Ubinafsishaji wa Magereza

Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,334
988
Wakati Mwl. Nyerere anapinga dhana ya ubinafsishaji alitamka kwamba "watanzania mtajikuta mmebinafsisha hadi magereza".

Kuna habari hapa inayosema kwamba Marekani imeshaanza kubinafsisha magereza muda mrefu sasa. Jimbo la Florida nchini humo ndilo lina gereza kubwa linalomilikiwa na kampuni binafsi (Private Prison).

Nadhani hakuna aisyefahamu kwamba binafsishaji zote zimeanzia hukohuko majuu.
Zinapoteremka huku kwetu kunakuwa na vikelele viwili vitatu lakini hatimaye ni kuzikumbatia.

Source: Soma mwenyewe hapa chini

http://news.yahoo.com/s/nm/20110512/us_nm/us_usa_prisons_florida
 
Ukisoma hiyo makala unakuta kuwa bado kuna upinzani mkubwa wa wazo hilo hapa Marekani. Hata wengine wamediriki kuhama vyama vyao ikiwa hatua hiyo itapitishwa. Kwa sababu kampuni binafsi lengo lake ni kutengeneza faida na si ku-rehabilitate wafungwa. Serikali inaweza ikajikuta inalipa zaidi kwa kampuni binafsi kuliko kuendesha wenyewe magereza hayo.
 
Ukisoma hiyo makala unakuta kuwa bado kuna upinzani mkubwa wa wazo hilo hapa Marekani. Hata wengine wamediriki kuhama vyama vyao ikiwa hatua hiyo itapitishwa. Kwa sababu kampuni binafsi lengo lake ni kutengeneza faida na si ku-rehabilitate wafungwa. Serikali inaweza ikajikuta inalipa zaidi kwa kampuni binafsi kuliko kuendesha wenyewe magereza hayo.

Nimeisoma yote kikamilifu. Kelele zinazopigwa kuhusu ubinafsishaji wa magereza hazifikii hata kidogo kelele za mwaka 1980 wakati Magreth Thatcher alipoanza kukaribisha Privatisation nchini Uingereza.

Ukiingia vitani usitegemee adui yako asikurupuke kukutupia hata risasi mbili hata kama umekuja na nuclear weapon.

Ndiyo maana nimesema vikelele vidogovidogo kama hivi vilikuwepo na kwenye hili vitakuwep lakini mwisho wa siku ni kuukumbatia ubinafsishaji.


Mimi nimesema mwisho wa siku na kelele hizi ubinafsishaji huu utakumbatiwa. Wewe hapa unasemaje?
 
ubinfsishaji umekuwa mbinu kuu kabisa duniani ya kuharakisha maendeleo. huko majuu tunakokwenda kukenua meno wameendelea kwa sababu nyingi ikiwemo ubinafsishaji. mimi ni mtaalamu wa eneno hili so nikipata muda nitawawekea details za kutosha na hata ni kwa nini ubinafsishaji unakwama tz na nchi nyingine za dunia ya tatu.

mawazo ya nyerere yalikuwa ni ya wakati ule ila kwa sasa yanajadilika, tena kirahisi tu! huko unakoita ku-rehabilitate, hata wewe ukitembelea magereza yetu na kuona maisha ya wafungwa utakiri kuwa kule wanaharibiwa zaidi kuliko kuwa-rehabilitate. mtu huingia akiwa na hatia ya uovu lakini akitoka huwa muovu zaidi na aliye sugu kwa uovu akiwa amejaa chiki dhidi ya raia na serikali, asiye na huruma wala utu na uwezekano wa kutenda kosa huwa mkubwa zaidi kwa aliyekwishaonja jela kuliko yule ambaye bado hajalijua jela

mi naunga mkono hata takukuru, BOT, ikulu, polisi nk zibinafsishwe! huenda watapunguza kutufanya mazuzu
 
Back
Top Bottom