Uchafu maeneo ya NHC Msimbazi

Baba Watoto

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2010
Posts
393
Reaction score
278
Habarini za asabuhi mabibi na mabwana, kama wiki mbili hivi nilibahatika kutembelea jiji la Dar es salaam kutoka huku bushi kwetu kwa kina Bujibuji.

Nilishangazwa na muonekano mpya wa jiji kuanzia unaingia huku kibamba hadi mjini kati kabisaaa.

Kikichonishtua zaidi ni namna Wadaslam wanavyoishi, nilienda kumuona jamaa yangu anaekaa maeneo ya Msimbazi pale, karibu na baa ya sabasaba. Ni aibu kwa NHC ni aibu kwa wahusika wa usafi wa manispaa na jiji kwa ujumla. Aibu zaidi kwa mabwana na bibi afya, hakuna kinachozingatiwa, hasa nyakati za usiku na wapo watu wanauza chakula na kuchoma mishkaki. Muda mwingi nilikua ghorofani dirishani nikiangalia heka heka za Wadaslam, huyo mchoma mishkaki anazunguka kwenye pipa la taka kukojoa na kurudi na kuendelea kuchoma bila kunawa, wapo wanaofanya matusi kwenye transfoma upande wa baa na vyoo vya baa ambavyo vinanuka balaaa.

Nikamuuliza mwenyeji wangu. Vipi hali hii? Akasema ndugu yangu acha tuuu, tumehangaika kila namna, maana kero tunayopata wakazi wa hapa ni kubwa, kuanzia moshi, kelele, harufu ya uchafu na kadhia zote unazozijua kutokana na hali hii. Nilichomshauri tuuu, ni kuwa aje kijijini nitampa hekari nzima ajenge hekalu lake akae. Sio kwa shida na karaha hizi, ia Wadaslam mnayaweza kwa kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baba Watoto fasta rudi huku kwetu bush..... ukikaa huko utaambulia kufanya matusi kwenye transfoma halafu ukarudi kwenye kiroba cha Coco Beach
Hawa Wadaslamu watu wa ajabu sana, nilitamani sana nimsaidie rafiki yangu lakini mm mgeni bwana nimeondoka nimemuacha na kero zake. Nilipanda zile mwendokasi zao aiseee, daaaaaaah. Niliminywa kiasi ilinilazimu kushuka magomeni nitembee hadi Ubungo. Hewa nzito balaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…