Habari wakuu,
Kilio changu naomba niungwe mkono na wakazi wote pamoja na watumiaji wa barabara ya Mbezi kwenda Makabe kupitia katika viunga vyake vyote vya shule ya St Ann's, Madukani, Kwa Brigenda, Post, Njia panda mpaka huko mwisho Makabe. Kilio hiki ni ubovu uliokithiri wa barabara hii. Hasa ukianzia tu pale Mbezi mpaka katika daraja lililosimamiwa na Mh. Mnyika miaka mingi iliyopita wakati akiomba kura zetu na kujituma kwa dhati ili tumpe ubunge.
Lakini naona Mh. Mnyika na diwani hawana tena muda kwa wananchi kuangali mustakabali wa maisha yao hasa katika barabara hii. Ni mbovu sana sana, magari yanaharibika, waenda kwa miguu wanateseka na daladala zinaenda kwa shida. Usafiri unakuwa mgumu sana. Tunakuomba Mh. Mnyika na Diwani mfanye hima kupitisha grader katika barabara hii.
Kura zetuhamtazipata kama mambo ndio hivi.
Rudini kwa wananchi mtuhudumie