Ubunge jimbo la Segerea

Ubunge jimbo la Segerea

mzalendo8

Member
Joined
Mar 19, 2015
Posts
26
Reaction score
9
NIA YA WAZI YA KUOMBA RIDHAA YA KUGOMBEA NAFASI YA UBUNGE OKTOBA 2015 JIMBO LA SEGEREA DAR ES SALAAM.

Na: BARAKA IBRAHIM
OMARI

Baada ya kutafakari kwa kina kuhusu hali ya WATANZANIA katika nchi yetu ukilinganisha na hali ya KISIASA tuliyonayo sasa nimefikia MAAMUZI ya KUOMBA RIDHAA YA CHAMA CHA MAPINDUZI (C.C.M) ili kuwania nafasi ya UBUNGE jimbo la SEGEREA mkoani Dar es Salaam kupitia chama hiki.

Maamuzi haya yamekuja baada ya Ushawishi nilioupata kwa kushawishiwa na watu na kwa kujionea hali halisi ya WATANZANIA kwa kuzingatia uhitaji wa WANANCHI hasa vijana wenzangu ambao ndio RASILIMALI muhimu ya taifa ukizingatia na uwezo wangu binafsi ninaouamini katika utendaji.

Ninaamini kuwa mimi BARAKA OMARI niliyezaliwa miaka 25 iliyopita mkoani kigoma na mkazi wa muda mrefu wa TABATA ni kijana niliyekulia mtaani katika hali ya kawaida sana na makazi haya yameniweka katika mazingira yaliyonifanya nijifunze mambo mengi ambayo kimsingi ndiyo yanayounda maisha halisi ya MTANZANIA katika nyanja kama ELIMU, MICHEZO, MIUNDOMBINU, HUDUMA ZA JAMII kama MAJI, AFYA na UMEME.

Maisha niliyopitia yamenifanya kubaini kuwa wako watanzania wengi tunaoishi katika hali ya UNYONGE kwa kukosa vipaumbele vyao katika maisha kama nimevyosema awali. Hii imenifanya kuamini kuwa mimi ni sehemu ya SULUHISHO la matatizo haya yanayowakabili WATANZANIA.

Ninaamini kuwa kupitia nafasi ya UBUNGE itakuwa nafasi kubwa ya KUPAZA SAUTI za WANYONGE tulio wengi ili kutafuta ufumbuzi wake kwa njia stahiki.

Kwa WATANZANIA wa jimbo la SEGEREA nimegundua ziko fursa nyingi ambazo tumepewa kama urithi na tunaweza kuzitumia ili kujikwamua katika maendeleo mfano Biashara, elimu, usafiri, Afya, miundombinu ya barabara na makazi.

Uzoefu nilioupata katika maisha ya uongozi niliyopitia tangu nikiwa mbunge na waziri wa serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha Dar es Salaa kama Waziri katika dhamana za Habari na Mawasiliano (2013), Fedha na uwekezaji (2014) na Naibu Waziri Maji na mazingira (2013). Pia Waziri wa Mipango na uzalishaji (2009 ~ 2010) KIBAHA Sekondari ulinisaidia KUPAMBANA na changamoto zinazowakabili watu katika maeneo husika hata kufanya MABADILIKO makubwa yaliyopelekea kuweka historia na LEGACY kwangu kwa KUPAMBANA na WAHUJUMU UCHUMI ambao walifikia hatua ya kunyoosha mikono na kutafuta mbinu KANDAMIZI ya kupambana na mimi KITAALUMA na KIBINAFSI kwa kutumia MADARAKA waliyonayo.

Nafasi hizi za UONGOZI zimenipatia fursa na mwanya wa kushiriki mikutano na midahalo mbalimbali ya KISIASA na KIDIPLOMASIA huku nikiongeza UWEZO wa kuzungumza na KUJENGA HOJA katika maeneo husika. Sambamba na hilo nimepata UZOEFU wa kuhudhuria mikutano na Vikao mbalimbali nikiwa kama mjumbe wa Baraza la Shule kibaha (BASHUKI), Kamati ya Nidhamu na Ustawi wa Shule Kubaha.

Pia nimepata fursa za kushiriki BARAZA LA CHUO UDSM (University Council), Kamati ya Mipango na Fedha (Finance and planning Comittee) ya Chuo, Investment and Resource Mibilization (IRM) na Senate of UNDERGRADUATE comittee. Katika mikutano na vikao vyote hivi ilinipa nafasi ya KUTETEA na KUSIMAMIA maslahi ya walionituma na kusababisha matokeo makubwa (Impact) ambayo ilisababisha mabadiliko na mustakabali wa maisha yangu ya kitaaluma na binafsi chuoni.

Hii imenipa UJASIRI na KUJIAMINI kuwa kwa hakika niko tayari KUWATETEA na KUWATUMIKIA watanzania katika hali zote bila woga, kuyumbishwa au kurudi nyuma. Bila kusahau uzoefu wa kukaa katika BUNGE la chuo kikuu cha Dar ea Salaam (DARUSO) ambapo nimepata fursa ya kujifunza nini hasa DHIMA kuu ya MBUNGE kwa WANANCHI waliomtuma na Bunge lenyewe.

Hivyo basi mimi, BARAKA IBRAHIM OMARI nikiwa na nia ya dhati kabisa na moyo wa uhodari wa kuwatumikia WATANZANIA naomba kutangaza wazi kuwa NINAKUSUDIA KUCHUKUA FOMU ya kuomba ridhaa ya kugombea UBUNGE jimbo la SEGEREA kupitia CHAMA CHA MAPINDUZI kadiri ya UTARATIBU ULIOWEKWA na chama.

Ninaomba Ushirikiano wenu WATANZANIA katika USHAURI, HALI na MALI hata KUNISEMEA PIA ili kuyafikia malengo na makusudio ambayo binafsi ninaamini ni yetu wote.

Mwisho, ninaomba KUWAPONGEZA vijana wenzangu wote waliokwisha kutangaza nia za kuwania nafasi za UONGOZI kupitia vyama mbalimbali huku nikiamini kuwa wamejipima na wanao uwezo wa kuwatumikia WATANZANIA wote.

ASANTENI SANA.
 
kama ni ccm umepotea....mi ni mpiga kura wa jimbo husika..
 
I beg to reserve my comments.

Tiba
 
Mkuu una kipato halali cha kuendesha maisha au unategemea ukatimize ndoto zako bungeni?

Kwanini umeamua kupitia CCM?Unakubaliana na sera za ufisadi na kulindana zilizotamalaki CCM

Mbunge aliyetangulia amekosea wapi ambapo wewe utarekebisha?

Kwani hauwezi kuwasaidia wanaSegerea kwa namna nyingine yoyote hadi uwe mbunge?
 
Back
Top Bottom