Mkuu Kingi,
Ukiona mtu ametangaza kuwania Ubunge jimbo fulani ni kwamba anaangalia ni wapi anakubalika zaidi na je uwezekano wa kushinda ukoje. Hayo majimbo mengine uliyoyataja yawezekana Nape hakubaliki na hata akienda kugombea huko haoni kama anaweza kushinda.
Kwani hujajiuliza ni kwanini Fred Mpendazoe ameamua kugombea jimbo la Dar wakati miaka 5 inayoisha alikuwa anawakilisha Jimbo la Kishapu?
Waache wachuane, ingawa nina mashaka sana kama jina la Nape linaweza kuvuka kwenye vikao vya chama. Misuguano iliyotokea ndani ya UVCCM na kupelekea kijana kumwaga kila kitu hadharani kuhusu ufisadi wa upangishaji wa Jengo la UVCCM Makao Makuu, ambao unamgusa moja kwa moja EL unaweka mashaka kama kijana anaweza kupenya.