Uchafu unavyotia doa utalii Bagamoyo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchafu unavyotia doa utalii Bagamoyo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jun 23, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Na Charles Kayoka
  Wiki iliopita nilikuwa ziarani Bagamoyo. Nilifika katika mgahawa mmoja ambao ulionekakuwa msafi. Tulikuwa wengi. Siku ya kwanza mmoja wetu aliwauliza wahudumu kama kuna huduma ya maliwato, lakini aliambiwa hakuna. Choo kilikuwa kimefungwa.


  Siku ya pili mwenzetu mwingine aliulizia huduma hiyo lakini alijibiwa hakuna kwa vile mzee anayehudumia sehemu ya maliwato hakuwapo kazini.


  Mimi pia nilienda stendi kuu ya mabasi na niliambiwa kwamba choo kimefungwa kwa sababu kimefurika na hakuna huduma.


  Mwenzangu alikwenda kichakani nyuma ya karakarana ya magari iliyopo hapo stendi. Wakati akielekea kichakani baadhi ya vijana walimtaka alipe Sh200 ili apate huduma hiyo.


  Mimi nilikimbilia kwenye moja ya vichaka vinavyozunguka bustani ya mchicha iliyoko upande wa pili kituoni hapo.


  Niliona huduma ya choo karibu na stendi kuu ya kituo cha zamani cha mabasi, lakini ubora bado ni wa kiwango cha chini kabisa. Na huu ndio mji wa Bagamoyo, mji unaovutia watalii, wanafunzi, wageni wa mikutano na watafiti kutoka pande zote za duniani.


  Lakini mji wa Bagamoyo hauna choo kinachoaminika kwa matumizi ya umma. Inashangaza zaidi kwenye mgahawa wa chakula hakuna choo na halmashauri ya wilaya inauruhusu mgahawa huo kuendelea kufanya kazi. Wahudumu wanajisaidia wapi?


  Je, wahudumu wanakwenda wapi wakipata tatizo hilo, na wageni watakwenda wapi kama wamekula na wanasumbuliwa na tatizo la tumbo


  Chakula kinaweza kusababisha mtu akaugua ugonjwa wa kipindupindu endapo chakula hakijaandaliwa katika mazingira ya usafi.


  Ni hatari kwa watumiaji wa mgahawa wanaweza kuambikizwa magonjwa mbalimbali kutokana na kutokuwapo kwa huduma ya choo.


  Nilipokuwa katika soko maarufu la samaki wabichi na wa kukaanga niliwaangalia wahudumu wa chakula na nilibaini kwamba eneo hilo halina karo maalumu kwa ajili ya kusafishia vyombo.


  Pia nilibaini kwamba kulikuwa hakuna huduma ya uhakika ya mabomba ya maji kwa ajili ya maji ya kusafishia vyombo, kuogea na kupikia.


  Ni jambo la kawaida kuona watu wakikimbilia nyuma ya majengo ya zamani na vichakani kupata haja. Pia mavazi ya wahudumu yalionekana kuwa machafu na nilibaini kwamba wamekuwa wakivaa sare zao bila kuzifua na kusababisha kinyaa. Wao wenyewe wanaonekana kutapakaa masizi na nguo zao zinanuka moshi na jasho.


  Sufuria hazina viwango vya kutosha vya usafi. Vibanda ni vya nyasi, na mvua ikinyesha ni matope tupu.
  Ni wazi kuwa eneo la soko la samaki ni moja wapo ya kivutio cha utalii. Kwanza sehemu ya kupikia chakula huwa ni sehemu ya wageni ambayo wanapenda kuitembelea ili kujifunza utamaduni na kuonja mapishi ya wenyeji.


  Mazingira machafu yanasababishwa na Halmashauri ya Mji wa Bagamoyo. Nasema hivyo kwa sababu haijaweka mikakati ya kuweka mji huo katika hali ya usafi na kuwavutia watalii zaidi.


  Haiwezekani mji ambao unawavutia watalii na kuiingizia Serikali kupato kikubwa kupuuzwa na kuendelea kuwa mchafu.


  Sifa ya mji uliostaarabika ni usafi. Ninashauri kabisa Serikali ya wilaya ione usafi ni kipaumbele kwa mji wa Bagamoyo ili kuwavutia watalii na kukidhi mahitaji yao hasa usafi wa mazingira.
  mohamedmusta@gmail.com , 0766959349
  http://www.mwananchi.co.tz/makala/31-uchumi/24088-uchafu-unavyotia-doa-utalii-bagamoyo

  Ahh Nyumbani kwetu kumekuwa kuchafu namna hii ahhh Hakuna hata Viongozi wa kutengenea mji mkongwe? Aibu sana.
   
 2. M

  Moony JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,593
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  pengine uchafu ndiyo sifa ya kuja kutazamwa!

  Mi nishawahi kusema UCHAFU Umekithiri, inabidi watendaji wooote waandamizi wa serikali hii waende study tour RWANDA
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Tena ndio nyumbani kwa mkuu wa kaya ambae kwao wanamuita "Mjomba"....anakubali mambo haya??alishasema atajitahidi kufanya bwagamoyo ije iwe manispaa kabla hajashuka kwenye utawala!!ataweza??
   
Loading...