Ubunge viti maalumu, hesabu zipoje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubunge viti maalumu, hesabu zipoje?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MpigaFilimbi, Jul 30, 2010.

 1. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2010
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Wakuu,
  Nimekuwa nikisikia harakati zinazoendelea huko CCM kuhusu kuwania viti maalumu wanawake, walemavu, vijana, wafanyakazi na zingine. Inavyoonyesha karibu kila mkoa wanatoa washindi wawili ambao wanatangazwa kuwa wameshinda viti maalumu. Sielewi hizi hesabu zinaendaje, hasa ukizingatia kuwa idadi ya mikoa ya Tanzania na idara zote zilizopo CCM, hainiingia akilini kuwa tunahitaji kuwa na wabunge wote hao kwa fedha za walipa kodi ambao kimsingi hakuna wanachokifanya zaidi ya kuongeza uwingi au kura za CCM.
  Nilichokuwa najua ni kuwa viti maalumu vinatolewa kutokana na asilimia ya wabunge ambao chama husika inapata katika uchaguzi mkuu, inakuwaje hao wanatangazwa washindi wakati hawajui kwa yakini hicho chama chao kitapata asilimia ngapi ya wabunge kwenye uchaguzi ujao? Inawezekana ninakosa facts, mwenye ufafanuzi tafadhali....
   
 2. Kamaka

  Kamaka JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 565
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wakuu, mmeulizwa tuna uchu wa kufahamu
   
 3. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  mwisho wa siku uamuzi wa mwisho utatokana na idadi ya wabunge wa kuchaguliwa waliopatikana na idadi ya kura za urais za chama husika. so hayo ni maendekezo ya awali tu
   
Loading...