UBUNGO MATAA KUMEKUWA PANGO LA WANYANGANYI Tarehe 12 Desemba 2011 nilichelewa kutoka katika mihangaiko ya maisha yangu mpaka kwenye saa mbili usiku. Kwakuwa mimi ni mwenyeji wa Kibaha na kesho yake tarehe 13 Desemba 2011 nilitakiwa kuwahi kwenye majukumu. Basi ilinibidi kulala kwa rafiki yangu mitaa ya Ubungo Kibangu. Wakati wa kuelekea Ubungo Kibangu nilipita mitaa ya Ubungo Mataa kunakokuwa na biashara nyingi ndogondogo. Kila mtu alikuwa bize na maisha yake wa kununua akinunua, wa kuuza akiuza, na wale waliokuwa wanapita kuelekea makwao wakifanya hivyo. Kutokana na kazi zangu kuwa za kitafiti, ghafla nilipata wazo la kufanya utafiti mdogo kuhusiana na maisha ya eneo hili. 1. Kwanza niligundua kuwa kuna dhuluma kubwa inafanywa na baadhi ya vijana wababe ya kutoza ushuru wafanyabiashara wadogowadogo hasa akina Mama Ntilie ambao hawana uwezo wa kutunishiana misuli. a. Katika suala la ushuru niligundua wale wababe hawalipi chochote lakini wale wanyonge kila siku wanalipa zaidi ya shilingi 2,000/=2. Pili, niligundua baadhi ya vijana wanaovizia watu wanapokuwa wamebanwa na haja ndogo na kujisaidia pembezoni mwa. Hili ndio jambo lililonidhi kuliko yote kutokana na kuwa vijana hawa wahuni wanajificha kwa lengo la kuvizia anayejisaidia halafu wanamtoza pesa kiasi wanachotaka waoa. Nilichogundua vijana hawa wahuni wanajifanya wamewekwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kusimamia usafi kwa kushirikiana na kituo cha polisi cha Ubungo Terminalb. Faini ya kujisaidia ni shilingi 50,000/= ingawa ikiwa una nguvu ya mabishano na msuli wa kusimama nao hata shilingi 5,000 inakubalikac. Cha kushangaza hakuna mabango yoyote yanayoonyesha kuwa ni marufuku kujisadia maeneo hayod. Pia vijana hawa hawana mavazi yoyote rasmi ya kujitambulisha kuwa wao wana jukumu Fulani. Ni vijana waliokaa kihuni na kuvaa kaoshi chafu na ni wachafu kwa ujumla na wavuta bangi3. Jambo jingine nililogundua ni suala la wizi mdogomdogo maeneo hayo hasa unaowakumba akina dada hasa maeneo ya bonde la Songas ambapo vijana wa kihuni na wavuta kambi wameweka makazi yaoa. Ni eneo hatari kupita baada ya saa mbili usikuRAI YANGU KWA SERIKALI IWE MAKINI KATIKA KUWEKA TARATIBU AMBAZO ZITAFUATWA NA KILA MWANANCHI. HII NCHI INAELEKEA PABAYA HATA KAMA NI SUALA LA UGUMU WA MAISHA BASI ISIWE NDIO BAADHI YA WATU KUISHI KIJANJA NA KUDHULUMU WENGINE MALI NA UHAI WAO.