Wanajamvi,
Mimi nimekumbana na huduma mbovu sijawahi kuona katika chombo cha kutoa huduma,nmekuwa nikiona watu wanalalamika kuhusu makato ya Airtel yatosha lakini kwa vile ilikuwa haijanitokea hata sikuelewa ni nini wanakiongelea. Ni kama wiki moja sasa imepita niliweka kwenye simu yangu pesa na nikaamua kununua bundle la wiki cha ajabu hela ikakatwa lakini nikawa siwezi kuingia kwenye internet nikaangalia salio nikakuta nina 0 byte nikaamua kujiunga tena kwa wiki mambo yakwa yaleyale. Nikaacha kwa siku hiyo nikajipa matumaini kuwa labda ni matatizo ya network kesho yake nitarudishiwa peasa au nitapewa bundle niendelee lakini kimya,kesho yake tena nikajiunga kwa 4999 lakini bado nikajikuta na sifuri! Nikapiga 100 huduma kwa wateja nilichokipta sipendi kuamini kuwa airtel ni "Customer centric" oriented company......nilisubirishwa kwa muda wa masaa 3.28 huku nikiambiwa wahudumu wetu wanahudumia wateja wengine watakuhudumia punde wakimaliza na nisikate simu kwa vile itanichukua muda kuhudumiwa. Niliamua kukata baada ya msaa hayo 3.28, baada ya siku moja nikapiga tena nikasubirishwa kwa zaidi ya lisaa bila kupata hudum. Nikamueleza mtu mmoja bahati nzuri yeye ni kati ya wateja ambao ni "Premium Customers" akapiga yeye na ndani ya nusu dakika akawa amejibiwa ndo nikaeleza shida yangu kwa mdada wa huduma kwa wateja akasema subiri kidogo akahamisha simu ambapo haikupokelewa tena! Yule mwenye simu akaamua kukata akwa ameshakasirika akapiga tena ikapokelewa na mkaka nikasema shida yangu akaulizia particulars zote akasema atanipigia muda si mrefu,hakupiga simu mpaka niandikapo. Baada ya siku mbili yule rafiki yangu "Premium Customer" akapiga tena huduma kwa wateja akaambiwa hilo ni "TATIZO LA KITAIFA" kuwa ni simu nyingi zinapata hilo tatizo.Nikabaki nimeduwaa....Hivi airtel an internationa company linashindwa kuwa na IT team ambayo inauwezo wa kutatua tatizo la system misbehaviour kwa zaidi ya wiki! au ndo out sourcing........Mpaka leo nimeamua kuachana na line ya airtel na kujiunga na Vodacom ambao waliwahi kupata tatizo linaloshabihiana na hili wakati mtambo wao ulivoungua lakini tulirudishiwa hela zetu ndani ya siku mbili na kuombwa samahani......ndugu zangu hawa nawaombeni mfute dawati la customer service kwa kuwa halina umuhimu kwetu.
Nawasilisha.