kuhakikisha kero za wananchi zinaondolewa ikiwemo ya kusombewa uchafu kwa wakati. Kwa upande wao, Ofisa Afya wa Kata hiyo, Peter Ilesha na Ofisa Mtendaji wa Kata, Sheru Bonaventura, walikiri uchafu huo kurundikana eneo hilo kwa muda mrefu licha ya kikundi hicho kulipia gharama za kusombewa taka hizo. Akijibu baadhi ya kero za wananchi wa Kata hiyo, Mbunge wa Jimbo hilo, Abood, alimtaka Ofisa Afya wa Kata hiyo kuhakikisha uchafu huo unaondolewa ndani ya wiki moja kuanzia Oktoba 16, mwaka huu
 
Back
Top Bottom