Uchafu katika miji yetu nayo ni siasa?

Uchafu katika miji yetu nayo ni siasa?

Nyami2010

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
227
Reaction score
50
Ndg wana JF

Kwa nini miaka yote, miji yetu ni michafu kiasi hiki? Kipindupindu....imagine!

Leo asubuhi, Radio One wametangaza hali ya uchafu katika Jiji la Arusha nimeogopa. Dar, Moro, Tanga, n.k usiseme!

Hivi, uchafu ni tabia au ni kushindwa kwa wahusika kuchukua hatua?

Nini kifanyike?
 
Hapa wananchi na viongozi wa mitaa ndio wa kulaumiwa!
 
Kwanza ni uzembe wa serikali kupitia wizara yake ya afya kutokufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa usafi wa mazingira. Pili wananchi kutokuwa na mwamko na moyo wa kujituma kutunza mazingira yao, hapa serikali inalo jukumu la kutoa elimu ya usafi na pia kuweka sheria kali wa wachafuzi wa mazingira.
 
hatun hulka ya kuwajibishana/, tunahamishana tu vituo, s hakuna mchawi hapa
 
Kwani Manispaa za Moshi na Iringa mbona wanajitahidi? Kulikoni, Arusha, Dar ni kwingineko? Au siasa zinatupeleka huko?
 
Hapa wananchi na viongozi wa mitaa ndio wa kulaumiwa!

Kama wananchi ndo wakulaumiwa basi tuanze kujilaumu sisi kwanza. Si wananchi bhana??????????????
Lakini hebu tuanzie kwakwo.
 
Back
Top Bottom